Wikileaks: Julian Assange aruhusiwa kufunga ndoa jela

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Julian Assange amepatiwa ruhusa kumuoa mpenzi wake Stella Moris katika jela ya Belmarsh, BBC imeambiwa.

Mwanzilishi huyo wa mtandao wa Wikileaks na bi Moris wana watoto wawili wa kiume , ambao alisema walipatikana wakati alipokuwa akiishi katika ubalozi wa Ecuador mjini London .

Huduma ya jela hiyo imesema kwamba ombi la bwana Assange liliruhusiwa na gavana wa jela hiyo. Bi Moris alisema kwamba amefurahi kwamba kumekuwa na uelewa.

Aliongezea kwamba : Nadhani hakutakuwa tena na usumbufu mwengine wa ndoa yetu.

Wafungwa wana haki ya kuomba kufunga ndoa wakiwa jela chini ya kifungu cha ndoa cha 1983 na ombi hilo linaporuhusiwa wanapaswa kusimamia gharama zote za ndoa hiyo bila usaidizi wowote wa fedha za umma.

Katika mahojiano na gazeti la Mail la siku ya Jumapili mwaka uliopita , bi Moris , wakili wa Afrika Kusini , alifichua kwamba alikuwa katika uhusiano na bwana Assangetangu 2015na amekuwa akiwalea watoto wao wawili yeye binafsi.

BBC Swahili

1636695883000.gif
 
Ila kwa wenzetu inawezekana ukawekewa utaratibu wa kugegeda
Hata Tz conjugal right ipo kwenye makaratasi.
Namkumbuka yule baba aliyekuwa anapata hasira na kufura kama chura kisa tu akina Sugu wanasikiliza radio wakiwa sero
 
Kumbe bongo inawezekana kuingia segerea na radio yako km mfungwa!! Nilikua sijui
 
Julian Assange amepatiwa ruhusa kumuoa mpenzi wake Stella Moris katika jela ya Belmarsh, BBC imeambiwa.

Mwanzilishi huyo wa mtandao wa Wikileaks na bi Moris wana watoto wawili wa kiume , ambao alisema walipatikana wakati alipokuwa akiishi katika ubalozi wa Ecuador mjini London .

Huduma ya jela hiyo imesema kwamba ombi la bwana Assange liliruhusiwa na gavana wa jela hiyo. Bi Moris alisema kwamba amefurahi kwamba kumekuwa na uelewa.

Aliongezea kwamba : Nadhani hakutakuwa tena na usumbufu mwengine wa ndoa yetu.

Wafungwa wana haki ya kuomba kufunga ndoa wakiwa jela chini ya kifungu cha ndoa cha 1983 na ombi hilo linaporuhusiwa wanapaswa kusimamia gharama zote za ndoa hiyo bila usaidizi wowote wa fedha za umma.

Katika mahojiano na gazeti la Mail la siku ya Jumapili mwaka uliopita , bi Moris , wakili wa Afrika Kusini , alifichua kwamba alikuwa katika uhusiano na bwana Assangetangu 2015na amekuwa akiwalea watoto wao wawili yeye binafsi.

BBC Swahili

View attachment 2007676
Kwenye jela za wenzetu huko
 
Back
Top Bottom