Wikileaks diplomatic cables release 'attack on world'

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,067
2,199
Wakuu internet na teknolojia ia habari vinaendelea kuwatoa kamasi wanasiasa wanafiki. Nadhani kuanzia sasa Hilary Clinton uzuri wako wote utapukutika, by the end of this week nadhani kutakuwa huenda Assange atakuwa katika hatari ya maisha, au wanasiasa wakubwa watapata matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Walijaribu kum-silence jamaa kwa kumsingizia kesi ya ubakaji lakini still ana survive.
 
Ningefurahi sana kama kutakuwa na yoyote inayowataja viongozi wetu.

Imenichekesha sana ya Rais wa Ufaransa kuitwa "mfalme ambaye yuko uchi", na inayolingana na ukweli kuwa Ahmedinejad analinganishwa na Hitler.

Ingekuwa vizuri sana tukijua wanamwitaje rais wetu au wa Zimbabwe.
 
Kuna mwenye link ya kudownload full documents? The guardian uk na new york times wametoa sketch ya information ilivyo, docs nilizonazo zinaonyesha kulikuwa na correspondence 755 kati ya US na Tanzania. Natamani kujua zina information gani
 
Re: Wikileaks - Ukraine in USA Diplomatic mail
TAG
29 Nov 2010 05:13
IP/Host: 193.239.129.---
Cable Viewer

¶6. (S/NF) Finally, Qadhafi relies heavily on his long-time
Ukrainian nurse, Galyna Kolotnytska
, who has been described as a
"voluptuous blonde." Of the rumored staff of four Ukrainian
nurses that cater to the Leader's health and well-being, XXXXXXXXXXX emphasized to multiple Emboffs that Qadhafi
cannot travel without Kolotnytska, as she alone "knows his
routine." When Kolotnytska's late visa application resulted in
her Security Advisory Opinion being received on the day
Qadhafi's party planned to travel to the U.S., the Libyan
Government sent a private jet to ferry her from Libya to
Portugal to meet up with the Leader during his rest-stop. Some
embassy contacts have claimed that Qadhafi and the 38 year-old
Kolotnytska have a romantic relationship
. While he did not
comment on such rumors, a Ukrainian political officer recently
confirmed that the Ukrainian nurses "travel everywhere with the
Leader."

Muammar-420x0.jpg
 
http://http://news.yahoo.com/s/afp/usdiplomacymilitaryinternetwikileakssaudiiran

PARIS (AFP) – King Abdullah of Saudi Arabia urged the United States to attack Iran to destroy its nuclear programme, according to US documents leaked by WikiLeaks and published Sunday by daily newspapers.
According to a leaked US cable, published by the New York Times, King Abdullah bin Abd al-Aziz made the call during an April 2008 meeting with US Ambassador to Iraq Ryan Crocker and US General David Petraeus.
"He told you to 'cut off the head of the snake'," Saudi Arabia's ambassador to Washington, Adel al-Jubeir, told the US embassy in Riyadh two days after the high-level talks, according to the State Department memo.
"The King, Foreign Minister, Prince Muqrin, and Prince Nayif all agreed that the Kingdom needs to cooperate with the US on resisting and rolling back Iranian influence and subversion in Iraq," the memo said.
"The King was particularly adamant on this point, and it was echoed by the senior princes as well. Al-Jubeir recalled the King's frequent exhortations to the US to attack Iran and so put an end to its nuclear weapons program."
But the memo goes on to say other Saudi officials were more cautious about the need for military action, with Foreign Minister Prince Saud al-Faisal and intelligence chief Prince Muqrin bin Abd al-Aziz pushing for sanctions.
"The Foreign Minister, on the other hand, called instead for much more severe US and international sanctions on Iran, including a travel ban and further restrictions on bank lending," the memo said.
"Prince Muqrin echoed these views, emphasizing that some sanctions could be implemented without UN approval. The Foreign Minister also stated that the use of military pressure against Iran should not be ruled out."
The leaked memo could prove embarrassing to Saudi Arabia, which, while known to be nervous of Iran's alleged nuclear weapons ambitions, has not publicly called for Western military action against its powerful neighbour.
Reacting to the leaks, a Saudi government advisor who asked not to be identified told AFP: "The whole thing is very negative. It's not good for confidence-building."
Riyadh had been warned by Washington that documents would be leaked, but they had not known in advance exactly what would come out, he added.
Official Saudi government spokesmen were not immediately available.

My take: So much for Arab solidarity amongst Arabs. Saudi Arabia and israel have the same goal i.e. to bomb Iran and they show to the world that they are enemies ..
 
Kuna mwenye link ya kudownload full documents? The guardian uk na new york times wametoa sketch ya information ilivyo, docs nilizonazo zinaonyesha kulikuwa na correspondence 755 kati ya US na Tanzania. Natamani kujua zina information gani

http://public.tableausoftware.com/views/tags/country

nimejaribu kuingiza Tanzania ukifuta neno country sijaona lolote but looks like information has been removed temporarily
 
Kwani Iran ikiwa na nuclera Saudi watapata hasara gani wote si Waislam na adui yao ni mmoja?
 
Kwani Iran ikiwa na nuclera Saudi watapata hasara gani wote si Waislam na adui yao ni mmoja?
Usiwashangae Waarabu. Ni wanafiki mno na wana wivu mno.

Saudi Arabia iko tayari kumtosa Iran Abutuliwe na Marekani kuliko kumwona akipata silaha za Nyuklia na kuwa na nguvu kuliko wao. Ni wivu zaidi ndio unaomsumbua ndio maana Middle East haiwezi kuwa Independent.
It is the same Spirit which operate in Iran . They blow the crap out of each others faces while leaving their real enemy walking in piece. Unless the Arabs change their attitude and stop their hypocrisy they will continue to be kicked forever.
 
Kwani Iran ikiwa na nuclera Saudi watapata hasara gani wote si Waislam na adui yao ni mmoja?
Swali juu ya swali: Hivi adui wa waislamu ni Marekani? Je maslahi ya waislamu wote duniani yanafanana? Ukielewa hivyo hapa duniani umeliwa.
 
Swali juu ya swali: Hivi adui wa waislamu ni Marekani? Je maslahi ya waislamu wote duniani yanafanana? Ukielewa hivyo hapa duniani umeliwa.

Uko sahihi kabisa

Unajua kuna watu wanaaangalia hii issue kisiasa au kidini na kuna wenye akili wanaweka taifa mbele
Mfano : Egypt na Turkey nchi kiarabu zina uhusiano na Israel. Jiulize kwa nini ?
Tanzania Nchi yenye dhahabu kibao biashara inayomilikwa na waisrael haina uhusiano wamoja kwa moja na israel ? Kwa nini

Political Vs National Interest nini cha kuweka mwanzo?

Ndio maana ni somo kwa Tanzania kuwa na Foreign policy yenye maslahi ya taifa badala maslahi ya kupata sifa za kisiasa.
 
Libya+papers+iamge.jpg

Veteran Libyan leader Muammar Gaddafi fears flying over water, prefers staying on the ground floor and almost never travels without his trusted Ukrainian nurse, a "voluptuous blond," according to a US document released by WikiLeaks.

Gaddafi's eccentric and unpredictable personality is described in the State Department cable, which was posted on the New York Times website, a small sampling of the more than 250,00 documents unveiled by WikiLeaks on Sunday despite Washington's protests.

The cable from September 2009 describes how Gaddafi's preferences for shorter flights and accommodation on the ground floor created logistical headaches for his staff, and that the Libyan leader never travelled without a certain Ukrainian nurse at his side.

Gaddafi had a team of nurses and "relies heavily on his long-time Ukrainian nurse, Galyna Kolotnytska, who has been described as a 'voluptuous blond,'" said a secret cable from the Tripoli embassy dated September 29, 2009, written by the US ambassador, Gene Cretz.

Romantic relationship

One source, whose name was blacked out by the Times, tells the US embassy that Gaddafi cannot travel without Kolotnytska, "as she alone 'knows his routine,'" it said.

"Some embassy contacts have claimed that Gaddafi and the 38 year-old Kolotnytska have a romantic relationship," it said.

"While he did not comment on such rumours, a Ukrainian political officer recently confirmed that the Ukrainian nurses 'travel everywhere with the Leader.'"

The cable was written after US officials had discussed arrangements for the Libyan leader's visit to New York last year to address the UN General Assembly.

My take: Huyu jamaa huwa anawadada flan wanamlinda hivi hawageuki kweli?
 
It's true maana hata mimi nimecheki kuna hii http://www.wikileaks.fi/wiki/Talk:Tanzania_Richmond_Report but not accessible

Mkuu hiyo ya Richmond ni ya zamani, lakini inaonekana kuna intel nyingi sana ambazo zinatuhusu watz. Inawezekana tumeuzwa tayari wenyewe hatujijui. Jamiiintelligence ingewasilana na Assange tungeweza kuzipata inaonekana sasa hivi website ya wikileak inasakamwa sana.

Wakuu halafu nina swali, nani kwa sasa ni mkurugenzi wa TISS, RO? ZOKA? au nani?
 
huyu Ahmedinejad apigwe tu na kuondoshwa madarakani, ana kiburi na hana maana yoyote, yuko kama dikteta, marehemu Sadamu Hussein!
 
Kwani Iran ikiwa na nuclera Saudi watapata hasara gani wote si Waislam na adui yao ni mmoja?

Waislamu si wamoja kama unavyofikiri! Saud Arabia ina Wasuni wengi wakati Iran ina Washia wengi! Madhehebu hayo makuu hayapendani sana Middle East! Pia waarabu ni watu wa ajabu sana, wakimaliza mgogoro na Israel wataanza kudundana wao kwa wao!
 
Hii ni funika kombe mwanaharamua apite, Marekani kwa kuzua conspiracy stories ndiyo wenyewe:
  • How war benefits USA Economy?
  • Nani waliomuua John Fitzgerald Kennedy?
  • Bay of Pigs invasion?
  • 'Civil War in Congo, Sierra leone'
  • Weapons of Mass destruction?
  • USA Fighting marxist/communist idealogy in 1970s Latin America?
  • Wikileaks
Mimi nadhani hapa hakuna kipya, kwani kila mmoja anaelewa kazi za maafisa ubalozi ni pamoja na ujasusi ndiyo maana kuna maafisa ubalozi wanaojificha chini ya majina haya 'military attaches', 'Education attaches', 'Economic Development attaches' n.k lakini kazi yao kubwa ni masikio na macho ya Usalama wa Taifa wa nchi zao.

Hapa dunia inafunukwa macho iweweseke na utamu wa story za Wikileaks huku Marekani inanufaika kwa kuchonganisha nchi kama Bahrain dhini ya Iran au kuchonganisha Saudia dhini ya Irani. Si tumesikia hii November 2010 wataalamu wa nuklia huko Iran wameshambuliwa na majasusi wa nje wakati wakielekea maofisini kwao na Iran inasema ni kazi ya Israeli na maswahiba wake wa nchi za Magharibi pamoja na Marekani.

Marekani inajua kuwa sasa kuna vyombo vikubwa vya habari ambavyo si vya kimagharibi vilivyo na heshima zaidi ya Voice of America (VOA) au BBC au CNN mfano vyombo ya RussiaToday, Aljazeera n.k Hivyo hii Wikileaks ni chombo cha propaganda kusambaza habari za nchi za magharibi kujijengea hoja kuzishambulia nchi za kimapinduzi kama Venezuela, Iran, Cuba n.k

Hii Wikileaks habari zake mbona hazipewi uzito mkubwa na vyombo vya habari ndani ya Marekani yenyewe? hii ni kwa sababu Wa-Marekani wanajua na wameshastukia mikakati inayosukwa na serikali yao yenyewe kuhalalisha kuanzisha vita katika maeneo mengine ya dunia mfano kifo cha Rais J.F Kennedy kilisukiwa hoja kuwa Fidel Castro wa Cuba anahusika!

Uchumi wa Marekani na nchi za Magharibi unaendeshwa kwa kusababisha vita kwa kuwa viwanda vya silaha ndivyo vinavyokuza uchumi wa nchi hizo pamoja na kuhodhi biashara ya mafuta. Hata Tanzania tumeathirika kwa kuuziwa radar na BAE na kisha serikali ya Uingereza kufukia kashfa chini ya zulia kwa kuwa Uingereza imenufaika kiuchumi na kiajira kwa kuuza radar hiyo ya kijeshi kwa Tanzania.

Hii Wikileaks ni conspiracy story nyingine ya kuitawala dunia kimawazo kwa kisingizio kuwa Wikileaks ipo huko nchi ya Skandinavia hivyo nchi za kibeberu hazihusiki na hivyo tuzame na kaamini habari hizi kijuu-juu.
 
Mkuu angalia wikileaks zenyewe halafu uzi asses kutokana na vitendi vya nchi mbalimbali. Kama ingekuwa ni porojo za magharibi zisingefikia kiasi cha kuivua nguo serikali ya Marekani na maswahiba wake. Mpaka sasa leaks hazioneshi mwelekeo wa kupambana na nchi unazoziita za kimapunduzi, inaonekana kuwa zinaonesha uchafu wa serikali ya Marekani na washirika wake. Ni kama inaonesha ushirika wa wachawi.

Usisikilize mamneo ya wanasiasa jaribu kufuailia information zilizokuwa zinaflow kwenye public domain halafu linganisha na leaks zenyewe, ndio utajua kuwa wikileaks hawafanyi mzaha.

Ni sawa tu na JF ilipokuwa inamwaga mchele wakati wa EPA etc.
 
Mkuu,
Hawa jamaa angalia hiyo conspiracy story ya mauaji ya JF Kennedy, ilisukwa kuwa ni 'mwendawazimu'' mmoja Lee Oswald Harvey tu ndiye aliyefanya njama na kuzitekeleza pekee. Na hii habari ya Wikileaks inasema Praiveti mmoja wa jeshi la Marekani akiwa jijini Baghdad ndiye aliyevujisha habari kwa Wikileaks. Maswali kibao hapa inakuwaje stori hizi zinafanana kuwa mtu mmoja anataka kuitikisa dunia kwa hatua zake iwe kwa kutumia bunduki kuuwa kiongozi wa taifa kubwa au iwe kutumia laptop kutikisa ulimwengu kwa kutoa habari 'nyeti' ?!*

Lakini ukisoma kwa undani ripoti zote kuhusu mauaji ya Rais J. F Kennedy wa Marekani, utaona ilikuwa ni ' mapinduzi ya kumwangusha Raisi Kennedy' kwa kuwa marehemu Rais Kennedy alikuwa anajitahidi sana kuiepusha Marekani kuingizwa mkenge na 'wenye viwanda vikubwa vya zana za kijeshi ndani ya Marekani kujitajirisha kwa kuingiza Marekani ktk vita ambazo zingine hazikuwa halali' huku Marekani ikishika bango la kueneza haki na demokrasia duniani.

Hivyo ni aibu gani kubwa zaidi kwa Marekani kama ilivyotokea Raisi Kennedy 'kuangushwa' (kupitia mauaji) na wafanyabiashara wa Kimarekani waliokuwa wamewashikisha mshiko majenerali wa jeshi, CIA , FBI n.k ndani ya Marekani? Hii habari ya wikileaks kuhusu kutaka kujua kila jambo ktk nchi ngeni ni la kawaida ktk balozi zote ulimwenguni na ndio maana kuna 'diplomatic bags' ambazo zinapitishwa ktk mipaka na viwanja vya ndege bila kukaguliwa, na humo ndani ya fuko lazima kutakuwako habari za dizaini ya wikileaks, sema tu wanataka kujifanya Marekani ni watu wa kufuata viwango vya heshima kutotafuta 'umbeya' toka kwa wenyeji wao wa kibalozi!

Mfano mwingine ni wa Israeli walikuwa wanakomba mkojo wa Yasser Arafat aliyekuwa kiongozi wa P.L.O kujua ana kaugonjwa gani na hivyo kumwacha afe kifo cha kawaida bila lawama baada ya Israeli kugundua ugonjwa wake Yasser Arafat haweziishi miaka mingi zaidi. Maofisa wa kibalozi kazi zao pamoja na diplomasia pia ni ujasusi wa kila aina iwe elimu-sayansi, teknolojia, kupindua nchi n.k n.k hivyo hii habari ya Wikileaks ni 'kiwingu tu' cha kupotezea lengo hasa la Wikileaks. Hizi pasipoti mbali ya kuzuia wimbi la wahamiaji pia ni nyezo nzuri za ki-usalama kufuatilia nyendo za watu wanaowatilia mashaka.

Hivyo habari hizi ni mikakati ya nchi beberu baada ya kuona kuwa vyombo vyao kama New York times newspaper, CNN, VOA, wiizara ya nje Marekani, White House au BBC na k.n haviaminiwi kama credible source ya habari duniani kwa ajili ya wao kujichukulia sheria mkononi au kuwasaidia marafiki wao kama Saudia. Hivyo wanajua internet news toka nchi moja ya Skandinavia itaaminiwa na watu duniani, na hivyo itafika wakati watatumia 'source' za Wikileaks kutimiza azma yao ya kujifanyia chochote hapa duniani. Hii habari kuwa Tanzania na vi-nchi vingine pia zipo ktk wikileaks ni kufunika kombe mwendawazimu apite.
 
Usiwashangae Waarabu. Ni wanafiki mno na wana wivu mno.
Kaka,

Hayo ndio maneno pia aliyoyasema Canal Ghaddafi, hawa jamaa wapo na self interest zao kuliko dini yao. Ni sisi waafrika ndio wenye matatizo ya kudandia mabasi kwa mbele. Sasa tazama na huko Yemen kumbe serikali inatambua ya kuwa marekani wapo inside na wanapigana na al-qaeda kinyemela. Lakini media na viongozi wanaongea kama vile America ni common enemy of Isalm to please their audiences (si ndio unafafiki wenyewe huo) hata huko Saudi Arabia na wao ni hivyo hivyo tu longolongo tu za kuuridhisha Umma wao. Bahrain na Jordan nao wote walitaka Iran ipate kibano.

News za leo asubuhi nimeona huko kwenye Egyptian elections chama kinacho jiita 'Muslim Brothers' walikutana na watemi wanapoenda kupiga kura na kuchezea kichapo. Kibaya zaidi kuna posters zimebandikwa kusema kwamba wagombea wao wamejitoa kugombea habari za kutunga tu. Na jamaa naona tayari wameshapewa somo na Raisi Kikwete maana mpiga kura mmoja anadai yeye kaenda kupiga kura mapema ajabu boksi tayari limeshajaa.

Embu tujifunze sisi ni waafrika kabla ya unafiki wa mzungu na mwarabu. Binafsi siamini kama ni Leak ya hivyo bali America inajaribu kujiosha sio wao tu na Waarabu pia wanasupport their actions and this is the way to let the World know.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom