king james son
Member
- Apr 6, 2016
- 16
- 17
Wadau natumai hamjambo
Mm ni mwajiriwa, ni baba wa watoto wawili na mke mmoja, mke wangu amejiajiri mwenyewe ana saloon na ana biashara ya chakula ya medium scale na biashara zingine flan flan hivi
Kwa karibu miaka mitano sasa amekua akishiriki katika shughuli za vikundi vya akina mama katika masuala ya akiba na mikopo, mfano vicoba, saccos etc
Kwa takribani miaka 3 sasa amekua akiishi ndani ya madeni mazito ya vikundi hivyo pamoja na mabenki, anakopa huku anaenda kulipa deni la zamani, Hali imeenda hivyo hadi kufikia hatua madeni hayo yakawa yamemshinda kabisa na haachi, anafanya ujanja wa makaratasi anaenda kukopa kwingine
Nyumbani kwangu imefika pahala nimezoea kupokea makundi mbali mbali ya akina mama wenzie katika vyama vyao wanakuja home kuchukua vitu vya ndani Kutokana na kuwachenga kila siku ya kikao inapofika, wengine wakija kwangu wakamkosa huanza kuporomosha matusi na maneno makali wakidai watamshika tu na kwamba nimpe ujumbe, wakati mwingine wakinikuta nimeghafirika huingia ndani na kuchukua panga na kuwakimbiza kundi zima hadi huko barabarani, nimeshapelekwa polisi mara mbili kwa shambulio la kudhuru mwili
Mwezi February taasisi moja ya fedha ilikwenda saloon kwake na kusomba vifaa vyote mule ndani, halaf benki moja ikaenda kwenye mgahawa na kuchukua vitendea kazi karibu vyote na biashara zote mbili zimesimama
Baada ya Hali kuwa mbaya mwezi March ilibidi ahame nyumbani na kwenda kuishi kwa dada yake mkubwa maana nyumbani hapafai tena, ni vikundi vinapishana hapa na wameweka watu wa surveillance Muda wote,
Nina mwezi na kitu naishi na hg na watoto tu, unyumba tunafanyia guest house iliyokaribu na huko uhamishoni karibu na hapo kwa dada yake
Baada ya mm kulalamikia Hali hii na kuwa mkali kaja na pendekezo kwamba tuhame nyumba nzima tukapange, halaf nyumba yetu tuipangishe, anadai tukapange mbali kabisa na hapo nyumbani
Kwa maneno mengine anataka kuyakimbia hayo madeni moja kwa moja,nimekataa pendekezo hilo, sasa benki imeniita kwa wito maalum kupitia serikali za mtaa na kunieleza kuwa madhara ya wife kukimbia ni kuwa wao watalazimika kwenda mahakamani kuiomba mahakama ruhusa ya kuuza nyumba yetu Ingawa hakuitumia kama dhamana wakati wa kuomba mkopo, walipewa mkopo wa pamoja na wenzie,
Nikawa mkali sana pale nikawaambia hilo haiwezekani na halitafanikiwa nikaondoka
Hata hivyo nimetafakali sana na kujiuliza mwisho wa yote haya ni nini? Nitaishi hivi hadi lini? Nimejitahidi kulipa madeni yake kadhaa kupitia mshahara wangu lakini bado haijasaidia sana,
Sasa nimepata wazo la kumuacha nichukue mwanamke mwingine nianze nae upya, maana huyu wa sasa kwanza ana tatizo la kutonisikiliza sababu nilimzuia kuchukua mikopo hovyo hovyo lakini akaendelea
Sasa hebu nishaurini niachane nae tu au? Maana nikishamuacha nitawatangazia wanaomdai wote kuwa mm sipo nae tena na hivyo wamtafute wanakojua, hivi sasa nawajibu amesafiri Ingawa huwa hawaamini
Help pls