Wiki ya vicheko kwa wahitimu: Laiti wangelijua kuanzia wiki ijayo mtaani itakuwaje

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Kwenye social media zote majoho yametamalaki kila Mkoa, vijana wana-graduate na kupewa vyeti mfano wa karatasi ngumu iliyorembwa kiasi. Ni wiki ya kufurahi, kucheka na ndugu, jamaa na marafiki. Baada tu ya sherehe kila mtu anarudi kwake. Inshallah!

Wenzangu na mimi, kuanzia wiki ijayo vichwa vitaanza kuwaka moto, lugha gongana, mambo yanakuwa hayaendi kama tulivyotegemea.

kila mlango umefungwa, kila mahali pamejaa mpaka pomoni. Hapo ndipo kichwa kitafanya kazi vizuri.

Nawatakia mahafali mema.
 
Tayari kielimu amefanikiwa so ni haki kufurahia maana nayo ni mafanikio makubwa unajua ni wangapi walipotea njiani? Mafanikio ya maisha ni hatua nyingine na kwasasa wengi wanatambua hali ilivyo so usijidanganye sana kuwa wahitimu wa vyuo hawajui hali watakayoikuta mtaani
Hujawa realistic. Mimi ningekuwa najua maisha ya mtaani yapoje. Ningeshaacha chuo tangu mwaka wa kwanza. Lakini kwa kuwa sikuwa najua basi niliendelea hadi mwaka wa mwisho.
 
Mleta uzi hana wivu wowote,bali amewatahadharisha tu wahitimu juu ya kinachofuata baada ya furaha ya kukabidhiwa vyeti.Mleta uzi yupo Tanzania na wahitimu wapo humu humu Tanzania,ambako tangazo la ajira linahitaji watu 4000,na waombaji ni 90000,kwahiyo 86000 wapo mitaani na karibuni wataungwa mkono na wahitimu wapya.Kutiwa moyo kuwa kuna amani wakati kuna vita ni uongo na unafiki mkubwa.
 
Mkuu waache wafurahie safari ya miaka 17 na wengine 19 sio mchezo sio dhambi kusoma Bali kwa alipofikia inabidi ajipongeze.

Usidhani hao wanachuo hawajui maisha ya mtaani yalivyo nadhani wanajua sana zaidi ya wewe unavyoyajua.

Sio kwamba ndio wanaingia mtaani Bali walikuepo mtaani since walipomaliza masomo Yao around mwezi wa Saba mpaka mwezi wa nane graduation ni sherehe tu ya kuhitimisha,

Mwisho usikariri kwamba maisha yatakua magumu kwa graduate wengine tayari ni wafanya biashara n.k

Opondo ja shirati
 
Nilikua zangu UDOM leo katika harakati zangu za ujasiriamali nikawa nawazoom tu madogo wanarusha kofia wamejiremba hatari mabinti so sexy nikaflash back 4 yrs ago na mimi nilikua kama wai na sikutegema kuwa hapa nilipo leo bt the way they looked its like u cant tell them nothing they own the world today acha wainjoy kabla hawajakutama na msoto....

Leo viwanja vikali vyote dom ni bata la ajabu from udom students..

Nakavizia kamoja kakike nikakachape af nikafundishe maisha baada ya kichapo
 
Mleta uzi hana wivu wowote,bali amewatahadharisha tu wahitimu juu ya kinachofuata baada ya furaha ya kukabidhiwa vyeti.Mleta uzi yupo Tanzania na wahitimu wapo humu humu Tanzania,ambako tangazo la ajira linahitaji watu 4000,na waombaji ni 90000,kwahiyo 86000 wapo mitaani na karibuni wataungwa mkono na wahitimu wapya.Kutiwa moyo kuwa kuna amani wakati kuna vita ni uongo na unafiki mkubwa.
Unatofautisha vipi unafki na utanzania ?
 
Kwenye social media zote majoho yametamalaki kila Mkoa, vijana wana-graduate na kupewa vyeti mfano wa karatasi ngumu iliyorembwa kiasi. Ni wiki ya kufurahi, kucheka na ndugu, jamaa na marafiki. Baada tu ya sherehe kila mtu anarudi kwake. Inshallah!

Wenzangu na mimi, kuanzia wiki ijayo vichwa vitaanza kuwaka moto, lugha gongana, mambo yanakuwa hayaendi kama tulivyotegemea.

kila mlango umefungwa, kila mahali pamejaa mpaka pomoni. Hapo ndipo kichwa kitafanya kazi vizuri.

Nawatakia mahafali mema.
Hatua moja,huanzisha nyingine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom