WikiLeaks:Kenya yaifokea Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WikiLeaks:Kenya yaifokea Marekani

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Saint Ivuga, Dec 12, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,784
  Trophy Points: 280
  WikiLeaks:Kenya yaifokea Marekani.


  [​IMG] Raila Odinga


  Serikali ya Kenya imepuuzilia mbali taarifa zilizofichuliwa na tovuti ya Wikileaks ambazo zinamnukuu balozi wa Marekani nchini humo, Micheal Rannenberger, akisema kwamba Rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga ndio kikwazo kikuu katika kuleta mageuzi nchini Kenya.
  Balozi huyo pia alinukuliwa akisema serikali ya Marekani haitasita kuendesha kampeni kupitia makundi ya kiraia ili kuhakikisha mabadiliko yanafanyika.
  [​IMG] Tovuti ya WikiLeaks


  Akizungumza na BBC akiwa jijini London, Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amemshutumu bwana Rannenberger kwa kuwa mnafiki. ''Taarifa zinazotolewa na WikiLeaks ni uvumi mtupu. Yale yote yaliyomo ni masengenyo. Ni watu wanaokusengenya, wanayozungumza kukuhusu hadharani ni tofauti na yale wanayozungumza kisiri,'' akasema bwana Raila.
  Kuhusu madai kuwa yeye na rais Kibaki hawakuchukuwa hatua zozote kwa kutekeleza mageuzi yanayohitajika, ili kuhakikisha kuwa machafuko ya baada ya uchaguzi kama yale yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 yatokee tena bw Raila amesema, '' Bwana Ranneberger anaishi nchini Kenya kama mgeni. Iwapo anataka kutushauri ana haki ya kufanya hivyo. Lakini vile vile wageni ni sharti watuheshimu''.
  Nayo taarifa kutoka ikulu ya rais ya Nairobi imepuuzilia mbali madai hayo ya balozi wa Marekani kwa kusisitiza kuwa rais Mwai Kibaki ana historia nzuri ya kutekeleza mageuzi kwa kufanikisha kuidhinisha kwa katiba mpya ya taifa hilo.
  Taarifa hizo za kisiri, ni miongoni mwa stakabadhi ambazo zimefichuliwa na tovuti ya Wikileaks , kuhusiana na nchi ya Kenya na viongozi wake
  SOURCE:BBC
   
 2. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wikileaks ni noma! Ituvujishie basi na ma-news ya hapa bongo ya kina rowasa na mafisadi wenzake.nadhani sasa hivi wanatetemeka huko waliko.
   
 3. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Hii mbona ipo wazi ila hili balozi aliripoti wakti ule jamaa wansusua kutengeneza katiba mpya!
  Ila bado kuna mwansheria mkuu na mzee wa tume ya rushwa wamerekani wanasema ni vikwazo kwa kurushwa, ha wawataki pia!
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,337
  Likes Received: 418,617
  Trophy Points: 280
  The niggling question for Kenya and the rest of Africa has always been how deep can we bite the very hand that presumably is feeding us?
   
 5. JS

  JS JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yaani naona kama wanachelewa vilee kutuvujishia za bongo..nazisubiri kwa hamu kweli
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  No question about kenya regarding kibaki and raila
   
 7. a

  asagulaga Member

  #7
  Dec 14, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  WikiLeaks inawapumbaza walimwengu, sijaona point yoyote ya maana katika WikiLeaks zaidi ya kuelezea umbea wa wanadiplomasia wa Marekani. Hakuna habari yoyote ambayo ni ya maana na Ulimwengu wa wakati huu. Watu watatumia muda mwingi kusoma WikiLeaks wakati wamarekani wanaendelea kujitanua duniani, isije ikawa WikiLeaks ni wakala wa Marekani na mashirika yake ili kuwapumbaza watu.
   
Loading...