Wiki hii tuishi kwa imani

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
276
250
Leo ni siku ya kwanza ya wiki.

Kila siku mpya yatupasa kuifurahia na kuishangilia sana kwani hiyo ndiyo zawadi kuu Mwenyenzi Mungu aliyotupa sisi sote bila ya upendeleo.

Tukitaka kufanikiwa kwenye malengo na mipango yetu ya wiki hii yatupasa kutembea kwa imani katika kila tunalolipanga na kutenda.
Imani yako ndio ngao yetu bila ya imani hakuna tunaloweza kulifanya tukafanikiwa hata kama kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kufanikiwa, bila ya imani mioyo yetu itatazama zaidi upande wa kushindwa pale panapotokea changamoto ndogo sana.

Faida mojawapo ya kuwa na kutembea kwa imani ni kupata nguvu ya kupanga na kufanya mambo magumu na makubwa ambayo kwa fikra za kibinadamu hasa kwa kutumia logic na mahesabu hatuoni uwezekano mkubwa wa kufanikiwa.

Wiki hii yatupasa kuondoa woga na mashaka moyoni.

Kumbuka, moyo wenye mashaka na woga hauwezi kuruhusu imani ifanye kazi ndani yake.
Kwa kifupi ni kwamba :

Imani na woga haviendi pamoja. Woga huzuia imani na Imani huondoa woga.

Woga na mashaka hulete nia mbili moyoni 'sitaki nataka' hii hukufanya ushindwe kujitoa kwa moyo wako wote katika lile unalolifanya.

Tukumbuke Mwenyezi Mungu mwenyewe kwenye moja ya amri 10 alizotupa anasema tumpende kwa moyo, akili na nguvu zetu zote.

Kwa mfano Petro alimuomba Yesu amuamuru atembee juu ya maji, Yesu alimwambia njoo na Petro alishuka chomboni na kuanza kutembea lakini alipoona upepo ALIOGOPA na kuanza kuzama. Kisa hiki tunakipata(Mathayo14:26-30)

Tukisoma kwa makini upepo sio sababu kuu iliyomsababishia Petro kuzama bali Petro alipoona upepo alipatwa na woga kutokana na kuwa na imani haba na kukosa kwake imani ndiko kulikomplekea yeye kuzama.

Wiki hii tukitaka kushinda yatupasa tumbee kwa imani huku tukijiamini katika yale tunayoyafanya huku tukiweka imani kubwa kwa Mwenyezi Mungu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom