Wiki 1 ya kifo cha Kamanda Soleiman: Kiongozi wa Hezbollah aapa kuwarudisha wanajeshi wa Marekani nchini kwao wakiwa kwenye majeneza

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah amesema kutakuwa na operesheni mbalimbali dhidi ya vikosi vya Marekani katika kanda ya mashariki ya kati, ili kulipiza kisasi Marekani kuwaua makamanda wa Iran na Iraq mapema mwezi huu.

Bw. Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba ya televisheni kwa ajili ya kukumbuka wiki moja ya vifo vya mkuu wa Kikosi cha Quds cha Iran Qassem Soleimani, na kamanda wa wanamgambo wa Iraq Abu Mahdi al-Muhandis.

Amesema Marekani haina chaguo lingine ila kuwaondoa wanajeshi wake kwa hiari, au kurudisha miili yao katika majeneza nchini mwao.

Bw. Nasrallah pia amekanusha madai ya Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Bw. Soleimani kuwa na mipango ya kushambulia ubalozi wa Marekani.

Aidha, Bw Nasrallah ameisifu Iran kwa ujasiri wake wa kushambulia vikosi vya jeshi la Marekani nchini Iraq.
 
Bora Osama bin laden alikuwa mjuzi wa kuwatesa USA na washirika wake. Namkubali sana.

Huyu watamcholopoa mapemaaaa .....
 
Kama waliweza kumdungua Osama aliyedhaniwa kushindikana, al-Baghdad aliyetisha kuliko magaidi wote tena kwa kumsakasia mbwa, na hatimaye wakamdungua Jen. Qassem kama njiwa pori sioni kinachoshindikana kwa Nasrallah. Asubuhi na mapema atakabidhiwa 72 huyu.
 
Nakumbuka kipindi hicho bado wadogo tulikuwa tunaambiwa Osama ana sura saba na wakati mwingine wakienda kumkamata anageuka na kuwa sisimizi
 
Daaa kweli Leo nime amini uongo waga una vuma kuliko ukweli hata sisi kijijini kwetu tulikuwa tuna ambiwa Osama ana sura 7 enzi hizo mara una ambiwa kuna muda ana geuka kuwa sisimizi, mara ana geuka kuwa ki siki daaa shikamoo mwaka 2000 hahaaaaaa haaaaaaaa😂😂😂😂😂.
 
Kama waliweza kumdungua Osama aliyedhaniwa kushindikana, al-Baghdad aliyetisha kuliko magaidi wote tena kwa kumsakasia mbwa, na hatimaye wakamdungua Jen. Qassem kama njiwa pori sioni kinachoshindikana kwa Nasrallah. Asubuhi na mapema atakabidhiwa 72 huyu.
Hiyo 72 ulioitaja hapo sijaielewa ndo nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaa kweli Leo nime amini uongo waga una vuma kuliko ukweli hata sisi kijijini kwetu tulikuwa tuna ambiwa Osama ana sura 7 enzi hizo mara una ambiwa kuna muda ana geuka kuwa sisimizi, mara ana geuka kuwa ki siki daaa shikamoo mwaka 2000 hahaaaaaa haaaaaaaa😂😂😂😂😂.
Hahahaaha noma sana mawanangu hizo stori zili trend sana
 
Daaa kweli Leo nime amini uongo waga una vuma kuliko ukweli hata sisi kijijini kwetu tulikuwa tuna ambiwa Osama ana sura 7 enzi hizo mara una ambiwa kuna muda ana geuka kuwa sisimizi, mara ana geuka kuwa ki siki daaa shikamoo mwaka 2000 hahaaaaaa haaaaaaaa.
 
Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah amesema kutakuwa na operesheni mbalimbali dhidi ya vikosi vya Marekani katika kanda ya mashariki ya kati, ili kulipiza kisasi Marekani kuwaua makamanda wa Iran na Iraq mapema mwezi huu.

Bw. Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba ya televisheni kwa ajili ya kukumbuka wiki moja ya vifo vya mkuu wa Kikosi cha Quds cha Iran Qassem Soleimani, na kamanda wa wanamgambo wa Iraq Abu Mahdi al-Muhandis.

Amesema Marekani haina chaguo lingine ila kuwaondoa wanajeshi wake kwa hiari, au kurudisha miili yao katika majeneza nchini mwao.

Bw. Nasrallah pia amekanusha madai ya Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Bw. Soleimani kuwa na mipango ya kushambulia ubalozi wa Marekani.

Aidha, Bw Nasrallah ameisifu Iran kwa ujasiri wake wa kushambulia vikosi vya jeshi la Marekani nchini Iraq.
walisema watadeal na kila mtu atakayeongea maneno kama haya, kama ni kweli kasema namtakia r i p iliyo salama ndugu Nasrallah amen
 
Kufa Wajibu Na Unavyokua Mpambanaji Hua Unatarajia Kufa Zaidi Kuliko Kua Hai Jamaa Anajua Muda Wowote Atasafirishwa Kuelekea Kifo Sasa Hamna Ajabu Hapo Na Wangekua Na Uwezo Waharaka Wangekua Washamuondoa Maana Ule Mchaka Mchaka Alowapeleka WAYAHUDI 2006 Mpaka Leo Wanajiuliza Maana Ulikua Msako WAHAYAWANI

nashukuru kwa kunielewa, ndio maana nikamuombea r I p iliyo salama au nilikosea ndugu?
 
Back
Top Bottom