Why sitaki .xx.tz domains na badala yake nataka .com au .in | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Why sitaki .xx.tz domains na badala yake nataka .com au .in

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by SamJet, Sep 25, 2012.

 1. SamJet

  SamJet Senior Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  TISPA na TCRA walifanya jambo la maana kuanza huu mchakato wa tld'z za Tanzania tznic i.e co.tz, .or.tz, .go.tz na kadhalika.
  Ila na ukweli ni kwamba mpaka leo nina imani jamii ya wanateknohama Tanzania wanaoyumia huduma zao ni less than 15%.
  WHY??? MOJA: UBUNIFU

  Sio kwamba TZNic(hao wasajili wa .tz) wanafanya ovyo, hapana, wanafanya EXELLENT kwenye industry yao.
  Ila mfano mimi binafsi sitaki HATA BURE domain ya .co.tz. KWANINI? simple question, KWASABABU NI NDEFU.
  Hebu imagine ourname.co.tz au ourname.in Ipi fupi kati ya hizo???

  tznic tuseme wamekosa ubunifu. NINGESAJILI DOMAIN NYINGI KAMA KIUNGANISHI KINGEKUA .tz PEKEE, mfano samwel.tz.
  cheki india .in au libya .ly na kadhalika. no need for .co.iz au .co.ly au .co.us.......

  PILI: UPATIKANAJI!
  Huwezi amini, mpaka leo najua DOMAIN REGISTARS wa wili tu bongo,(miaka minne sasa, tangu nikiwa 16, najua wawili tu), Ila wanasema kuwa registars wako wengi.
  GOOD, NILIFANYA UTAFITI NA KUGUNDUA NDI WAKO WENGI, ILA SASA UNAFANYAJE ILI KUREJISTA?
  Kuna wengine wanataka uende ofisini kwao, wengine hata ofisi zao huzioni (siwataji kwa majina)
  PIA JINSI YA KUWALIPA NI NOMA, MI NIMEZOEA, NALIPA DOMAIN ZANGU ZA .COM,.US..ME...ETC ONLINE KWA DEBIT CARD YANGU, ILA WAO WANAKUAMBIA UKADEPOSIT BENKI,
  DU, mpaka nifike benki na niwatumie bank slip, si mtu mwingine atakua ameshasajili hilo jina langu????

  ILA KAMA KUNA MAHALI SIJAWAELEWA tznic, MNIREKEBISHE
   
 2. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,817
  Likes Received: 7,153
  Trophy Points: 280
  kumbe na wewe unaongeaga point am with u kwa hilo

  lakini naona kama umetaja tatizo tu je hakuna solution? niliskia kuna mdau anasema sjui .co.tz zinakua registered zambia au zimbabwe kitu kama hicho

  unaonaje ukaanzisha wewe kampuni yako ya malipo kwa tigo m z pesa
   
 3. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nini ujumbe wako? Unalalamika au unashauri?
   
 4. SamJet

  SamJet Senior Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  KAMPUNI!??!! Utakua umefanya vizuri ili kufanya vibaya.
  I mean, easyness of paying ni moja ila pia na swala la kumake iwe short like .tz only instead of .co.tz???
   
 5. SamJet

  SamJet Senior Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kazikubwa,,,use common sense, nalalamika, we umeona ushauri hapo...
   
 6. L

  Loloo JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tena sa hivi kuna waraka umetoka gvt employee email zao lazima wayumie hiyo kikoa ya bongo
   
 7. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Pole sana kwa hilo kama ulikuwa hautujui sisi Watz/Waafrika sababu ya kutumia hiyo .co.tz na sio tu .tz ni kwa sababu Uingereza wanatumia .co.uk basi hamna kitu kingine ni kama tulivyobadilisha kutoka TVT kwenda TBC kwa sababu Wazungu Waingereza wanatumia BBC hamna kingine na mwisho kama ulikuwa unatafuta mtu ambaye mnaweza mkajadiliana mambo ya msingi kama hayo humu JF basi umepotea kwani sana sana utaambulia kashfa na Matusi ukitaka wachangiaji humu njoo na Mada kuhusu wanawake na Ngono au Ridwani kanunua Mlima sehemu fulani hapo mtajadili mpaka utakimbia mwenyewe!
   
 8. N

  Nyakwec's Bro JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ndg Kijakazi hapo ndiyo unapokosea kama vitu wewe umehusika usiweke wa Tz wote kwa maelezo yako unaonesha ww na

  wenzako mmehusika katika hayo uliyoeleza sasa yanini kuweka wa tz wote badilika ongelea nafsi yako usiongelee

  watu,mkuu uliyepost ww siyo mtz mbona umeposti kitu tofauti na watu wanapost vitu hivi kila siku nani wa tz,tuache

  hayo?..

  Kwa swala kwamba jina ni refu mkuu mimi sioni kama hiyo hoja ni nzito ya kushindwa kutumia hayo majina

  na jinsi ilivyo hayo majina yanamaana sana lakini ukitaka kuyachukulia tu ni majina kweli utayaona marefu

  lakini kuna .co hii ni kwaajiri ya kampuni,kuna .ac hii ni kwaajiri ya academics institutions,kuna .go hii ni kwajiri

  ya governiment institutions,kuna .org hii ni kwaajiri ya organizations na nyingine nyingi kwa mimi binafsi

  kwakweli sijasikia kesi kama hii yako kwamba jina hilo linakuwa refu zaidi zinanisaidia kama ninajua jina la

  taasisi ninayotafuta inakuwa rahisi kuotea website yao kwa jinsi hii kwa kujua hizo maana zake mi ninaona

  zinamaana zaidi ya jina refu au fupi!...

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Aisee umetukosea sana hili jukwaa, kama ni desturi yako, basi never under-estimate people here. Omba radhi tafadhali!!

  Okay, back to topic, as Nyakwec's Bro said, sioni kama ni sababu ya msingi kusema hiyo ni long domain, kwa watu wenye uelewa, wanajua maana ya hizo ext. go.tz, or.tz, co.tz, ac.tz
  co.za, The Presidency | Home, University of KwaZulu-Natal, (what you are saying is urefu ni hizo herufi mbili au tatu..) I beg to differ SamJet, unless kama you are just excited to have one pronto.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  bado nafigure out jinsi ya kujenga mfumo wa malipo online ambao utaaccept m.pesa, tigopesa, airtel money online kwa ajili ya manunuzi coz nahisi ndo njia rahisi kufanya manunuzi kwa sasa, wadau wangu NingaR, SamJet, GIVENALITY, leh, e2themiza, MziziMkavu mnadhani this can achieved?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu C6 upo juu wewe katka mambo hayo endelea tupo tunakuunga mkono.......
   
 12. Given Edward

  Given Edward Verified User

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 862
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kusajili domain ya .tz inawezekana na Tanzania wamepewa hii TLD. However, TZNic wanasajili third-level domain via hii .tz. Sijajua kama wanafanya kwa kudhamiria au kama imewabidi ila ninachojua ni kwamba, if they're willing to register domains with .tz, they can. Details kuhusu .tz hizi hapa:
  TZNic pia wana uwezo wa kusajili domains hizi:

  • .co.tz: Za biashara
  • .ac.tz: kwa vyuo vinavyotoa baccalaureate degrees
  • .go.tz: web za serikali
  • .or.tz: not-for-profit organizations
  • .mil.tz: hii hutumika kwa website za jeshi la Tanzania PEKEE.
  • .sc.tz: website za shule za primary na secondary (ingawa sijaona bado shule zitumiazo hii extension)
  • .ne.tz: network infrastructure
  Tarehe 14 February 2012, sechond-level domains ziliongezwa:


  • .hotel.tz - Web za mahoteli
  • .mobi.tz - site za simu (manase na wenzake wangeacha kutumia wen.ru za warusi, I'm just saying)
  • .tv.tz - website za mashirika ya television (kama EATV, ITV, StarTV na wengine)
  • .info.tz - hizi ni kwa ajili ya kutoa information resources (Kama Tanzania kungekuwa na labda online Directory basi ingetumia hii)
  • .me.tz - sijajua bado matumizi yake.... :(

  Jambo jingine linalofanya hizi domain zisitumiwe sana ni bei yake. The payment ya .co.tz ni pound 99/year! Tunapenda sana kukuna web technology ya TZ yakini tubebane sasa.
  [TABLE]
  [TR="class: odd"]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 13. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,451
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Inshort hizo domain ni gharama sana kulinganisha na nyingine, wakati .com inauzwa 22,500 basi .co.tz inauzwa 30,000. Ni dhahiri mtu atanunua .com tu
   
 14. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,225
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa nzuri mkuu.
  Masahihisho kidogo hapo pekundu, Shule ya Sekondari META iliyopo jijini Mbeya wanatumia hicho kikoa cha .sc.tz.
   
 15. Given Edward

  Given Edward Verified User

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 862
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Thanks mkuu, sikusema hakuna ila sijaona. Hata hivyo, only 1 of hundreds of schools still isn't enough.
   
 16. SamJet

  SamJet Senior Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  With a blink of an eye, TES, kinachomatter sana hapo ni security.....
  Pia idea hiyo nimeipenda mnooo. This idea resembels pesapal inkenya, right??? sema pesapal is too much complicated. You can simplify this by using only few MOBILE payment gateways, kam M-PESA, AIRTEL MONEY, ZAP N.K
   
 17. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,451
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Ila mi nadhani wakiwezesha malipo kwa MPESA ama Tigo pesa basi wanaweza weka mchakato wa kuingiza zile receipt code. Na kama kawaida ikawezeshwa within 24Hours. Pia bei ipungue, mfano .in domain zinauzwa kwa nje ya india lakini ndani ya india bei ni rahisi sana.
   
 18. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  inakuaga .gov kama sijacrame
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  mhmmm!!! Aisee mkuu kwenye hilo swala la registrers na mfumo wa kulipia domain hapo mimi naomba nipingane na wewe kwa sababu mimi sijawahi kupata shida yoyote katika kulipia na kuregister domain yangu...huwa natoa order na kulipia kwa njia ya Airtel Money na M-Pesa na ndani ya 24 hrs domain yangu inakuwa imeshasajiliwa...Sasa sijui wewe hiyo ya kwako umeitoa wapi.

  na kuhusu domain extension ya Tanzania nadhani kuna vitu ambavyo unapaswa kuvifahamu na ukishavifahamu hutoongea tena hilo unaloliongea sasa hivi. Kila domain extension unayoiona imewekwa kwa ajili ya kuwalenga watu wa aina flani...eg: .com domain imelenga commercial organizations, .net imelenga organizations involved in networking technologies.

  Sasa usione hao tzNIC walioweka different .tz domain extension ni wajinga. Soma kwanza uelewe ndio uanze kutoa maoni yako.
   
 20. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Wazo lako ni zuri sana mkuu na ninaliunga mkono kwa 100% lakini kabla ya kwenda mbali embu jiulize maswali yafuatayo; unadhani ni watanzania wangapi ambao wanaweza kupata access ya internet? unadhani ni watanzania wangapi wenye ufahamu wa mambo ya computer? Je unadhani njia hiyo itarahisisha kwa namna moja au nyingine watu kulipia bill zao au ndio itazorotesha huduma hivyo? nadhani katika kuyajibu maswali hayo wewe mwenyewe unaweza kupata picha kama hiyo huduma inaweza kufanikiwa au la. Kwa sasa nadhani mfumo huu wa kulipia kwa njia ya simu wa kawaida unafaa na ni wa haraka zaidi kuliko huo wa internet...labda kama itaanzishwa huduma tofauti na hiyo ambayo itakuwa bora zaidi kuliko hiyo ila kwa hali ya nchi yetu kwa sasa sidhani kama njia hiyo itafanikiwa sana.
   
Loading...