WikiLeaks mtusaidie kuwajua wamiliki wa kampuni ya Simba Trust

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
26,030
2,000
Naiomba hii Taasisi itusaidie kuwafichua wamiliki wa hii kampuni maana kwa sisi wazawa naona hili jambo kila mtu analigwaya ingawa nakumbuka kuna mdau mmoja aliwahi lileta hapa mtandaoni siku za nyuma.

Ikiwezekana hata wale waliochota mabilioni pale bank ya Stanbic kwa mifuko ya sandarusi orodha yao nayo muiweke hadharani maana sisi hiyo kazi imetushinda na kilio chetu kimekuwa ni sawa na kilio cha samaki.

Nasema hivi kwasababu naamini Kama mmeweza kufichua ufisadi wa matajiri/viongozi kutoka mataifa makubwa na yenye nguvu duniani, sioni ni nini kitawashinda kufichua taarifa za watu kutoka nchi masikini hizi za ulimwengu wa tatu.

Nachojiuliza hapa ni watu hawa wana nguvu gani kuwashinda mabwana wakubwa wa huko ulaya?

Watanzania mlio ndani na nje ya nchi na wenye access na kampuni hii ya WikiLeaks,fanyeni mawasiliano nao juu ya hili jambo watusaidie maana sisi ni wazi limetushinda ingawa tatizo huenda ni watu kukosa ujasiri tu ila data zote wanazo.
Wikileaks ni taasisi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom