Wigi: Nywele inayopunguza gharama za kusuka

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari.

Wigi ama less wigi ni nywele inayotamba sana mjini pamoja na kuwa na aina nyingi za nywele lakini wigi imeteka wadada.

Kwanini wigi au less wig imetokea kupendwa sana ni kwakuwa imekuwa na muonekano kama wa nywele.

Pia aina ya nywele hiyo imekuwa ikivaliwa na kuvuliwa wakati wowote mtumiaji akitaka.

Nywele hiyo pia imekuwa ikifanya wadada wapendeze sana.

Mbali na kupendeza kwa nywele hizo pia zimewapa muonekano wa tofauti.

Hii ni kutokana na aina mbalimbali ya ya nywele hizo kama Bob na mengineyo.

Ajabu za nywele hizo yaani wigi huweza kudondoka na kumdhalilisha.

Maajabu hayo hutokea tu pale anapokuwa hakuzisuka vizuri nywele au kuosha.

Upande wa gharama ni nywele zinazouzwa ghali na wanaovaa wanajiweza kifedha.

Pia yapo mawig fake nayo yanatumika na watu wenye uwezo wa hali ya chini.

Nayo yamewapendeza wadada hii ni kutokana na hali ya uchumi wa mtu.

Nywele hizo pia zimewafanya wadada wapunguze gharama za kusuka.
 
Back
Top Bottom