Wiki mbili zitanitosha kujua gari?

Habari zenu ndugu zangu.
Ninataka kujifunza kuendesha gari, haya magari madogo ya familia.

Je, wiki mbili zitanitosha kujua kuendesha manual na automatic?
Zinakutosha sana,ukiwa na kichwa kizuri cha kuelewa hata wiki inatosha,iliyobakia utajiendeleza mwwnyewe kwa kuendesha.Muhimu ukishajifundisha usiache kuendesha.Ukikaa mda mrefu utaingia yoga,na hutaendesha tena.
 
Hazitoshi. Kwa usalama wako na watumia barabara wengine nashauri chukua muda kujifunza gari from alama, kuendesha, usalama barabarani na ufundi mdogo kama kubadili tairi regardless of manual/automatic transmission

Tunazungumzia chombo cha moto hapa incompetence yeyote inaweza pelekea madhara ambayo hata hujawahi yafikiria aidha kwako au kwa watumiaji wengine. Nimesikia habari nyingi nyingine zilizopelekea hata mauti sababu ya watu kujifunza gari kwa mwendokasi na kujiona wamekomaa.

Lingine ukishajua endesha ndani ya mji hadi ukomae kabla ya kuendesha safari ndefu, uendeshaji wa masafa marefu ni tofauti sana na ule wa ndani ya mji ukizingatia na ubovu wa barabara zetu. Kila la kheri
 
Automatic kwa week 2 zinatosha kabisa kujua gari,ila unaweza kusumbuliwa na alama za barabarani,sababu kujua gari ni jambo moja,kujua kutumia alama pamoja na gari ni jambo jingine...
Kwa manual Transimission utahitaji muda kidogo ukizingatia na jinsia yako ya kike...Ila ukitaka kuitwa dereva usiwe na haraka,nenda kajifunze kwa kutumia manual.
 
Gari sio kuweka gia tu litembee,,,Lina kanuni zake moja ya kanuni in kujua sheria linapokwenda kutembea barabaran,,ukishajua alama za barabaran nenda kajifunze kwenye barabara zenye hiyo michoro itakua poa zaid kulko kujifunza uwanjana
 
Back
Top Bottom