Why Mkapa alimchukia sana Chachage Chachage (R.I.P)

Nyerererist

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
438
5
Tukiwa tunaelekea miaka miwili toka Mpiganaji Chachage Chachage Afariki dunia,,Naomba tukumbushane mambo machache yaliyowahi kumkuta au aliyowahi kuyaongea Chachage katika harakati zake...

Moja ya vitu vinavyonifanya leo hii nimkumbuke ni kitendo cha yeye kuchukiwa hadharani na rais wa wakati huo bwana Mkapa hadi kufikia kusema
"Watanzania tusiwe kama Chachage Chachage maana yeye kila siku anakosoa tu na kuangalia mabaya kwa serikali"

Yote hayo yalitokana na chachage kua anapiga kelele sana katika vitendo vyote visivyokua vya kheri kwa jamii ya watanzania.

Je, tukiangalia yanayomkuta Mkapa sasa hivi je, Chachage alikua na uwezo wa kuona mbali zaidi?????

KARIBUNI
 
Yeye Alikuwa Na Haki Ya Kusema Hivyo Lakini Wasomi Wengi Wanasikitisha Sana Walivyokuwa Na Moyo Wa Kusema Makosa Ya Wenzao Wakati Hawatoi Suluhisho La Matatizo Hayo Wanayoyakosoa Kazi Ni Kukosoa Na Kuingia Mitini Akilazimishwa Basi Atakuja Kuomba Msamaha Yaishe Kwahiyo Alichosema Mkapa Namuunga Mkono Asilimia Mia Na Zaidi

Huyo Msomi Angekuwa Analalamika Nakutoa Suluhisho Sidhani Kama Mkapa Angemchukia
 
Naweza kukubaliana na wewe kwa asilimia kadhaa,,but kwa upande mwingine sikubaliani na wewe kutokana na wanasiasa wa Tanzania kutothamini mtazamo na maoni ya wasomi..Kwa mfano mzuri na mdogo swala la Richmond wataalam (Wasomi) waliikataa hiyo kampuni but wanasiasa wakalazimisha hadi likapita na kutusababishia hasara kubwa...

On the other hand nani hata siku moja anakubali maoni ya wasomi kuhusu suala la Zanzibar...So naweza kusema wasomi tunao wazuri na wanatoa maoni kwa ajili ya masuluhisho mbalimbali but wanasiasa hawayafuati
 
Ndugu yangu SHY, wanaosema hivyo yaani "wanaolalamika bila kutoa suluhisho hawasaidii" wao mara nyingi wanakuwa na matatizo. Kama mtu akilalamika serikali kuwa na ufisadi, suluhisho ni kupambana nao na kuacha ufisadi, kama mtu akilalamika kuwa serikali ni chanzo cha watu kuwa maskini inachotakiwa kufanya ni kuwaondolea watu umaskini, pamoja na kwamba watu wanasiasa walioambiwa ukweli walimchumkia chachage mimi naona aliyokuwa anasema yalikuwa kweli.
Naona sasa yameanza kuonekana kweupe.
Sasa kama na wewe unasema hivyo ntakushangaa sana. Ukiingia madarakani ina maana una mbinu za kutondolea umaskini sio uulize sulihisho kutoka kwa aliye nje. Na yeye alikuwa free kusema kwa sababu hakuwa na political ambition, kwa hiyo hakuwa mnafiki kama walivyo wengine, ambao wanajua 1+1=2 lakini wanakubali kusema 1+1=3 just to please others so as wakapewa nafasi za kuteuliwa.
 
Bongolander thats is,,siku zote kazi ya Political analyst kama Chachage ni kutoa maoni au kuongea kwa kutumia theory mbalimbali...ndani yake ndio kunakua na suluhisho...Siamini maneno ya SHY kwamba Chachage alikua anapiga kelele bila kutoa suluhisho si kweli hata kidogo...Suluhisho linakua mikononi mwa wanasiasa wanaoongoza serikali..

Chachage alipigia kelele utaratibu wa ubinafsishaji wa mashirika ya umaa na rasilimali mbalimbali za nchi.. na wananchi wengi hawakumuunga mkono...Madhara yake ndio tunaanza kuyaona leo yale yaliyotendeka wakati Chachage akiwepo yaani Kiwira, TICTS, Migodi, Ununuzi wa Rada etc. SHY sikubaliani na mtazamo wako
 
SHY,
Unajua mkuu haya maneno ya kusema watu hawatoi suluhisho ni mchezo wa siasa ambao binadamu wengi huwa tunautumia baada ya madhara kutokea.
Ningependa sana utuonyeshe pale Chachage alipolaumu serikali bila kutoa suluhisho maanake isiwe tu tunajaribu kumpamba Mkapa.
Mkapa anajulikana kwa kiburi hasa ktk awamu yake ya Pili.. swala la nyumba za serikali lilizungumziwa sana na wengi walitoa ushauri.. hakukubali kwa sababu mkewe alikuwa mmoja watu waliojipanga, hivyo utaonekana mwenye wivu ma mchawi kwa mafanikio ya mkewe wakati swala la kuuza nyumba za serikali halihusiani kabisa na sisi kumtazama mkewe.

Swala la miundombinu kutouzwa iwe NBC, ATC ama mashrika mengineyo kubinafsishwa yalizungumziwa sana lakini hakumsikia mtu isipokuwa maslahi ya kundi lake yaliwekwa mbele.. Hivyo kila mtu aliyezungumza nje ya ubinafsishaji wa miradi hii alionekana mchawi. Mkuu tumebinafsisha hadi mbuga zetu kweli hapa hapa unataka suluhisho?...tumebakiwa na hiyo Ngorongoro na Serengeti tena basi baada ya kelele nyingi sana za wananchi. Madini,gas na kadhalika unafikiri watu hawakutoa mawazo yao?..

Haya mara ngapi tumeomba serikali kuwekea mkazo kilimo, Uvuvi na ufugaji vitu ambavyo vinawahusu wananchi moja kwa moja kwa aslimia 80..Tumesema miaka nenda rudi kipi alichokifanya.. Maendeleo siku zote huanzia shinani huko chini kwa wananchi ambao kama wao watakuwa na kipato cha kutosha wataweza kununua mali nyinginezo hivyo kukuza uchumi wa nchi lakini wapi?.. tunachoona ni imports tu ambazo zinategemea asilimia 20 ya middle class na wenye nacho, kwa sisi watoto wa wakulima tuna aagiziwa chakula!..
Leo nguvu yote ipo ktk Madini na Utalii ambavyo vinachangia kidogo sana ktk mfuko wa Taifa. wanachokifanya wanasiasa ni kutupa hesabu kubwa ya mauzo (mchango ktk GDP) hali fedha zote zinaingia mifukoni mwa wageni ktk accounts za mashirika mama yao ambayo yako nje.
Hapa mkuu mnataka ushauri gani?..
 
kwa ufupi watu waliowahi kupata nafasi ya kumsikiliza au kusoma machapisho ya Chachage watakubaliana na kwamba yanayotokea yote aliyapigia kelele miaka ya 2000-2003 hadi akatunga hadithi ya "makuadi wa soko huria". Wanasiasa wetu hasa wa CCM walimuita "mpiga kelele" ......leo hii vikao ni kila kukicha mara wengine wameamua "kuroga" hadharani...R.I.P Chachage
 
Ndugu SHY,

Inaelekea hukumbuki vizuri au umeamua kusahau mambo mengi yaliyotokea kipindi cha che Mkapa na jinsi watalaam walivyokuwa wakishauri na kutoa alternatives, lakini yeye alishia kuwadhihaki (tena siyo Prof. Chachage tu) kwa kuwaita wasomi mchwala. Pia ukumbuke kuwa mara nyingi aliwachanganya pamoja na waandishi wa habari na wapinzani.

Jaji Kisanga (jaji makini mpaka akamwamini kumpa kazi ya kuongozi kamati ya white paper) alimtukana waziwazi mbele ya wana ccm wenzake kwa sababu tu kamati yake ilitoa tathmini ya maoni ya watu na kuelezea umuhimu wa kuwa na muungano wa serikali tatu badala ya mbili ya hivi sasa.

Talk of Prof. Haroub Othmani juu ya mpasuko wa Zanzibar, ongelea ubinafsishaji wa NBC na baadaye iliyokuja itwa NMB. Ulitaka ushauri gani watu watoe ili ukubaliane nao. Au umesahau alivyoivunja board ya NMB iliyokuwa chini ya Mhe. Kaduma??? Kumbuka kamati ya Bunge ya uchumi iliyokuwa chini ya Mhe. Njeru Kasaka? Kumbuka tume ya rushwa ya Mhe. Warioba...watalaam mbalimbali walitoa ushauri wa kila hali namna ya kushughulikia lakini kila che Mkapa alipopandwa jukwaani aliishia kuwa ponda kila mtu. Sanasana akaishia kumfuatilia Mhe. Kiula na katibu wake lakini ni wazi kuwa hawakuwa pekee waliokuwa wachafu wa rushwa. Hii itaendeleapia kwa aliemuachia kijiti...Kikwete.

Ingawa huyu hajaonesha wazi kuwadhihaki wasomi, waandishi, ila kidogo kwa wapinzani, lakini taratibu wameanza kujifua nguo wenyewe. Kumbuka kiwete mara nawafahamu wala rushwa wote, nawapa muda wa kujurekebisha...mpaka leo kimy. Mara napambana na madawa ya kulevya, wenye majina waniletee..mpaka leo kimya. Sana sana naye kapambana na Prof. Mahalu. Inaelekea hawa viongozi wetu wanakuwa na visasi na baadhi ya watu. Kumbuka baada ya wapinzani kutaja majina ya mafisadi na joto kupamba kila kona ya nchi, msanii huyu (Kikwete) aliwahi kusema kuwa makelele ya wapinzani hayamnyimi usingizi, ingawa ukweli si hivyo.

Pia tatizo ambalo nahisi linawasumbua ni kule kuona majina ya wahusika wakuu ni ya wale waliowasaidia sana kuwaweka madarakani sasa wanaishia kuona aibu na kulipa fadhila.

NB: Ni vizuri watu wakaelewa kuwa vita hii ya ufisadi inayoendelea haijaanzishwa na system ya watawala bali ni pressure groups zilizo nje ya mfumo, na kizuri zaidi moto umewashwa na wanashindwa kufunika kombe ili mwanaharamu apite.
 
Last edited:
Kwa kweli mie simhurumii hata kidogo mkapa hata akinyongwa....alikua anawadharau sana wataalam yeye na vilaza wenzake kina SUMAYE, LOWASA na Wafanyabiashara waliokua marafiki zake.
 
Yeye Alikuwa Na Haki Ya Kusema Hivyo Lakini Wasomi Wengi Wanasikitisha Sana Walivyokuwa Na Moyo Wa Kusema Makosa Ya Wenzao Wakati Hawatoi Suluhisho La Matatizo Hayo Wanayoyakosoa Kazi Ni Kukosoa Na Kuingia Mitini Akilazimishwa Basi Atakuja Kuomba Msamaha Yaishe Kwahiyo Alichosema Mkapa Namuunga Mkono Asilimia Mia Na Zaidi

Huyo Msomi Angekuwa Analalamika Nakutoa Suluhisho Sidhani Kama Mkapa Angemchukia

Tatizo sion wasomi wengi. Tatizo ni ninyi mnaowapima wasomi kwa kusoma maoni ya magazetini na kuamini propaganda za wanasiasa.

Hakuna ukweli wowote kuwa Prof Chachage alikuwa akikosoa tu bila ya kutoa suluhisho. Wakati wote alikuwa akitoa masuluhisho, yawe katika mihadhara, makala magazetini na zaidi katika maandiko yake kisomi. Tatizo wanasiasa wanakosa guts za kutambua masuluhisho ya kisomi kwani mengi yao yanahatarisha maslahi yao binafsi na maslahi ya makundi yao kisiasa/kiuchumi.

Hivi SHY umewahi kusoma andiko lolote la Prof Chachage? Ama umewahi kufanya juhudi zozote za kuona maandiko yake? Kumbuka platform ya wasomi sio katika mikutano ya kisiasa ama mbele ya vyombo vya habari bali katika mijadala ya kisomi na maandiko yao.

Ni wazi wanasiasa kama MKAPA aliyekuwa akiamini sera ya Utandawazi(chachage alimwonya kuwa huwo ni utandandawizi) na Ujaririamali (wasomi wanaamini Ujasiri wa kuiba mali) hawakuwa tayari kusikia ya wasomi kwani sio wote walikuwa wakiongea yale watakayo kuyasikia ambayo yangekuwa yanahalalisha ujinga wao.

Cha kusikitisha hata Kikwete aliyemdhihaki MKAPA kwa kumtambua na kumpa kazi nyeti Kamarade Chachage ambayo alifariki akitekeleza naye pia ameonyesha kukusa guts za kutekeleza maoni ya kisomi ya Chachage na wenzie.

Kwa hiyo kaka, ni muhimu kuwapima wasomi kwa kujua/kusoma maandiko yao kwa umakini na sio kukimbilia kuamini propaganda za wanasiasa haswa wale mafisadi walitukuka kama alivyonyesha Mzee wetu MKAPA ambaye ametuangusha wengi hata kama hatujawahi kuwa waumini wake kisera na kiitikadi......

Tanzanianjema
 
Mkapa hakumchukia Marehemu Chachage peke yake, Mkapa aliwachukia wasomi wote wa UDSM.Aliwahi hata kuwatukana kwamba wao si lolote wala chochote wamekosa mahali pa kwenda ndo maana wako TZ.
 
Hivi SHY umewahi kusoma andiko lolote la Prof Chachage? Ama umewahi kufanya juhudi zozote za kuona maandiko yake? Kumbuka platform ya wasomi sio katika mikutano ya kisiasa ama mbele ya vyombo vya habari bali katika mijadala ya kisomi na maandiko yao.
......

Kwa hiyo kaka, ni muhimu kuwapima wasomi kwa kujua/kusoma maandiko yao kwa umakini na sio kukimbilia kuamini propaganda za wanasiasa haswa wale mafisadi walitukuka kama alivyonyesha Mzee wetu MKAPA ambaye ametuangusha wengi hata kama hatujawahi kuwa waumini wake kisera na kiitikadi......

Tanzanianjema

Huo ndio ukweli inabidi Shy utafute hata chapisho moja la Chachage,,kama uko interested niko teyari kukutumia machapisho kadhaa uone masuluhisho aliyoyatoa Chachage,
 
Mkapa hakumchukia Marehemu Chachage peke yake, Mkapa aliwachukia wasomi wote wa UDSM.Aliwahi hata kuwatukana kwamba wao si lolote wala chochote wamekosa mahali pa kwenda ndo maana wako TZ.

Is this serious? ebwana eeeehhh..........sasa mbona wengi wao walikua wanajikomba sana kwake??? Lakini anyway ndio utawala wa nchi zetu no way out usipojikomba kibarua kinakua hatiani...Mkapa alikua Dictator aise
 
Nimesoma Sana Na Nimehudhuria Sana Mihadhara Na Matamasha Yaliyomkutanisha Yeye Pamoja Na Wasomi Wengine , Wengi Hawakuwa Na Lolote Zaidi Ya Kauli Toto Za Woga Na Zisizokuwa Na Uhakika Wowote Kwa Maendeleo Ya Nchi Hii Ndio Maana Wengi Wakiondoka Na Maandiko Yao Yanawekwa Kapuni .

Mpaka Sasa Hakuna Anayeweza Kunishawishi Kwamba Amewahi Kutoa Suluhisho La Likaweza Kutatua Kitu Fulani Katika Maisha Ya Mtanzania Wa Kawaida Kule Kijijini Zaidi Ya Kulipwa Hela Za Walipa Kodi Na Wao Kuendelea Kutumbua Maisha .

Hatupendi Hivi Na Ndio Maana Mkapa Alioona Haya Akawapa Onyo Kali Kuanzia Hapo Walishika Adabu Naona Siku Hizi Wameanza Kufikiria Kabla Ya Kuandaa Hiyo Mihadhara Na Kauli Zao Zingine Ninazotishia Maslahi Kitaifa
 
Is this serious? ebwana eeeehhh..........sasa mbona wengi wao walikua wanajikomba sana kwake??? Lakini anyway ndio utawala wa nchi zetu no way out usipojikomba kibarua kinakua hatiani...Mkapa alikua Dictator aise

NDIO MAANA NIKASEMA HUKO MWANZO KWAMBA TUWE MAKINI SANA TUNAVYOJARIBU KUWALISHA WATANZANIA MAMBO MABAYA NA YA AJABU KUHUSU VIONGOZI WETU WA SASA NA HATA WALE WALIOPITA , UNASHANGAZA SANA HATA WEWE UNAVYOTHUBUTU KUMWITA MKAPA DICTATOR HII NI AJABU SANA .

KAMA UNAMWITA MKAPA DICTATOR BASI HATA MADA HAIFAI KUENDELEA NA HICHO NDICHO ULICHOKUWA UNATAKA TANGIA MWANZO
 
SHY,
Mkuu unachekesha sana!
sasa kama hizo theory zilikuwa hazina uzito zikatupwa kapuni, mkaendelea na theory zenu ambazo zimeturudisha nyuma zaidi baada ya kuwa applied huoni kama hapa suluhisho halikutolewa na either theory!..
Kisha basi afadhali ile uliyotupa kapuni, pengine ingeweza kufanya kazi kama ingetumiwa.. Tatizo ni kwamba mliitupa ktk jalala hivyo hamkumbuki hata ilikuwa anasema kitu gani..
Mkuu hiyo ni dharau kubwa kwa kiongozi wa nchi kutupa kapuni mapendekezo ya watu wengine. Pia mkuu samahani inaonyesha wazi kuwa una dharau fulani kwa baadhi ya watu hivyo maandishi yao hayawezi kuwa yanaweza kujenga kitu...
Sii tabia nzuri mkuu jaribu kujitazama vizuri kwani kiongozi bora huanzia ktk maswala madogo mdogo kama haya.
 
Nimesoma Sana Na Nimehudhuria Sana Mihadhara Na Matamasha Yaliyomkutanisha Yeye Pamoja Na Wasomi Wengine , Wengi Hawakuwa Na Lolote Zaidi Ya Kauli Toto Za Woga Na Zisizokuwa Na Uhakika Wowote Kwa Maendeleo Ya Nchi Hii Ndio Maana Wengi Wakiondoka Na Maandiko Yao Yanawekwa Kapuni .

Mpaka Sasa Hakuna Anayeweza Kunishawishi Kwamba Amewahi Kutoa Suluhisho La Likaweza Kutatua Kitu Fulani Katika Maisha Ya Mtanzania Wa Kawaida Kule Kijijini Zaidi Ya Kulipwa Hela Za Walipa Kodi Na Wao Kuendelea Kutumbua Maisha .

Sidhani kama una uhakika na kauli zako,,,au naomba utufafanulie nini maana ya "Suluhisho" kwa upeo wako? Maana sielewi mtazamo wako unaelekea wapi kutokana na kutolitumia vyema hilo neno
 
NDIO MAANA NIKASEMA HUKO MWANZO KWAMBA TUWE MAKINI SANA TUNAVYOJARIBU KUWALISHA WATANZANIA MAMBO MABAYA NA YA AJABU KUHUSU VIONGOZI WETU WA SASA NA HATA WALE WALIOPITA , UNASHANGAZA SANA HATA WEWE UNAVYOTHUBUTU KUMWITA MKAPA DICTATOR HII NI AJABU SANA .

KAMA UNAMWITA MKAPA DICTATOR BASI HATA MADA HAIFAI KUENDELEA NA HICHO NDICHO ULICHOKUWA UNATAKA TANGIA MWANZO

Ni mtazamo wako son,,,,kama unaona mada haifai kuendelea sio lazima uendelee kuwepo...hapa tunabadilishana mawazo na sio kudharauliana na kuambiana maada haifai
 
SHY,
Mkuu unachekesha sana!
sasa kama hizo theory zilikuwa hazina uzito zikatupwa kapuni, mkaendelea na theory zenu ambazo zimeturudisha nyuma zaidi baada ya kuwa applied huoni kama hapa suluhisho halikutolewa na either theory!..
Kisha basi afadhali ile uliyotupa kapuni, pengine ingeweza kufanya kazi kama ingetumiwa.. Tatizo ni kwamba mliitupa ktk jalala hivyo hamkumbuki hata ilikuwa anasema kitu gani..
Mkuu hiyo ni dharau kubwa kwa kiongozi wa nchi kutupa kapuni mapendekezo ya watu wengine. Pia mkuu samahani inaonyesha wazi kuwa una dharau fulani kwa baadhi ya watu hivyo maandishi yao hayawezi kuwa yanaweza kujenga kitu...
Sii tabia nzuri mkuu jaribu kujitazama vizuri kwani kiongozi bora huanzia ktk maswala madogo mdogo kama haya.

Mimi sina dharau kama unaona nina dharau huo ni mtizamo wako huo ndio tunaita ubinafsi sasa kama unataka nisipingane na maoni yako wewe sema tu hakuna tatizo kuanzia sasa sema anayepingana na maoni yangu yeye anadharau , anajisiikia na ni fisadi namba moja .

Well ita vyovyote napenda kukutaarifu hautafika mbali wala kudoea chochote kile kama msimamo wako ni huo kama unavyo hapo juu , kama propaganda zinaendeshwa kwa njia hiyo basi upinzani umekwisha

Bwana Mkandara mimi utaniona mwaka 2015 moshi vijijini au jimbo la ubungo nafikiri nitatoa funzo nzuri sana kipindi hicho niko tayari
 
kwa mtazamo wangu Suluhisho ni pale kunakua na alternatives nyingi then you choose the best kwa ajili ya kutatua tatizo flan..Chachage na wasomi wengi wamekua waki suggest alternatives mbalimbali but no one cares wanasema wanatekeleza ilani ya chama ambayo huandaliwa na Mzee Kingunge
 
Back
Top Bottom