Wiki moja (1) kwa kampeni za wenyeviti Serikali za Mtaa inatosha

Am a star

Senior Member
Sep 22, 2015
167
158
Natumaini mko vizuri wote!

Niende kwenye maada moja kwa moja,.

NAJUA week moja ya kampeni kwa wale wanaotaka kugombea kwa mara ya kwanza uenyekiti, inawapa changamoto sana jinsi ya kujitangaza na kueleweka kwa watu!

Usiogope pamoja na kampeni za kuwakusanya watu, unaweza kutumia njia za kitechnologia ambazo ni rahisi kuweza kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja na kwa muda mfupi.

Tafuta mtaalam wa PRODUCTION
au wa ANIMATION akutengenezee promo video fupi ya utambulisho yenye
JINA LAKO KAMILI:
MAHALI UNAKOISHI
CHAMA UNACHOTOKA
KWA NINI UNAGOMBEA HIYO NAFASI
MAONO/ AHADI ZAKO
OMBA KURA
video isizidi dakika 5.. mda wa kampeni utakapofika sambaza kwenye magroup ya watu wako ili waendelee kukusikiliza hata ukiwa umelala.
hakikisha unapicha nzuri hata kumi kwaajili ya kushare na watu wako.

kuna watu humchagua mtu kwa uvaaji wake tu au kwa kua walimuona mahali hata kama hawajaskia alichosema.

hata kama ni gharama tumia vizuri technologia uone matokeo yake.
si mjuzi sana wa sheria ila natumai utaratibu huo hauvunji sheria

kwa msaada zaidi na ushauri wa uifanye namna gani ili iweyenye maana njoo DM au comment ntakujibu hapa hapa

Nawatakia mafanikio.
 
Wewe si bure, hizo simu za tachi na salio utawapa wewe! Msambazaji atasambaza kwa mkokoteni au kwa ndoo?
 
Kwani kuna uchaguzi hapo? Au ni uchafuzi, miaka minne chama kimoja tu ndio kina ruksa ya kufanya siasa, wanavyotaka, vyama vingine mje shindane na huyo kwa wiki moja? Na bado anategemea hujuma, awafanyie kwenye. Hiyo wiki moja kuna nini hapo? Ni kupoteza pesa za wanachi tu,
 
Hivi hata hizo nafasi za uenyeviti wa mitaa nazo zinawatoa watu roho eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Kwani kuna uchaguzi hapo? Au ni uchafuzi, miaka minne chama kimoja tu ndio kina ruksa ya kufanya siasa, wanavyotaka, vyama vingine mje shindane na huyo kwa wiki moja? Na bado anategemea hujuma, awafanyie kwenye. Hiyo wiki moja kuna nini hapo? Ni kupoteza pesa za wanachi tu,
KUCHUKUA HATUA NI BORA KULIKO KULALAMIKA
 
Wanasiasa wanajua kua kuna gia ya kuingilia so uenyekiti ni MLANGO. Hvyo kutoana roho imo
Yaani mie naona kama hiyo nafasi ni ya usumbufu. namuona mwenyekiti wa mtaa ambavyo kila mara anapelekewa shida za kila aina, mara agongewe usiku kisa bibi na bwana wamegombana kwa kunyimana unyumba...
 
haha kesi na mtonyo sio bure kusolve hizo kesi, pia Title.
 
jisaidie ili usaidiwe.. anesubiri bando aendelee kusubiri NITAPITA....
Kheri yako kijijini kwenu ni matajiri! Hata kama wangekuwa matajiri huo mtandao wa simu ni wao wenyewe? Siamini kama umewahi kwenda kwenu tangu uzaliwe, acha zakuleta.
 
Kheri yako kijijini kwenu ni matajiri! Hata kama wangekuwa matajiri huo mtandao wa simu ni wao wenyewe? Siamini kama umewahi kwenda kwenu tangu uzaliwe, acha zakuleta.
bahati mbaya sijaelewa tatizo ni nini,
ni kama unapanick bila sababu.

(kunguru w3w)
 
Back
Top Bottom