Why Magufuli administration misses the point on government splurge

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
179,521
2,000
HABARI MPYA YA MJINI!!!

GARI LAKO SASA LINAWEZA KUTUMIA GESI ASILIA


Utangulizi:

Taasisi Tecknologia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na wadau wengine wa gesi asilia tunaongeza mfumo wa gesi asilia kwenye magari yanayotumia petrol. Mfumo huu unamwezesha mwenye gari kuwa na uwezo wa kutumia gesi asilia au petrol kulinga na upatikanaji wake. Kwa sasa tunafunga magari yote ya petrol kuanzia madogo IST hadi makubwa V8. Pia tumeanza kufunga gesi asilia kwenye daladala.

Gharama za kuweka huu mfumo:

Gharama inategemea na ukubwa wa injini yaani idadi ya cylinder za injini yako. Mfano kwa gari zenye;
1. cylinder 4 gharama ni 1.8m,
2. Cylinder 6 gharama ni 2.2m
3. Cylinder 8 gharama inaenda mpaka 2.5m.
Hata hivyo kuna baadhi ya gari gharama hizi inaweza zidi kutokana na mfumo wa injini (kama brevis, crown na voxy ambayo injini zake ni GDI)

Faida za huu mfumo:

1. Unafuu wa gharama za uendeshaji;
Kutumia gesi unapunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 40 mpaka 50. Bei ya gesi asilia iko chini sana, ukilinganisha na petrol. Mfano 1kg ya gesi ni sh 1500/= ukilinganisha na sh 2200/= kwa lita ya petrol.
1kg ya gesi unaweza kwenda zaidi ya km 20, na kwa mtungi wa 15kg ambao ni sh 22,500/= unaweza kwenda zaidi ya km 200.
2. Kupunguza uchafuzi wa mazingira;
Gesi ni safi ukilingalinisha na petrol au diesel.
3. Kuongeza kipindi cha kufanya matengenezo ya injini yako;
Kwa kuwa gesi asilia ni safi, basi hata injini yako inakuwa salama zaidi. Mfano kama ulikuwa unafanya matengenezo kila baada ya km 3000, kwa kutumia gesi asilia unaweza kufanya hata baada ya km 9000.
4. Gesi asilia ni salama zaidi;
Gesi asilia ni salama zaidi ukilinganisha na petrol kwani inahitaji joto kubwa sana ili iweze kuwaka ukilinganisha na petrol.


Mahali pa kubadilishia mfumo:

Kwa sasa Tanzania nzima ni sehemu moja tuu inafanya kazi ya kubadili, nayo ni Taasisi ya tecknologia Dar es Salaam (DIT).

Mahali pa kujazia Gesi:

Kwa sasa mahali pa kujazia gesi ni ubungo maziwa. Hata hivyo serikali iko mbioni kuongeza vituo zaidi ya 5 sehemu mbalimbali hapa Dar es salaam.

Hitimisho:
Taasisi ya Tecknolojia Dar es salaam DIT inakukaribisha sana uje uweke mfumo wa gesi asilia kwenye gari lako, kwani ni nafuu na salama zaidi.

Asante
Dr. Esebi Nyari
Mratibu wa gesi asilia- DIT
0755821240

Benjamin Kamtawa
0717962127

----------------------------------
Please share

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom