WHY TURN UP WAS 8.6mil people ie 42.84% of REGISTERED VOTERS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WHY TURN UP WAS 8.6mil people ie 42.84% of REGISTERED VOTERS

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Njowepo, Nov 5, 2010.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona kuna haja ya kulijadili ili jamani bse ni aibu.
  Kwa kuanzi point zangu
  I. NEC haikujipanga vilivyo kutoa elimu ya uraia the next question comes are they unfit for the job or mis used the fund given to them
  II. Rai walianticipate ushindi wa CCM by anymeans ivyo hawakuona haja ya kwenda kuungua na jua kama baadhi yao walivyoojiwa
  III. Baadhi ya watu kutoona majina yao kwenye vitabu uku wakiwa na vitambulisho
  IV. Ufungaji wa vyuo vya ualimu kule makete na arusha
  V. Kuchelewa kufunguliwa kwa vyuo vikuu
  VI. .......................
   
 2. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Uwezekano mwingine ni kuwa hiyo idadi ya wapiga kura walioandikishwa yawezekana isiwe ya ukweli kuwa walikuwa millioni 20.
  Uwezekano wa hili ni mkubwa ukizingatia na ari ya watu kwenda kupiga kura mwaka huu ilikuwa ni kubwa sana.

  Haiwezekani kwamba karibu nusu ya idadi ya watanzania wako eligible kupiga kura.

  Namba ya wapiga kura kwenye daftari la wapiga kura ni kubwa mno. Yawezekana wapiga kura halali ni wachache.
   
 3. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  pia idadi kubwa ya wakristo hushiriki ibada jpili. nalo limechangia. kama kumbukumbu ya kifo cha Karume na Nyerere tunapumzika ili kushiriki hafla ya kuwa kumbuka watu waliokwisha kufa, haingii akilini kushindwa kutenga siku za kazi kuwa ajili ya future ya Taifa. hizi ni njama za NEC kuvuruga uchaguzi kwa kuwa nyima watu muda mzuri kushiriki ibada.
   
 4. R

  Rugemeleza Verified User

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Si kweli miaka yote uchaguzi umefanyika jumapili hivyo watu "wachache" kwenda kupiga kura si sababu ya kusali Jumapili suala ni kuwa idadi ya wapiga kura ni ya kughushi. Idadi ya kwenye daftari ni ya uongo na hiyo ni sababu tosha ya kuwafuta kazi Makame na Kiravu kwani ni watu wazembe na waliolidanganya taifa.
   
 5. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Katika hali ya kawaida, katika maeneo mengi, idadi ya watoto ni zaidi ya mara mbili ya watu wazima.
  Kwa hali hiyo, ikiwa waliojiandikisha kupiga kura ni 20m basi idadi ya watu wote ni zaidi ya 60m.
  Kuna ulazima wa kuhakiki Daftari la wapiga kura ili kuondoa mapungufu yaliyopo!
   
 6. Novatus

  Novatus JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 331
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kwamba hao 8.3 million walipiga kura najuta kupiga kura yangu ikachakaghuliwa!!!!!!!!!!!!!!!!11
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Isije ikawa vitisho vya JWTZ vimechangia
   
 8. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mi nafikiri idadi hiyo kwenye Daftari la Wapiga Kula ni feki zaidi !!!!!!!!!! na imepikwa. Nzuri kufanyia research hii kitu.
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hofu na mashaka
   
 10. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Heri ya wewe mwenye uhakika uchwara.
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ni wazi kwamba Tanzania haina wapiga kura 20M.

  Watu walienda kujiandikisha kama ishara ya kupata vitambulisho ili waweze kupata mikopo ya SACCOS etc. in short zoezi lilitumika kama ya vitambulisho vya kitaifa... pia kulingana na elimu ndogo wakati wa kuhamisha kumbukumbu kama mtu amehama kata wengine walifanya fresh registration... akili kichwani... so in my honest opinion wapiga kura waTanzania hawazidi 15M.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 12. N

  Njaare JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Toka mwanzo kulikuwa na malalamiko kuwa idsadi ya wapiga kura haiwezi kuwa milioni 19 kama tume ilivyosema. Huenda ilikuwa 9 milion. Hao 10 milioni huenda ilikuwa ni kwa ajili ya kubalansi kama slaa angezizoa zote 9 milioni.

  Huenda pia Ilishindikana kuyaingiza masanduku kwa vituo sababu ya ulinzi mkali wa wananchi na huenda polisi kwa sababu nao ni watanzania wanaoumia kama raia wengine walionekana kuwa wangeweza kuharibu dill ndo maana labda mbinu ya ucheleweshaji ikatumika hivyo 80% ya kinana haikufika.

  Labda tuiombe tume iweke hadharani karatasi ambazo hazijatumika zihakikiwe na kuhesabiwa. Ni imani yangu kuwa kama zitahakikiwa zitakuwa zimepigwa halafu zikaachwa.
   
 13. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kwa uozo uliotokea, ningekuwa mwenye Mamlaka, ningeshawafutilia mbali watendaji wote wa NEC.
  Hata kura za marudio ktk majimbo yaliyokwamishwa kiuzembe hawana credibility kuyasimamia tena. Ila akina Kiravu na Makame lazima waachwe kama ahsante ya JK kwao kwa 'kuwezesha'.

  Ndiyo irresponsibility ambayo kwa mbele hatuioni kama kuna mwanga wowote, thus no new substance to be expected of the 'new dawn'
   
 14. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #14
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Kwa hali halisi, TUSIJIDANGANYE kwamba NEC itatoa elimu ya uraia au upigaji kura kwa wananchi. HILI HALIWEZEKANI HATA SIKU MOJA!

  NEC si tume huru, watendaji wakuu wameteuliwa na Rais. Kwa NEC kutoa elimu hiyo ni sawa na kuwapa wapigakura silaha ya kuing'oa madarakani CCM!

  Kilichobakia - na kama kweli kuna upinzani, zaidi ya CHADEMA - ni wadau hao kutoa elimu hiyo wao wenyewe, kuanzia sasa na kuendelea, bila kutegemea ufadhili kutoka nje. Vyanzo vya mapato viko vingi, hatuna shida ya pesa. Nakataa kwamba Wapinzani hawana fedha!
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna haja ya kutafiti juu ya ili.
  Ivi why tusichukue sample ya ambao hawakupiga kura then watupe majibu alafu next time iwe sheria kupiga kura ikiwezekana mtu awe fined.
  Bse mwisho wa siku kama hawatachagua atakaepita atawaongoza tuu
   
Loading...