WIFE kaichukua mateka simu yangu

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,706
10,170
Leo nimesahau simu nyumbani.
Kwa kuwa kazi zangu haziniruhusu kutoka nimeshindwa kuifuata hivyo nimeona bora nimpigie kwa landline kumjulisha kuwa aniletee.
Alichonijibu kuwa eti, ni kwamba simu sio muhimu kwangu hivyo basi hawezi kuileta.
Yote hayo kayafanya sijui ni kwa sababu gani, hakika kanisababishia usumbufu usio na kifani
 
Asubiri suprises SMS kutoka kwa secretary wako a.k.a Nyumba ndogo.
 
Kama mkeo ni 'Wangu Mama keri'
Andika urithi tu, maana kabla asubuhihaijafika utakuwa ushatolewa utumbo kwa sms zitakazoingia
 
Hahaha. Tena ningekuwa mie ningekuambia sijaiona na mie ninetoka home na narudi late. Ili uriraksi nijionee senema, usiwashtue vichanchuda. Afu ukirudi jioni sigombani, nakucheka! Nakuachia homework ujiulize au na wife nae anafanya zaidi yangu?
 
umesema ni mkeo?si umwambie yeye, sisi tutajua anayafanya hayo kwa sababu gani kweli, hatuishi naye, hatumjui...
mpigie tena kwa hiyo landline muulizane, mumalizane huko
 
Hahaha. Tena ningekuwa mie ningekuambia sijaiona na mie ninetoka home na narudi late. Ili uriraksi nijionee senema, usiwashtue vichanchuda. Afu ukirudi jioni sigombani, nakucheka! Nakuachia homework ujiulize au na wife nae anafanya zaidi yangu?
Hahahaha! Jamaa leo atakoma , vinginevyo kama ni msafi atapona.... Nani asiyependa kujionea senema la bure?

Mke mwenza msalimie shemeji Paw na wifi letu AshaDii.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Paw
hahahaha she cant be serious kwann anajitakia magonjwa ya moyo?
ila mwambie kama anataka kukaa nayo baadae hautaki maswali sababu hautakua na majibu kama ameshakuambia simu haina umuhimu kwako hahahahahahah
 
Kwani unafanya biashara kupitia simu hiyo?Au wewe ni loan officer utashindwa ku-chase kwa simu?Kama jibu ni hapana,hiyo simu haina umuhimu.Utaikuta ukirudi!
 
Usihofu mkuu ukirudi utaikuta ila kama ni muhimu kwa kazi zako basi mkeo ni kilaza namba moja...
 
Afu wewee

Unatakiwa uende ukatese mateka kule gwantamo bay

Adhabu gani hiyo unamfanyia Paw?

Hahaha. Tena ningekuwa mie ningekuambia sijaiona na mie ninetoka home na narudi late. Ili uriraksi nijionee senema, usiwashtue vichanchuda. Afu ukirudi jioni sigombani, nakucheka! Nakuachia homework ujiulize au na wife nae anafanya zaidi yangu?
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Leo nimesahau simu nyumbani.
Kwa kuwa kazi zangu haziniruhusu kutoka nimeshindwa kuifuata hivyo nimeona bora nimpigie kwa landline kumjulisha kuwa aniletee.
Alichonijibu kuwa eti, ni kwamba simu sio muhimu kwangu hivyo basi hawezi kuileta.
Yote hayo kayafanya sijui ni kwa sababu gani, hakika kanisababishia usumbufu usio na kifani

Leo wafa kama hujakariri zile namba za ..... ili uwaombe chonde wasipige!! Itakula kwako!! Yaani leo wife wako atakuwa tu karibu na simu yako!! Sasa unaona kihoro sasa kama mambo si shwari? Mimi hata nikisafiri naenda na line ambayo ina roaming tu na nyingine zinapokelewa kama kawa!!! Tusipende kuishi maisha ya utumwa.
 
Hiyo simu hatumii password

otherwise mapema sana angeenda kwenye kampuni ya simu anayotumia akai block mapema aseme ameibiwa
 
Nimejikuta nacheka sana maana najua jioni itakuwa mahesabu.Jiandae tu kukabiliana na utakayoyakuta mkuu.
 
Leo nimesahau simu nyumbani.
Kwa kuwa kazi zangu haziniruhusu kutoka nimeshindwa kuifuata hivyo nimeona bora nimpigie kwa landline kumjulisha kuwa aniletee.
Alichonijibu kuwa eti, ni kwamba simu sio muhimu kwangu hivyo basi hawezi kuileta.
Yote hayo kayafanya sijui ni kwa sababu gani, hakika kanisababishia usumbufu usio na kifani

:cheer2:..Mzee kama unatabia chafu na kusaliti my wife wako.....hapo kazi unayo.... lakini kama mambo nishwari unawasiwasi gani na my wife wako? siku nyingine ukisahau kodi hata bodaboda urudi kuifuata kama unaona ndani yake kuna msala.......lakini kama hakuna longolongo poa tu... lakini ni lazima ujue kwamba hiyo simu yako my wife wako lazima ......aipekenyue.... aichunguze...... abeep namba zinazo bepika n a zisizo bipika..... :target:
 
Leo nimesahau simu nyumbani.
Kwa kuwa kazi zangu haziniruhusu kutoka nimeshindwa kuifuata hivyo nimeona bora nimpigie kwa landline kumjulisha kuwa aniletee.
Alichonijibu kuwa eti, ni kwamba simu sio muhimu kwangu hivyo basi hawezi kuileta.
Yote hayo kayafanya sijui ni kwa sababu gani, hakika kanisababishia usumbufu usio na kifani

Kwa majibu hayo tu, nahisi tayari kuna tatizo, au mligombana asubuhi?
Ni kwa nini simu yako isiwe na umuhimu? toka lini amegundua hivyo?
 
Back
Top Bottom