Wiki ya kufa, kupona Igunga: HESABU ZAVIBAKISHA CUF, CHADEMA NA CCM KATIKA KINYANG’ANYORO

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Monday, 26 September 2011

07cufmgombea.jpg

Mgombea Ubunge Jimbo la Igunga kwa tiketi ya Cuf, Leopold Mahona (kulia) akicheza mchezo wa bao kwenye kijiwe kilichopo mtaa wa kijiji cha Mbutu, Wilaya Igunga, jana, ikiwa ni sehemu ya kampeni yake ya kuomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo. Picha na Fidelis Felix

HESABU ZAVIBAKISHA CUF, CHADEMA NA CCM KATIKA KINYANG'ANYORO

Daniel Mjema, Igunga

KAMPENI za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga, leo zinaingia katika wiki ya lala salama huku tathmini ikionyesha kuwa mchuano mkali ni baina ya vyama vitatu, licha ya vyama nane kusimamisha wagombea wake.

Vyama vyenye ushawishi mkubwa kisiasa jimboni humo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2, ni CCM kilichomsimamisha Dk Dalaly Kafumu, CUF kilichomsimamisha Leopard Mahona na Chadema ambacho kimemsimaisha, Joseph Kashindye.

Uchaguzi huo pia unavishirikisha vyama vya SAU, UPDP, DP, AFP na Chausta, lakini baadhi yake kampeni zake zinaendeshwa kwa kusuasua, huku vingine vikishindwa kabisa kufanya kampeni hizo.

Katika muda wa wiki mbili za kampeni Igunga, kumekuwa na matukio baadhi ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kutuhumiana kwa matukio ya uhalifu, ukiwamokampeni chafu, ubakaji, kumwagiwa tindikali, udhalilishaji na hata vitisho vya kutumia silaha za moto kama bastola.

Mvutano mkali zaidi upo baina ya CCM na Chadema, ambavyo makada wake wamekuwa wakipiga kambi za muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kulala katika maeneo yenye idadi kubwa ya wapigakura.

Juzi Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wenye ushawishi alitua kukiongezea nguvu chama chake, lakini tayari CCM kilikwishaongeza wapiga kampeni wake wakiwamo, Katibu Mkuu mstaafu wa chama hicho Philip Mangula. Kwa upande wake CUF kinajivunia mtaji wa kura 11,000 ilizopata katika uchaguzi wa mwaka jana.

Mbinu nyingine ambayo imekuwa ikitumiwa katika kampeni hizo ni wagombea kujinadi kwa lugha ya kisukuma kutokana na wapigakura wengi wa jimbo hilo kuzungumza lugha hiyo ikilinganishwa na Kiswahili.

Hali hiyo imekuwa ikiwapa wakati mgumu wanahabari kufuatilia mikutano hiyo kutokana na wengi kutofahamu lugha hiyo, isipokuwa pale anapokuwapo mkalimani wa kutafsiri maneno husika Kiswahili.

Katika wiki ya mwisho iyaoanza leo, viongozi wa kitaifa wa vyama vyenye ushindani, wanatarajiwa kuhamia Igunga, ili kunadi sera za wagombea wao ili kujihakikikisha ushindi.

Inachojivunia CCM
CCM ambacho kinadai kuwa na mtaji wa kura 39,000 ilizozipata katika uchaguzi mkuu uliomalizika Oktoba mwaka jana, kimekuwa kikijivunia mfumo wa uongozi kuanzia ngazi ya mabalozi, shina, kata hadi wilaya.

Chama hicho kinaamini kuwa kama viongozi wao hao hawatakisaliti basi kina uhakika wa kutetea kiti hicho kilichoachwa wazi na Rostam Aziz aliyejiuzulu huku kikiamini kushinda kwa zaidi ya asilimia 60.

Mbali na uongozi huo, lakini chama hicho kina madiwani 24 kati ya 26 na kinaamini kuwa madiwani hao pia wana ushawishi mkubwa kwa vile walichaguliwa na wananchi kwa kura.

Katibu Mkuu wa CCM, Willison Mukama wiki iliyopita alisema chama chake pia kinajivunia sera nzuri kwenye huduma za jamii ikiwamo mradi mkubwa wa maji wa Shinyanga-Nzega-Igunga ambao utafanya tatizo sugu la maji Igunga kuwa historia.

CCM kimejenga imani kwamba tuhuma dhidi ya Chadema kwamba wanafanya vurugu, zinaweza kukisadia kuendelea kuliongoza jimbo hilo ambalo halijapata kuwa na mwakilishi wa upinzani.

Baadhi ya makada wa CCM wanaweka wazi kwamba Chadema ambacho ni chama kikii cha upinzani nchini, kimejikuta kikisigana na CUF ambao pia ni wapinzani na kwamba CCM wanaweza kunufaishwa na hali hiyo.

Kwa mtizamo huo, CCM kinaamini CUF kitasaidia kupunguza kura za Chadema ambacho hakina mizizi jimboni humo ikilinganisha na CUF ambacho kilishiriki uchaguzi mkuu 2010 na kunyakua kura 11,000.

Hivyo ipo imani kwamba Chadema na CUF vinaweza kujikuta vikigawana kura za wale wanaounga mkono upinzani, hivyo CCM kushinda kwa urahisi.

Vijana kuwabeba Chadema

Kwa upande wake Chadema ambacho ni chama kipya katika siasa za Igunga, kinaamini kitashinda uchaguzi huo kwa kile kinachodai ni kufanikiwa kujipenyeza katika kundi la vijana ambao ni wengi.

Hakuna ubishi kwamba katika mikutano ya chama hicho, kundi kubwa linaloonekana kukiunga mkono ni vijana ambao wanaamini matatizo makubwa ya ajira na maisha magumu yamesababishwa na CCM.

Jambo jingine, Chadema kinaamini mgawanyiko ndani ya CCM uliosababishwa na kujiuzulu kwa Rostam, pia utapunguza kura za chama tawala na kuwanufaisha wapinzani.

Wafuasi wa Rostam wanadaiwa ‘kununa' na kufanya kampeni za chinichini ili kuhakikisha CCM hakishindi uchaguzi huo.

Jambo lingine ambalo Chadema kinaamini litapunguza kura za CCM ni hatua ya kumsimamisha Dk Kafumu katika wakati ambao kuna kelele nyingi kuhusu ufisadi katika sekta ya madini ambayo yanadaiwa kutowanufaisha Watanzania.

Kabla ya kuteuliwa kwake kupeperusha bendera ya CCM, Dk Kafumu alikuwa kamishina wa madini na Chadema na CUF vinatumia hilo kama silaha ya kummaliza mgombea huyo kwamba alishiriki ufisadi.

CUF na mtaji wa kura 11,000
CUF kwa upande wao wanaamini kuwa kura 11,000 kilizozipata 2010, mgawanyiko ndani ya CCM unaotokana na kundi la Rostam na vurugu zinazotokea jimboni humo zitasaidia kukivusha na kushinda.

Mbali na hayo lakini CUF kinaamini kuwa ndicho pekee kimeendesha kampeni za kistaarabu kulinganisha na vyama vingine na kutokana na hulka ya wenyeji kutoshabikia vurugu basi watakipa kura.

Pia CUF kinaamini kwamba mchuano mkali kati ya Chadema na CCM kutavifanya vyama hivyo viwili kugawana kura hivyo wao kupata ushindi kutokana na ushawishi walioufanya kwenye kampeni.

CUF kinaamini mgombea wake ndiye mwenye nguvu na anayekubalika zaidi na kwamba hata 2010 angeweza kuibuka mshindi lakini kutokana na ‘nguvu' kubwa aliyoitumia Rostam ndio iliyochangia kumwangusha.

Kinachotarajiwa

Kutokana na hali ilivyo na ushindani mkubwa baina ya vyama vya Chadema, CUF na CCM, wadadisi wa siasa wanasema lolote linaweza kutokea katika jimbo hilo.

Wiki ya mwisho ya kampeni hizi inaweza kutoa mwelekeo wa nani atakuwa mshindi lakini kwa mtizamo wa kidadisi, hadi sasa hakuna chama chochote chenye uhakika wa ushindi.

Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kufanyika Oktoba 2 huku wapiga kura waliojiandikisha wakiwa 170,000 lakini wanaweza wasijitokeze wote kama ilivyotokea mwaka jana ambapo ni asilimia 40 waliojitokeza.

atakayekuwa na mikakati mizuri ya kumalizia hii ngwe ya lala salama ndiye atakeyeshinda.
 
Uchaguzi bwana huleta matokeo hata yasiyo tarajiwa,Wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010,CCM ilikuwa ikijivunia asilimia karibu 75 za REDET,mgombea Urais CUF alijiita mlima na kumfananisha wa CHADEMA na Kichuguu,baada ya matokeo wote tulishangazwa na miujiza ya uchaguzi huo, Kwa igunga, rekodi za nyuma zinaweza zisiwe kigezo kabisa kubaini nani ataibuka mshindi,
Binafsi naona kuna kila dalili za kushuhudia miujiza mingine ya uchaguzi Igunga, muhimu ngoma ichezwe salama.
Mungu Ibariki Tanzania
 
CCM walishajua kitambo hawatashinda jimbo la Igunga!
Kuleta wazee waliostaafu kuipigia kampeni si mchezo!
 
I totally dislike CCM but am sure,they will emerge winners in this election,simply because of a number of reasons,but the big one is rigging!!! and ignorance or rather illiterate of igunga people
 
CCM walishajua kitambo hawatashinda jimbo la Igunga!
Kuleta wazee waliostaafu kuipigia kampeni si mchezo!

CCM wameshindwa kabisa. Mpaka wanawaangukia kina Mangula---wazee ambao walionekana hawafai eti ndio wamekuwa wapiganaji Igunga!!!!!!!!! !! Kweli kichekesho....

Yule Mzee alishindwa uenyekiti wa ccm Iringa eti sasa anafaaaa. Wana Igunga fanyeni kweli hao ccm huwa hawamalizi, siku zote huwa hawana Vision. wameishiwa wanatabia za Dainosor......chama kikubwa na kikongwe lakini hakina madhara chanya kwa wananchi kwa sasa.
 
I totally dislike CCM but am sure,they will emerge winners in this election,simply because of a number of reasons,but the big one is rigging!!! and ignorance or rather illiterate of igunga people

Tupo wote, nakubaliana na wewe kabisa. Ignorance ya watu wa Igunga tu ndio itawafanya CCM washinde. Thse people are ignorant, hawajitambui shida yao ni nini. kama mtu anaweza kulia eti Rostam kajiuzulu, basi analeta mashaka mengi zaidi
 
Hivi huyu kilaza Lusinde wa mtera ameshaandaa sumu? Kama bado mimi nimtafutie cyanide.
 
Wiki hii ndio muamzi wa hatima ya nchi. CHADEMA ikifanikiwa kuchukua kiti hiki cha igunga itakuwa imemaliza kazi ila ikishindwa itakuwa imepiga hatua kadhaa nyuma. Natamani niwe salama nishuhudie matokeo
 
CCM walishajua kitambo hawatashinda jimbo la Igunga!
Kuleta wazee waliostaafu kuipigia kampeni si mchezo!
Walikosea sana kumleta mzee asie jua kushawishi watu kama Mangula. Wamuulize Mangula anamfahamu Sanga a.k.a. Jah People? anakumbuka alivyoaibika alipogombea uenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa? Ningekuwa yeye nisingejiingiza kutetea sera ambazo hazitekelezeki, ningebaki Imalinyi kuendelea kunywa ulanzi na wanakijiji wenzangu wa huko.Hata hivyo mzee pekee anayeweza kampeni za chaguzi ndogo ktk CCM ni Mzee Malecela a.k.a Tingatinga bin bulldoza.
 
Ukweli ni kwamba CCM itapata around 42% ya kura zote. 58% watagawana CDM na CUF ambapo CDM watapata around 38% na CUF 20%. Ni bahati mbaya kwamba Igunga bado wanaiona CUF kama chama cha upinzani ili hali ni CCM B. Elimu ya uraia inahitajika sana. Turufu ya mwisho ya CDM ni walimu. Kama Walimu wa Igunga ambao wana ufahamu wataacha kuendekeza njaa, waka mu-support mwalimu mwenzao na wakahamasisha wanafunzi kwenda kupiga kura kwa CDM, matokeo yanaweza kubadilika CDM wakapata 48%, CCM 42% na CUF 10%. Huu ni utafiti wangu usio rasmi.
 
Uchaguzi bwana huleta matokeo hata yasiyo tarajiwa,Wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010,CCM ilikuwa ikijivunia asilimia karibu 75 za REDET,mgombea Urais CUF alijiita mlima na kumfananisha wa CHADEMA na Kichuguu,baada ya matokeo wote tulishangazwa na miujiza ya uchaguzi huo, Kwa igunga, rekodi za nyuma zinaweza zisiwe kigezo kabisa kubaini nani ataibuka mshindi,
Binafsi naona kuna kila dalili za kushuhudia miujiza mingine ya uchaguzi Igunga, muhimu ngoma ichezwe salama.
Mungu Ibariki Tanzania

Well kwa tafsiri yangu nakuunga mkono. CUF walipata kura nyingi kwa sababu hapakuwa na upinzani, CDM mgombea alijiengua.
Ukiangalia kwa makini utaona kuwa kuna dalili watu wa Igunga wanataka mabadiliko. Kama waliweza kumpa mgombea wa CUF kura 11,000 basi sasa wamepata nafasi nzuri ya wagombea wengi. Pia ikizingatiwa kuwa mwaka 2010 walipiga kura 40% tu, basi wale waliosusa kupiga kwa kuwa walijua CCM wangeshinda tu sasa watakuwa na nafasi ya kupiga kura kwa mkombozi wa matatizo yao, na ni dhahiri aliyejipanga vizuri ndie atakayeshinda. Nafasi ya CCM kushinda itakuwa ndogo sana kama wananchi wengi zaidi wakijitokeza, sidhani kama uibaji wa kura utakuwa rahisi this time mana uchaguzi ni jimbo moja na wapinzani hasa CDM inaonekana wamekaa vizuri katika kila kata.
Naamini kutakuwa na miujiza na uchaguzi huu ndio utakuwa mwanzo wa mapinduzi ya kuikomboa Tanzania.
 
atakayekuwa na mikakati mizuri ya kumalizia hii ngwe ya lala salama ndiye atakeyeshinda.
Kuna Tetesi kwamba CCM watakuja kumaliza mchezo na kulamba kula zoote siku chache zijazo kwani wanataka kumleta Jakaya Mrisho Kikwete aje amalize mchezo, hii itakuwa ni karata dume maana Kikwete ana mvuto.
 
Well kwa tafsiri yangu nakuunga mkono. CUF walipata kura nyingi kwa sababu hapakuwa na upinzani, CDM mgombea alijiengua.
Ukiangalia kwa makini utaona kuwa kuna dalili watu wa Igunga wanataka mabadiliko. Kama waliweza kumpa mgombea wa CUF kura 11,000 basi sasa wamepata nafasi nzuri ya wagombea wengi. Pia ikizingatiwa kuwa mwaka 2010 walipiga kura 40% tu, basi wale waliosusa kupiga kwa kuwa walijua CCM wangeshinda tu sasa watakuwa na nafasi ya kupiga kura kwa mkombozi wa matatizo yao, na ni dhahiri aliyejipanga vizuri ndie atakayeshinda. Nafasi ya CCM kushinda itakuwa ndogo sana kama wananchi wengi zaidi wakijitokeza, sidhani kama uibaji wa kura utakuwa rahisi this time mana uchaguzi ni jimbo moja na wapinzani hasa CDM inaonekana wamekaa vizuri katika kila kata.
Naamini kutakuwa na miujiza na uchaguzi huu ndio utakuwa mwanzo wa mapinduzi ya kuikomboa Tanzania.

Yale yale ya dawa za kwa babu..hivi bila strategy hakuna miujiza mkuu aliyejipanga ndio atakayeshinda, aliye na uwezo wa kujenga hoja ndiye atakayeshinda other things constant kuibiwa, etc..
 
Yale yale ya dawa za kwa babu..hivi bila strategy hakuna miujiza mkuu aliyejipanga ndio atakayeshinda, aliye na uwezo wa kujenga hoja ndiye atakayeshinda other things constant kuibiwa, etc..

Well muujiza sio kwa maana kwa kidini, bali ni jambo litakalotoea kinyume na matarajio ya wengi.
Chama kitakachojipanga ndio kitashinda, na kwa jinsi ilivyo ni kati ya CCM & CDM.
CDM wanajitahidi kuziba mianya ya wizi wa kura, CCM wanataka kutumia uzoeafu wao ndio mana wamealika wazee kufanya campain.
Muujiza utakuwa pale ambao CCM itaangushwa, kwa mantiki kuwa watanzania wengi bado wanaamini CCM ndio inaweza kufanya kila jambo kushinda, so isipotokea this time ndio utakuwa mwanzo wa mabadiliko nchini hasa ikizingatiwa uchaguzi huu ni maandalizi ya 2015(kimkakati)
 
Analysis yako imesahau kwenye equation hiyo kuna CUF...

Chadema na CUF watagawa kura za wapenda mabadiliko...

CCM itabakiza kura za wanachama wake..na kuchukua partly kutoka kwa undecided

CCM itashinda lakini kwa margin ndogo maana kila chama kimetumia nguvu nying kubakiza wapiga kura wake..
 
Kuendelea kukipa kura ccm nikuyatowesha kabisa matumaini ya angalu kama kuna kitu kimebaki basi tuifaidi sote hasa rasilimali za nchi yetu.
 
Kuna Tetesi kwamba CCM watakuja kumaliza mchezo na kulamba kula zoote siku chache zijazo kwani wanataka kumleta Jakaya Mrisho Kikwete aje amalize mchezo, hii itakuwa ni karata dume maana Kikwete ana mvuto.

Wanataka kulileta gamba original
 
Back
Top Bottom