Wiki ya Maji: Charambe, Mbagala wakazi wanapewa maji yasiyofaa kwa matumizi

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,654
22,250
Inasikitisha sana kuona wanasherehekea wiki ya maji huku DAWASA ikiuza maji yasiyofaa kwa matumizi ya binaadamu, maji hayo yana kiwango kikubwa sana cha chumvi na harufu ikiashiria kuwa yanatoka kwenye kisima kifupi.

Pamoja na chumvi limo pia tope lenye rangi ya njano na kuna wakati maji hutoka yenye rangi hiyo ya njano. Maji haya yamekuwa yakitoka kwa muda wa miaka miwili sasa bila hatua kuchukuliwa licha ya DAWASA kuwa na taarifa ya hali ya maji yao.

Maji haya ukifulia nguo zikikauka hubaki na chumvi nyeupe, na nguo zikipata jasho au kuloa na mvua zikikauka chumvi nyeupe hujitokeza, pia ukiyachemsha hubadilika rangi na kuonesha weupe wa chumvi.

Tangu tatizo hili lianze wakazi wengi wamehamia kwenye kutegemea maji ya visima vya watu binafsi ambavyo ni afadhali japo hayatiwi dawa kuyasafisha.
 
Back
Top Bottom