Wife bwana, ananikagua kinoma na asipoona kitu ananiuliza kama nime-block

thebogo055

Member
Jun 22, 2020
19
176
Nina mwezi mmoja sasa tangu nimtolee huyu binti ambaye soon atakuwa mke wangu halali wa ndoa.

Kama unavyojua mila zetu Africa ukishatoa kishika uchumba + mahali binti anakuwa huru kuja kwako akaspend quality time na wewe bila kuwa na ile hofu ya wazazi kuulizwa ulizwa maswali au kutafutwa tafutwa.

Saa kabla ya kuamua kutulia na kufanya jambo la kumpendeza Mungu nilikuwa nimeacha mazoezi yangu yooooooote especially ya wanawake na mawasiliano yasiyokuwa na maana ili nikiwa na mwenzangu niwe huru kabisa maana najua wanawake wanapenda kukagua kagua simu na kuingia kwenye gallery kuangalia mapicha picha ya zamani na kuanza kuji compare. Nikawa nimeacha kabisa mambo hayo.

Sasa cha ajabu huyu mwenzangu sasa hivi amekuja naishi nae huku tukipanga maandalizi ya ndoa. Ila ananikagua kinoma na asipoona kitu ananiuliza kama nimeblock watu especially wanawake maana sitafutwi tafutwi hovyo.

Anauliza au labda kuna app nime-install inaficha mambo yangu kwenye simu. Jana kaniomba simu yangu akawa anaingia app moja moja kutaka kujua kama nina mazoezi ya wanawake. Hahahahahaha huwa nacheka sana.

Maisha ya kutulia raha sana asikuambie mtu.
 
Hapo sipati picha ungekuwa na vimeo iyo simu ungeiona kama bomu la mkono lile la kutoa kipini ila vimeo vyote ushaviseti au kuvimaliza kabisa ndo mana raha mustarehe.
 
Kama unavyojua mila zetu africa ukishatoa kishika uchumba + mahali binti anakuwa huru kuja kwako akaspend quality time na wewe bila kuwa na ile hofu ya wazazi kuulizwa ulizwa maswali au kutafutwa tafutwa.

Sasa cha ajabu huyu mwenzangu sasa hivi amekuja naishi nae huku tukipanga maandalizi ya ndoa.

Samahani OP, hizi ni mila za Africa kweli? Kwamba binti anaruhusiwa hayo kabla ya ndoa?
 
Samahani OP, hizi ni mila za Africa kweli? Kwamba binti anaruhusiwa hayo kabla ya ndoa?
I guess ni mazoea tu ambayo tumejiwekea hasa kizazi hiki cha siku hizi sidhani kama wazee wetu walikuwa wakifanya hivi au tamaduni/dini zinaruhusu hivi, anyway ngoja OP aje akujibu vizuri. 😎
 
I know this feeling. Ile kujihisi upo huru hata simu yako huihofii. Lakini kwa kumzoesha anachofanya utakuja kujuta.

Kwanza anaonekana ni manipulative.

Pili ni gaslighter.

Tatu anaonekana hajiamini.

Nne my nigga usipomshape hii ndoa utaichoka soon as hizo tabia zake hua zinachosha faster.

Hua hawana jema watu wa hivyo.
 
...mazoea mabaya,usimzoeshe sana ashikeshike simu yako mzee...ipo siku uko mbeleeni utajuta kwa huo mchezo labda utafute kisimu chengine
 
I guess ni mazoea tu ambayo tumejiwekea hasa kizazi hiki cha siku hizi sidhani kama wazee wetu walikuwa wakifanya hivi au tamaduni/dini zinaruhusu hivi......anyway ngoja OP aje akujibu vizuri.
Yawezekana hi ni sababu mabinti wanakaa na pete za uchumba vidoleni miaka bila ndoa. Hadi inabidi wavue tu watafute wachumba wengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom