Wifi anatoa siri za ndani kwa housegirl.

debon

Senior Member
Oct 6, 2011
134
62
Habari zenu wana jf. Mwenzenu wifi yangu ananishangaza na nashindwa kumsaidia. Ana msichana wa kazi ana miaka 20, huyo msichana sio kwamba katulia kivile anapenda umbea na akisikia jambo lolote anasema bila kufikiri. Wifi yangu yuko masomoni cha kushangaza karudi likizo na kumsimulia house girl kwamba ana wasiwasi mume wake(kaka yangu) anatembea na mwanamke ambaye ni jirani kwa sababu huyo mwanamke anampigia kaka yangu simu na kumtumia sms, mara anamsimulia hamwamini mumewe maana wanakaa bila kuonana mda mrefu. Mara ooh mume wangu ana mpango jambo fulani nimemkataza, mara ndugu wanaomba fedha tumekataa. Yani anamwambia siri zote za ndani. Na mimi nkifika hourse girl ananhmwagha kila kitu akisahau wale ni ndugu zangu. Na kama ananiambha mi bila woga majirani. Alafu anavyoongea naona anawadharau wifi na kaka zaidi. Naogopa kumwambia wifi awe makini na hg asijeniona namfatilia. Siwezi ongea na kaka nisijekuwa mchonganishi.Cha ajabu huyo hg anayemwamini nshamfurumua mara nyingh akimwandalia kaka chakula huku kavaa kanga na chupi tu. Mi sielewi
 
Wifi yako mjinga, tena ***** anampa Hg njia ya kumkamata mumewe, yeye kama hapati chakula cha usiku aongee na mumewe na si HG, ni kosa kubwa ambalo tunalifanya wanawake wengi.
 
Sasa wewe umeleta huu uzi ili iweje? Tumnange wifi yako au? Unataka ushauri wakati wewe pia ni third third party?

Ngoja nikwambie kitu...huyo wifi yako ni wa kumsaidia kimawazo na si kumtundika na kumcheka.

Wanawake wengi wako so insecure na inapofikia situation kama hiyo si wote wana busara za yupi wa ku share nao yaliyopo moyoni. Wewe una mume?

Ni kweli kuwa haipaswi kumuonyesha house girl kuwa huna imani na mumeo...ila fact kuwa yuko mbali ameona atapata clue kupitia kwa h/girl which is wrong. Lakini jua yuko confused na anataka comfort si kuchekwa.

Ukizingatia Tanzania private investigators hawapatikani...unakuta anaamua kutumia any means at her disposal kukusanya data za mumewe.

Muite umwambie kama unampenda wifi yako...mwambie huyu H/girl si wa kumpa siri zako...hata mimi najuua mnayoongea., hata majirani wanajua. Tafuta mwingine wa ku m-confide si h/girl...maana it seems like she needs someone to talk to.
 
Watu walio soma dini wanasema ukisha ona mtu anamshakia shakia mme wake/mke wake na hafichi siri zake za ndani, basi kwenye ubongo wake kuna kasoro flani.

Poleni sana kuwa na wifi kama huyo :biggrin:
 
Habari zenu wana jf. Mwenzenu wifi yangu ananishangaza na nashindwa kumsaidia. Ana msichana wa kazi ana miaka 20, huyo msichana sio kwamba katulia kivile anapenda umbea na akisikia jambo lolote anasema bila kufikiri. Wifi yangu yuko masomoni cha kushangaza karudi likizo na kumsimulia house girl kwamba ana wasiwasi mume wake(kaka yangu) anatembea na mwanamke ambaye ni jirani kwa sababu huyo mwanamke anampigia kaka yangu simu na kumtumia sms, mara anamsimulia hamwamini mumewe maana wanakaa bila kuonana mda mrefu. Mara ooh mume wangu ana mpango jambo fulani nimemkataza, mara ndugu wanaomba fedha tumekataa. Yani anamwambia siri zote za ndani. Na mimi nkifika hourse girl ananhmwagha kila kitu akisahau wale ni ndugu zangu. Na kama ananiambha mi bila woga majirani. Alafu anavyoongea naona anawadharau wifi na kaka zaidi. Naogopa kumwambia wifi awe makini na hg asijeniona namfatilia. Siwezi ongea na kaka nisijekuwa mchonganishi.Cha ajabu huyo hg anayemwamini nshamfurumua mara nyingh akimwandalia kaka chakula huku kavaa kanga na chupi tu. Mi sielewi

Kama kweli unania ya dhati ya kuinusuru ndoa ya kakaako, tafuta namna na njia sahihi ya kukaa na huyo wifi yako na kumueleza madhara ya kutoa siri za ndani za familia yake. Siyo lazima uongee naye wewe directly ila waweza kutafuta watu wa karibu wakiwemo ndugu au rafiki wamama watu wazima. Uwe makini maana mawifi mara nyingi huwa mnatafsiriana vibaya kana kwamba mnaoneana wivu.
 
Kwanza nina wasiwasi na nyie mnamteta wifi yenu kwa h/girl...ni mule mule tu.

Wote mna feed data zisizomuhusu kila mtu kwa muda wake.
 
Hii ni dalili kwamba mume anakula wote yaani mke, house girl, jirani na dada mtu. Ama kila mmoja anang'ang'aniwa kuliwa. Huu ni wivu wa wanawake kwa mwanaume lijari.

Ushauri wangu kama umeshaliwa nenda tu kapime ngoma ili uwahi dawa kama mambo yatakuwa yameharibika tayari.
 
Katika watu wote kwa sasa mwogope sana house maid. Mipaka yenu iishie kazi na huduma zake tu no more!! Ukimleta karbu kila kitu kitakuwa karibu. Jaribu uone!!!
 
Tena unaweza kuta naye ana discuss na huyo huyo h/girl na majirani pia. Maana anaonekana yuko aware na data walizo nazo majirani...amejuaje kama nae akai kwenye majungu na umbea?

Haya mambo ya uwifi haya. Mi nashukuru mume wangu kwao wote ni wanaume.

Mbona na wewe unatoa mambo yenu ya ndani na kumwaga JF? Wewe utakuwa hatari zaidi
 
una uhakika wifi yako anamwambia hayo hg?
Isijekuwa hg keshaonja vya kaka yako anatafuta kuleta chokochoko?
 
Sasa wewe umeleta huu uzi ili iweje? Tumnange wifi yako au? Unataka ushauri wakati wewe pia ni third third party?

Ngoja nikwambie kitu...huyo wifi yako ni wa kumsaidia kimawazo na si kumtundika na kumcheka.

Wanawake wengi wako so insecure na inapofikia situation kama hiyo si wote wana busara za yupi wa ku share nao yaliyopo moyoni. Wewe una mume?

Ni kweli kuwa haipaswi kumuonyesha house girl kuwa huna imani na mumeo...ila fact kuwa yuko mbali ameona atapata clue kupitia kwa h/girl which is wrong. Lakini jua yuko confused na anataka comfort si kuchekwa.

Ukizingatia Tanzania private investigators hawapatikani...unakuta anaamua kutumia any means at her disposal kukusanya data za mumewe.

Muite umwambie kama unampenda wifi yako...mwambie huyu H/girl si wa kumpa siri zako...hata mimi najuua mnayoongea., hata majirani wanajua. Tafuta mwingine wa ku m-confide si h/girl...maana it seems like she needs someone to talk to.

hapo kwenye green hapo....u can hire me if hujiamini....
 
Biashara matangazo ati. Wewe toa terms mbona wateja tupo.

Nilikuta comment moja Michuzi Blog. Jamaa analalamika eti kuna kampuni iko PPF Tower inauza software za kutrack mazungumzo ya simu.

Mimi mwenzenu nikaona mbona hii ni good news. yeye kaona ni kikwazo...kumbe ameitangaza kiaina. Anasema serikali iifute. Mwe! Nikija huko lazima niitafute aisee.

Back
Top Bottom