Mazungumzo baina ya Marafiki wawili Wa Huko Mbinga.
Bwana Ndunguru &
Bwana Komba.
Ndunguru: Naumwa sana rafiki yangu Komba nimelazwa wiki ya pili sasa sina pesa kabisa.
Komba: Unaumwa nini Kaka?
Ndunguru: Homa imenibana kweli aisee na naona pesa za kugharimia matibabu zinaniishia kabisa.
Komba: Ningekusaidia Bro bahati mbaya kuna kiwanja tulipatana na muuzaji majuzi ndo nataka kesho nikanunue.
Ndunguru: Sawa Kaka, ila siko vizuri kabisa kipesa. Nisaidie walau kidogo Ndugu yangu.
Komba: Iko hivi, bajeti zote tunazopanga Mimi na Mke wangu, huwa hazivunjwi Ndugu yangu. Nimebakiwa na hiyo Milioni 5 tu ya kiwanja.
Ndunguru : Ukinisaidia hata laki mbili tu inatosha Rafiki yangu. Nikipona tu nitakulipa, nitazirudisha.
Komba: Hapo itakuwa ngumu kidogo, na vipi umejaribu kuupigia Uongozi wa Chama chetu cha Wafanyabiashara?
Ndunguru : Ndio, wamenichangia 30,000 tu.
Komba: Anzia hata hiyo Bro. Get well soon.
BAADA YA NDUNGURU KUFARIKI
Komba : Bw. Ndunguru alikuwa rafiki yangu mkubwa tulioshibana, tuliyeshirikiana katika mambo mengi sana, hivyo Mimi kama Rafiki aliyekuwa zaidi ya Ndugu natoa mchango Milioni moja cash.
Chama cha Wafanyabiashara: Tumehuzunishwa sana na taarifa hii, kwani Bw. Ndunguru alikuwa Mtu muhimu sana katika Chama chetu, ameacha pengo kubwa, halitazibika.
Sisi tutagharamia gharama zote za hapa msibani, kuanzia chakula, usafiri hadi mazishi yote yaishe.
UJUMBE WANGU KWENU
Naomba ifikie kipindi tubadilike kwa kuanza kumthamini Mgonjwa kuliko Maiti. Yaani Mtu akishafariki, Marehemu ndio tunamuenzi sana kuliko alipokuwa Mgonjwa!!?
Maana kuthamini Maiti, Marehemu kuliko Mgonjwa ni unafiki uliopitiliza sana.
Huenda huyo Mtu angesaidiwa kwa nguvu kubwa kama inayoonekana kwenye mazishi asingefikia hadi kufa.
Kibaya zaidi ni pale ambapo Mtu hakuwahi kwenda hospitali kumjulia hali Mgonjwa makusudi kabisa, lakini anajifanya yeye ndo Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi na kutayarisha risala ndefu ya wasifu wa Marehemu.
MUNGU atuhurumie. Tujitafakari saana na Tubadilike jamani!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.