Why to muslims, why islam ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Why to muslims, why islam ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpevu, Jan 28, 2011.

 1. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wadau na waungwana wote jamvini,
  Naanza kwa kuwasalimu, ASSALAAM ALAIKHUM...BWANA ASIFIWE...TUMSIFU BWANA.

  Nimekuwa nikifatilia saana mijadala mingi hapa jamvini hususan hili suala lililoingia ktk moja ya sehemu za maisha yetu- UDINI. Hli imekuwa ikikua siku hadi siku ambapo nimeshuhudia hata hapa jamvini wadau wakitoa majibu kwa uegemezi wa udini zaidi na maslahi ya umoja wetu tuliourithi toka kwa babu zetu kabla ya uhuru na hata baada ya uhuru.
  Mara kadhaa msigano mkuu umeegemea zaidi katika moja ya dini kuu haa nchini mwetu UISLAMU, ya kwamba wamekuwa hata wakiwahadaa jamii yenye imani ya Uislamu. Hivi karibuni pia baada ya matokeo ya kidato cha nne kumekuwepo na hali ya KEJELI na MAJIGAMBO dhidi ya uislamu/waislamu. Ieleweke huu mtandao unasomwa kwa upana na uwazi sana, sisi tuliopo humu jamvini mara tunapo sign-off baadhi ya mambo huwashirikisha wadau walio nje ya mtandao huu juu ya wimbi baya hili la udini, NI HATARI SANA KWA JAMII NZIMA.
  Tunashabikia saana juu ya udini, iwapo tunaukaribisha UDINI hapa nchini...ni zaidi ya nusu ya raia watateketea kwa vita ya udini (NAWAHAKIKISHIA). Tena itokeapo hali hiyo basi na laana ya Muumba nayo itawashukia wote wenye kuchochea udini.
  Enyi viumbe wa Mungu, ni fahari gani mliyonayo katika kujifakharisha kwa imani unayoiamini ilhali kwa muumba mtarejea?
  'Enyi wanaadam, je hilo mlifikirialo ndio dhamira ya Muumba wenu katika kuwapulizia pumzi na kuwaleta duniani? '
  'Enyi viumbe wenzangu, ni nani ajuaye kwa dhati imani yake ndio pepo na kwamba NA BASI AWANYANYASE WENGINE JUU YA IMANI ALIYONAYO ilhali dini zote zilishushwa nae Muumba? '
  Enyi wanaadam, epukeni kujifakharisha, epukeni kujiona ninyi ni wabora kuliko wengile...ilhali hamjui'
  'Enyi wanaadam mliojaa KIBRI, na tambueni ya kuwa vyote vilivyomo duniani na mbingu ni vyake Muumba, je! hamtambui? '.
  Enyi wanaadam, MUOGOPENI MUUMBA WENU, MUOGOPENI MUUMBA WENU, MUUGOPENI MUUMBA WENU.

  Ninawasihi na ninaisihi jamii hi ya kiTanzania, na ole wao waanzishao dhambi ya udini...hii itawarudia leo ama kesho, NA OLE WAO WAWALETEAO VIKONGWE NA WAGONJWA NA MASKINI NA DHALIMU mateso ya udini...laana zote zitawaangukia wote waanzishao uchokozi wa udini, laana ya Muumba itakuwa nao.
  Ninawaombeni saana wanajamii wake kwa waume, TUEPUKE FAKHARI YA MGAWANYO WA DHAMBI YA UBAGUZI WA DINI.
  IKIISHA UDINI NA KUBAKIA DINI PENDWA (mfano wa somalia) BASI ITAREJEA DHAMBI YA UKOO NA HITIMISHO ITAKUWA NI DHAMBI YA UKABILA.
  Nimenena, nimeusia,, TUMUOGOPE MUUMBA NA MALAIKA WEMA KWA ADHABU KALI ITAKAYOSHUSHWA KWA DHAMBI HII.
  Enyi wanaadam !!!
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama kupigana ili kupata haki na iwe hivyo
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  'Ewe kiumbe, umeumba na hali ya subra ili uipate rehma zake muumba. Kuwa ni kiumbe mwenye subra na mtangulize muumba wako na jitenge na dunia'.
   
 4. I

  Ipole JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mr. Mpevu mawazo uliyotoa nakuunga mkono tunapoingilia mambo ya kidini ni hatari sana maana huo moto Ukiwaka hakuna wa kuuzima
   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  John 1:45, "We have found him, of whom Moses in the law, and the prophets, did write, Jesus of Nazareth, the son of Joseph." Nope..not Muhammad! It was Jesus of Nazareth!
  ooops...
   
 6. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Oh mankind!
  Kindly trust on your faith to YOUR GOD but kindly don't betray/abuse/criticise on someones' faith, probably they might be right.
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Waislam tutambue kuwa kunamambo ambayo hakika siku ya kiama tutajibu mbele ya mwenyeenzi Mungu, hivi zaka wanazotoa waislam zinaenda wapi? Mbona hatuoni juhudi za jumuiya za kiislam katika kuwaendeleza binadamu walioumbwa na Mungu?, tazama waislam wanaanzisha shule ya sekondari- shule ina enroll watoto kwa miaka nenda rudi lakini watoto hawa ni kufeli tu na kujifunza uhuni na hakuna muislam anayestuka na kuona kuwa tunaangamiza vizazi vyetu. Wanajanvi wakisema uislam ni hopeless wewe unasema uislam unakejeliwa?!, na kutishia kumwaga damu!,nashauri hizi criticism tuzichukue positive ili vizazi vijavyo visiangamie kwa uzembe na ufisadi wa waislam.
   
 8. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  ...Hata mi nashangaa!... Ilaa mi nmegundua asilimia kubwa wanaoanzisha mada hizi ni waislam wenyewe!
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  mpevu+mpole, hoja nyingi dhidi ya uislam humu janvini katika kipindi hiki zinzlenga kushauri watu waone umuhimu wa kutoa huduma sahihi kwa jamii zao, hakuna haja ya kuwa na shule harafu wanafunzi hawafaulu, kubalini kusemwa pale ambapo kuna ukweli na mujibu hoja na si kulalama ati ni kejeri kwa uislam.
   
 10. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nakuomba rejea tena hii thread yangu, irejee kwa makini utambue dhamira iliyopo.
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hilo la rangi nyekundu ndio SHAKA.
   
 12. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  MaxShimba,
  Unajua msingi wa hoja yangu ni kutoa tahadhari KUU juu ya msigano wa kiimani kwa misingi ya utaifa, hili ndio langu na hata ukiirejea kwa dhati thread yangu utaelewa maudhui yake.
  Kwa nini sijagusia Hindu, Bahai, wapagani etc...hii ni kutokana na wimbi la imani mbili hapa nchini kusigana, Je! tunatambua hatma ya yote haya? why cant we prevent these confrontations/controversials ilhali wote tubaki na amani na uhuru pasipo mabalaa ya UDINI.
  These are my takes.
   
 13. October

  October JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Uisilamu una tatizo la kutokujifanyia tathmini na kujua kiini cha matatizo yao yanayowakabili. Badala Yake Mara zote uisimalu umekua ukinyooshea watu wengine vidole kwa matatizo ya waisilamu bila kufanya uchunguzi yakinifu wa chanzo halisi cha matatizo yao. Hali hii imewafanya waisilamu mara zote kuona kama vile wananyanyaswa na watu wengine wakati ukweli ni kwamba mengi ya matatizo yao yanasababishwa na wao wenyewe.

  Katika Elimu, ni miaka 50 sasa tangu tumepata uhuru na waisilamu wamekuwa wakilalamika kuwa wamenyimwa Elimu, Cha kushangaza ni kwamba hata baada ya miaka hii hamsini hakujawa na muamko kwa waisilamu kufanya juhudi za makusudi kuanzisha shule na kuzingatia masomo kwa dhati ili kutokana kujikwamua na hali mbaya ya Elimu walio nayo. Ukisema kuwa waisilamu ni maskini ndio maana hawana shule utakua muongo kwa sababu wapo waisilamu wengi tu wenye uwezo mzuri sana tu wa kifedha na wangeweza kusaidia kufungua mashule na kuajiri waalimu kwa ajili ya kuwaendeleza waisilamu.

  Kupanga ni kuchagua. Twajua kuwa nchi za kiarabu hutoa mabilioni kila mwaka kwa ajili ya kujengea misikiti nchi nzima, waisilamu wangekuwa na nia wangeziomba nchi hizi kusaidia katika sekta ya Elimu kwa fedha na wataalamu kuja kufundisha katika shule za waisilami ili kuwainua waisilamu.
  Misikiti hukusanya mabilioni ya zaka na sadaka, sijui kwanini hawazitumii hizi sadaka na zaka kwa ajili ya kuikwamua jamii yao ya kiislamu kielimu na kiafya.

  Nadhani matatizo ya waisilamu katika Tanzania ni ya kujitakia yenyewe tu. Hakuna atakaeweza kuwasaidia mpaka waamke wenyewe wakubali kubadilika, watambue kwamba wao ndio tatizo na wakubali kufuata kanuna na hatua za kubadilika.
   
 14. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Solution anza na wewe na jirani yako
   
 15. soine

  soine JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Tatizo la udini na hoja za udini zimekuwa gumzo mno wakati wa kampeni na mara baada ya kampeni. Yuko aliyekuwa akilalamika udini kila apandapo jukwaani kuomba kura, huyu muomba kura akishadadiwa na redio heri na gazeti 1 la kiislamu ndio chanzo cha sumu ya udini. Waulizeni hawa maana ndo wanafanya uislamu uönekane ndivyo sivyo.
   
 16. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kwanza Waislamu inabidi muanze nyinyi kubadilika na kutuona wakristu binadamu wenye akili timamu kama nyinyi na muache kutukejeli eti tunaamini "binadamu" Yesu ni MUNGU. Pia muache kutuita MAKAFIRI na sisi tutawaheshimu pamoja na dini yenu. Mbona wakristu tunawaheshimu baniani wanaona NG'OMBE. Msisema hata waislamu munawaheshimu vinginevyo msingekuwa mmapigana nao kila leo huko India.

  Mbona sisi Wakristu tunajuwa mapungufu mengi ya Muhammed (SAW), yameandikwa kwenye Quran na Hadith za Mtume lakini hamujawahi kutusikia hatu siku moja tukiyahubiri hayo makanisani mwetu.

  Inadidi kwanza muanze kutoa vibanzi katika macho yenu ndio mtaona boriti katika macho yetu, Lakini hizo provocation zenu dhidi ya wakristu hazitawafikisha popote.

  Na pia mkubali kwamba Elimu dunia ni ufunguo wa maisha na pia ili uweze kwenda mbinguni a SOUL needs to live in healthy body hence mjenge mahospitali.

  BTW wafanya biashara mabillionnaire wakubwa hapa Tanzania about 60% ni waislamu wakifuatiwa na wahidi about 30% na Wakristu ni ONLY 10% (Personal observation). Sasa hao wenzenu waislamu waliojaliwa kuwa na uwezo huo kwanini hawachangii mashule na mahospitali?

  Ninajua hapa ndio tatizo linapoanzia and hamutaki kua admit but the TRUTH IS YOU'VE INVERTED PRIOTY. Your prioty is to build mosques and madrassa NOT Schools for Elimu dunia and hospitals.

  If you've inverted prioties sasa sisi wakirustu kosa letu liko wapi?
   
 17. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  nakuunga mkono, lililopo sasa tuiombe serikali iratibu shughuli za jamii zinazofadhiliwa na taasisi za kiislam maana sasa zinzleta athari kubwa kwa jamii, waislam wanaanzisha shule lakini shule haifaurishi- hapa wanaoathirika ni watanzania na si waislam pekee. Serikali ichukue hatua maana hii taasis imekuwa mzigo kwa taifa na jamii kwa ujumla.
   
 18. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  I feel sorry to muslims and islams collectively
   
 19. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Schmidt, same feelings to Christians and Christianity.
   
 20. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  why so, tell/ask me smthn that u 'feel' where i cn clarify clearly.
   
Loading...