wikiendi ukweni!...

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844

...umeenda ukweni kuchumbia rasmi,

baada ya utambulisho na wenyeji kuwapa muda 'mjisikie mpo nyumbani' , Baba mkwe anakutupia swali la papo kwa papo; ..." eti kijana, iwapo tumepata ajali majini, na uwezo wako kumuoka mtu mmoja tu, utamuokoa nani kati yangu, mama mkwe, mkeo au mwanao?"

Ingelikuwa weye ungejibu nini?
 
mke...kwani nimekuja kuoa ukoo hapa??!!lkama mtoto tutapata wengine kibwena as long as the factory is still working!!hao wakwe wakajipumzikie tu kwanza wameshakula chumvi mingi!!
 
...umeenda ukweni kuchumbia rasmi,

baada ya utambulisho na wenyeji kuwapa muda 'mjisikie mpo nyumbani' , Baba mkwe anakutupia swali la papo kwa papo; ..." eti kijana, iwapo tumepata ajali majini, na uwezo wako kumuoka mtu mmoja tu, utamuokoa nani kati yangu, mama mkwe, mkeo au mwanao?"

Ingelikuwa weye ungejibu nini?

Sasa kama naweza kumuokoa mtu mmoja, si nitajiokoa mwenyewe. Au?
 
Of coz mke, kama yeye atahitaji mambo ya kuokoana amwokoe mkewe si kila mtu na wake bana? khs mtoto tutatafuta mwingine. so simpo!
 
...umeenda ukweni kuchumbia rasmi,

baada ya utambulisho na wenyeji kuwapa muda 'mjisikie mpo nyumbani' , Baba mkwe anakutupia swali la papo kwa papo; ..." eti kijana, iwapo tumepata ajali majini, na uwezo wako kumuoka mtu mmoja tu, utamuokoa nani kati yangu, mama mkwe, mkeo au mwanao?"

Ingelikuwa weye ungejibu nini?

Mie ningemjibu hivi : -
Nitamuokoa Mke wangu.
 
Majibu yenu yanamaanisha wengi wenu ni realists kuliko idealists,

nawahakikishia, iwapo mke ndiyo angepewa nafasi ya uokoaji angemuokoa mwanawe kwanza! ...
 
hehehe yah its possible ka mke angepewa nafasi angetoa jibu hilo....so wat does it mean wajimini???we love wake zetu more than hw they love us cz upendo wao umehamia kwa watoto??
 
hehehe yah its possible ka mke angepewa nafasi angetoa jibu hilo....so wat does it mean wajimini???we love wake zetu more than hw they love us cz upendo wao umehamia kwa watoto??

...ndio maana mimi hapo sijaona bado busara ya kumuokoa mke, any way, tuvute subira watu wazidi 'kujikaanga'.
 
mtoto kwanza ati,hakuna hata kufikiria.mke anaweza kujitahidi akjiokoa mwenyewe.najua hata yeye atapiga kelele,"baba nanihii muokoe mtoto".
 
mtoto kwanza ati,hakuna hata kufikiria.mke anaweza kujitahidi akjiokoa mwenyewe.najua hata yeye atapiga kelele,"baba nanihii muokoe mtoto".

akishakuwa na nguvu ya kusema baba nanihii muokoe flani basi huyo sio wa kuokolewa tena...mtoto si waweza pata mwingineee lakiniii sasa waweza pata mume mwingine wa hata kuweza mlea mwanao the way mlivyokuwa mwamlea mkiwa wawili?!

lets be wema jamanii mlikula kiapo cha kuwa bega kwa bega kwa mema na mabaya so hapo ndo mahala pa ku prove hw u can b for each other
 
Ebwana hiyo ajali wakati inatokea we utakuwa wapi?anyway ukweli nikwamba mke ndo atakuwa wa kwanza then kama nafasi ina kuwepo basi mtoto atafuata ikishindikana ntajitahidi kutafuta mwingine.yote mipango ya mungu.
 
Mi ntaokoa mke kwanza.....mtoto ni majaliwa tu na mungu akipenda tutapata mwingine. Bsbs mkwe na mkewe watabaki wanaokoana wenyewe
 
...yaani hapa kuna wengine wanaona maji yamejaa nusu gilasi, na kuna wanaoona maji yamepungua nusu gilasi,... raha kweli kweli!

enhe, nawasikiliza tu mnavyojikaanga!

tuendelee kuchangiana mawazo...
 
mtoto kwanza ati,hakuna hata kufikiria.mke anaweza kujitahidi akjiokoa mwenyewe.najua hata yeye atapiga kelele,"baba nanihii muokoe mtoto".

...umetoa 'mwangaza'... je, unausimamia ukweli huu?
 
nitamuokoa mwanangu hapo..ooppps kumbe wameulizwa madume

Jamani hamjambo humu nimeingia bila kupiga hodi
Heshima yenu ndugu
 
nitamuokoa mwanangu hapo..ooppps kumbe wameulizwa madume

Jamani hamjambo humu nimeingia bila kupiga hodi
Heshima yenu ndugu

...NANOO karibu bibie, hujambo weye?

jibu lako marhaba kabisa, ndio maana nikawaambia 'wenzangu' upande wa pili wa shilingi umuhimu ni tofauti...

Karibu kwenye mdahalo!
 
...umeenda ukweni kuchumbia rasmi,

baada ya utambulisho na wenyeji kuwapa muda 'mjisikie mpo nyumbani' , Baba mkwe anakutupia swali la papo kwa papo; ..." eti kijana, iwapo tumepata ajali majini, na uwezo wako kumuoka mtu mmoja tu, utamuokoa nani kati yangu, mama mkwe, mkeo au mwanao?"

Ingelikuwa weye ungejibu nini?

...Mimi ningejibu (ki-diplomatikali!); Mzee sitaweza jibu hilo, bado SIJAOA!
 
kwi kwi kwi asilimia 90% ya wanaume / kaka zetu humu JF wameonjeshwa au kulishwa limbwata wallahi .. kila mtu mke mke .. mtoto je . . nyie mmeshakula maisha mpeni mtoto nafasi naye ... mimi huniambii chochote bwana namuokoa mwanangu ...
 
Mimi nitamjibu hivi'; kwa leo mkwe wangu siwezi kukujibu, ila jibu litakuja siku hiyo hiyo ambayo tutakuwa tumepata hiyo ajali ya majini. Hapo ndio nitajua nitamuokoa nani....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom