Wiki ya Taifa ya Vijana: Mnyika sauti pekee nyikani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wiki ya Taifa ya Vijana: Mnyika sauti pekee nyikani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Oct 12, 2012.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tupo kwenye wiki ya vijana na zimebaki siku chache kilele kifike tarehe 14 Oktoba.

  Mnyika ni sauti pekee nyikani kuhusu wiki hiyo, nimemsoma: JOHN MNYIKA: KUELEKEA WIKI YA VIJANA: WAZIRI AELEZE HATUA ILIYOFIKIWA KATIKA KUANZISHA BARAZA LA VIJANA, BENKI YA VIJANA NA KUPANUA WIGO WA AJIRA KWA VIJANA nikamsoma tena: JOHN MNYIKA: KIJANA AU MDAU WA MASUALA YA VIJANA WIKI YA VIJANA IMEANZA LEO; UMEPANGA KUFANYA KAZI GANI MOJA KWA MUSTAKABALI WA VIJANA NA TAIFA?

  Nataka sasa kuwasikia wale ambao mara kwa mara wamepiga kelele kuwa ni vijana na wanataka vijana wenzao wawaunge mkono kwenye uchaguzi, nataka pia nisikie kutoka kwenu kuhusu mustakabali wa vijana na taifa.

  Kwa waandishi wenzangu, tuipe wiki hii uzito ili ilete tija kwa vijana, kama wiki hii haina maana basi ifutwe badala ya kuwa na wiki isiyochangia katika maendeleo.

  PM
   
Loading...