Wiki ya pilika pilika mitaa ya Msimbazi na Jangwani

Mawawa

Senior Member
May 2, 2020
130
250
Miamba ya soka Tanzania Simba na Yanga jumapili hii zitamenyana katika kombe la FA hatua ya nusu fainali.

Ikumbukwe msimu huu yanga kapata matokeo mazuri dhidi ya mtani wake simba.

Jana katika pita pita zangu nilipita kwenye moja ya vijiwe vikubwa vya mashabiki wa timu hizi.

Kulikuwa na tambo nyingi ila mashabiki wa simba walienda mbali zaidi, pale walipo dai kuwa wao walisha acha zile tamaduni za kwenda kwa wataalamu yaani waganga.

Ila watani zao yanga tamaduni hizo bado wanazo. Ndipo mashabiki hao wa simba walipo apa kuwa, awamu hii matawi yao yote na vingozi wao wote, lazima waungane na kuwa kitu kimoja awamu hii lazima wazirudie zile tamaduni zao.

Kwa muono wangu mchezo huu utakuwa mkali na wa kusisimua. Licha ya simba kuwa na kikosi bora huku yanga wakiingia kama underdog kwenye mchezo huu.

Linapokuja suala la kujitoa basi wachezaji wa yanga huwa wanajitoa kweli kweli licha ya ubutu wa kikosi walichonacho.

Ila natoa tahadhari kwa vikosi vyote.

A. Yanga mnapaswa kusahau matokeo ya nyuma mliyoyapata dhidi ya simba.

Mnapaswa kukaa tena chini na kuja na mkakati mpya ni vipi tunaweza kupata matokeo mazuri tena dhidi ya simba.

Mkija na mentality ya kujiamini kuwa hawa tunawaweza huwa hawatusumbui hili linaweza likawagharimu. Ikumbukwe hii ni hatua ya mtoano ukifungwa huna chako.

B. Simba mpaka leo wanaamini kufungwa na watani zao ilikuwa ni bahati mbaya.

Ni kweli simba wanakikosi kizuri kuliko yanga, ila linapokuja suala la derby weka ubora wako pembeni.

Simba mnapaswa kuwaheshimu yanga kama mnavyo waheshimu Azam mnapokutana nao.

Mkakati wenu uwe tunakwenda kucheza na timu bora, tunapata vipi matokeo? Kaeni na wachezaji wenu muwaeleze wale ni bora kama sisi tunapaswa kujiandaa kweli kweli.

MWISHO

Marefarii tafadhali chezesheni vizuri msilete mapenzi yenu mkatuharibia mchezo.

Simba_Sports_Club_on_Instagram:_“Mtani_tunakuja_🦁_#VPLchampions_#ASFC_#NguvuMoja”%22_.jpg
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,322
2,000
Kiubora Simba wako juu kuliko yanga ila yanga wana kocha mzuri kuliko simba na kocha wao anajua kuhusu ubora wa simba ndio maana amesema ameomba msaada kwa makocha wenzake ubeligiji na afrika kusini wamsaidie mbinu lakini kocha wa simba anacheza kwa kukariri.
Mechi ya jana hakuwa na haja ya kupanga kikosi cha kwanza kuepusha majeruhi na kubadirisha mbinu za timu lakini amerudia upuuzi uleule aliofanya na azam
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom