Why Magufuli administration misses the point on Government splurge

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,340
2,000
God not like a man who judges according to physical appearance but He judges according to what is in the heart
jicholauswazi_20210223_170727_1.jpg
jicholauswazi_20210223_170727_2.jpg
jicholauswazi_20210223_170727_0.jpg
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,340
2,000
Ifuatayo ni orodha mpya ya nchi 20 za Kiafrika zenye uchumi mkubwa kwa Pato ghafi la Taifa kwa mwaka huu wa 2021 (Top 20 Latest List of African countries ranked by GDP (nominal) in 2021).

1.Nigeria $466.88 billions

2.Egypt $374.89 billions

3.South Africa $317.19 billions

4.Algeria $147.323 billions

5.Morocco $112.220 billions

6.Kenya $101.048 billions

7.Ethiopia $95.588 billions

8.Ghana $69.757 billions

9.Tanzania $64.1231 billions

10.Angola $62.724 billions

11.Côte d'Ivoire $61.5022,billions

12.Democratic
Republic of the
Congo $46.062 billions

13.Tunisia $39.2263 billions

14.Cameroon $39.0361 billions

15.Uganda $37.733 billions

16.Sudan $32.576 billions

17.Senegal $24.4091 billions

18.Libya $21.8053 billions

19.Zambia $18.9091 billions

20.Mali $17.685 billions

N.B: katika list hii nchi 5 zimepanda ambazo ni Tanzania, Kenya, Algeria, DR Congo na Egypt. Nchi hizi uchumi wake umeimarika na kupanda daraja.

Pia nchi 6 zimeporomoka kiuchumi ambazo ni South Africa, Morocco, Angola, Sudan, Tunisia na Libya.

Pia taifa la Ghana ndio ambalo uchumi wake umukua kwa kasi na kupanda daraja kwa kasi kutoka taifa la 13 kiuchumi mwaka 2019 mpaka taifa la 8 2021.

Pia Egypt imeshika nafasi ya pili kiuchumi Afrika, imeiondoa South Africa nafasi hiyo.

Pia Egypt ndio taifa la pili ambalo uchumi wake unakua kwa kasi Afrika.

Pia unaweza kutembelea website hii kuona orodha ya nchi zote 55 za Afrika katika rank ya nafasi zao kiuchumi (see all 55 African countries GDP) https://lnkd.in/e85-VF4)

Chanzo cha taarifa hii ni kutoka shirika la fedha duniani pamoja na Bank ya dunia, tembelea website hii ya mchumi mahiri duniani Mark-Anthony Johnson kuona orodha mpya iliyotolewa mwaka 2021 Mark-Anthony Johnson on LinkedIn: #Africa #data #InternationalMonetaryFund | 47 comments
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,340
2,000
Dr Criss Cyrilo Writes:

NENDA ZAKO SHETANI!

Rais Magufuli ana jopo la Madaktari bingwa Tanzania. Wanamzunguka kuhakikisha anabaki katika afya bora. Hiyo ni kawaida dunia nzima, kwamba afya ya viongozi wa nchi inalindwa kwa kadiri inavyowezekana.

Rais Magufuli analindwa na makomandoo waliofuzu medani za juu za mapambano. Makomandoo hao wanaingia naye hadi Makanisani, na Misikitini pindi anapoingia. Hii ni kawaida kwa kiongozi wa nchi. Anapaswa kulindwa kwa 'udi na uvumba'.

Rais Magufuli analindwa na mitambo ya kisasa yenye teknolojia kubwa kabisa. Nayo anaingia nayo kanisani kumuomba Mungu. Hii pia ni kawaida.

Jambo lisilo la kawaida ni pale Rais anapotuambia tumtumainie Mungu kupambana na janga la Covid halafu anawananga wanaovaa barakoa.

Kuvaa barakoa ni mbinu mojawapo ya kupambana na Covid. Ni sawa na kuambatana na madaktari bingwa wenye vifaa tiba vya kisasa kabisa kila mahala ili kuwa na msaada wa kiafya mara tu unapohitajika. Ni sawa na kuzungukwa na walinzi waliofuzu medani za juu za mapambano. Ni sawa na kuambatana na mitambo ya ulinzi ya kisasa kila mahala.

Je! ikiwa Mungu anaweza kutulinda dhidi ya Covid bila sisi waja wake kuchukua hatua kama kuvaa barakoa, kwanini huyo Mungu asimlinde Magufuli bila madaktari bingwa, bila makomandoo na bila mitambo ya kisasa?

Mungu aliyepo kichwani mwa Rais Magufuli ni Mungu kigeugeu? Ni Mungu asiye na misimamo? Ni Mungu asiyejielewa?

Basi Yesu akamjibu Pilato; kutoka Yohane 18:36-37; akasema, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini sasa ufalme wangu si wa hapa.”

Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme.

Ufalme wa Rais Magufuli kama ulivyo ufalme wa Wafalme' wengine ni wa hapa duniani. Ndio maana anajilinda kwa mbinu za kidunia; Madaktari na teknolojia zao, makomandoo na teknolojia zao. Ni Mambo ya kidunia. Yesu hakulindwa na jeshi lolote kwakuwa hakuwa mfalme wa dunia. Yeye hakuwa wa dunia hii (kwa maneno yake mwenyewe). Ndio maana alikamatwa bila ukinzani, akasurubiwa bila ukinzani, akafa bila ukinzani.

Mwanadamu anayeamini kwamba Mungu anaweza kumlinda bila kujichujukulia hatua za kujilinda, atasurubiwa bila ukinzani, na atakufa bila ukinzani. Atakutana na kile alichokutana nacho Yesu, wakati yeye si Yesu.

Rais Magufuli anajua hilo, ndio maana analo jeshi la kumlinda - madaktari bingwa na vifaa tiba vyao, makomandoo na vifaa vita vyao.

Ajabu ni pale anapowashangaa watu wanaovaa barakoa kujilinda na Covid huku akihubiri eti Mungu hashindwi! Ni kweli Mungu hashindwi lakini Mwanadamu anashindwa. Mwanadamu asiyechukua hatua dhidi ya Covid atashindwa kwa sababu anamjaribu Mungu wake. Rais Magufuli anapojilinda dhidi ya hatari za kidunia kwa mbinu za kidunia anafanya sahihi, lakini anawazodoa wanaojilinda na Covid kwa kuvaa barakoa, ni kama anawataka wavue barakoa ili wamjaribu Mungu wao.

Mathayo 4: 5-7
''Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: ‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe.’” Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia: ‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.''

Usimjaribu Mungu wako kwa kutochukua hatua za kujilinda dhidi ya Covid eti kwa imani kwamba Mungu atakuokoa. Yesu alikataa kujitupa chini pamoja na kwamba maandiko yalisena malaika watamuokoa. Alikataa kumjaribu Mungu Baba.

Mathayo 4: 8-10
"Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake, akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.” Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani!

NENDA ZAKO EWE SHETANI. Mnafiki mkubwa shetani. Acha kujilinda kwa mitutu ya bunduki kwakuwa imeandikwa ‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe'.

Nawatakia Jumapili njema!
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,340
2,000
My Eyes Were Opened

It was as if I was blind. I must have heard many times that Jesus died for our sins. But I simply did not see it. I was spiritually blind. But when I understood the cross, my eyes were opened.
Since then, I have noticed that as I have attempted to pass on the message of ‘Christ crucified’, there are different responses. Sometimes very intelligent people simply cannot see it (see 1 Corinthians 1:23–25). On the other hand, I am often amazed at the understanding of others, including very young children. For all who see it, it is life changing: ‘to us who are being saved it is the power of God’ (1 Corinthians 1:18).
I think it is fascinating that in today’s New Testament passage, after Jesus has explained his death, we have the story of blind Bartimaeus having his eyes opened (Mark 10:46–52). He says to Jesus, ‘I want to see’ (v.51). Jesus replies, ‘“Go… your faith has healed you.” Immediately he received his sight and followed Jesus’ (v.52). The word used for healed is the same Greek word as saved (sozo).
Do you see it? The passages for today help us to see the significance of Jesus’ death.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom