Why do Tanzanians hate Maintenance?

SASATELE

Senior Member
Sep 12, 2011
167
89
Watanzania tuna tatizo sugu la lack of maintenance!! Ukiangalia barabara zetu unakuta mitaro ya maji taka imeziba na wahusika hawazibui, ukiangalia nyumba, kuta zimechakaa hazipakwi rangi miaka nenda miaka rudi. Ukimpangisha mtu nyumba yako hafanyi simple maintenance hata ya kunyonya maji taka anataka mwenye nyumba umfanyie kila kitu. Nyavu za mbu zimetoboka na wanawe wanapata shida eti ofisa wa benki na tai anasubiri hadi baba mwenye nyumba aje. Ukiangalia watu wanavyoteseka na vitambi utachoka, mtu kupanda ngazi anahema ulimi nje, ukiwaambia fanya mazoezi upunguze uzito na uwe fit uishi zaidi ya miaka 50 anakwambia ya nini tabu kukimbia/kujog kama kichaa? Nenda Gym basi, aah sina hela lakini bar hakosi!!. Yaani hakuna maintenance kuanzia public utilties hadi miili yetu watz. Jamani hili nalo ni sababu ya umaskini au culture? Tufanyeje tutoke hapo nasi tuyaendee maendeleo kama ya wenzetu?
 
HEla tu ya kuleta hicho kitu hatuna, ya maintanance tutapata wapi?
 
Tuna mtizamo usio sahihi kimaisha.
Ndo maana utatusikia tukisema fulani kaukata! kaula! nk. ikimaanisha huyo fulani maisha yameshamnyookea na hahitaji kuweka juhudi zaidi kupata maisha mazuri.

Tunasahau kwamba maisha ni mapambano yasiyoisha mpaka kifo. Kifo chenyewe kinapatikana kwa mapambano.

Kufanya ukarabati wa kitu chochote ni kukubali kupambana dhidi ya nguvu za maumbile ambazo siku zote zinataka kurudisha hali za vitu kuwa ghafi. Mfano ni kama kutu kwenye bati la nyumba, rangi kukosa mng'ao, mafuta ya kulainishia kukosa utelezi, mwili kukosa kinga dhidi ya maradhi nk.

Maisha yetu yanatakiwa yawe kama ya viumbe waishio kwenye miti ambao siku zote hujitahidi wasianguke chini hata wawapo usingizini.
 
HEla tu ya kuleta hicho kitu hatuna, ya maintanance tutapata wapi?

Kongosho,
Suala la kufanya maintenance sio hela bali ni attitude/mtizamo. Watz tunataka kila kitu tufanyiwe sisi tufurahie tu. Hii attitude ya "umwinyi" ni mbaya. Wafadhili wanatujengea miundombinu tunataka wafanye na maintenance? Unategemea tutatoka kwenye umaskini kweli. Nimetembelea mikoa yote ya humu Pwani nikaona hiyo attitude imeota mizizi. Kila mtu anaomba wafadhili waje wawasaidie. Nikawauliza ninyi mnaweza kufanya nini zaidi ya kuzaana? hawakuwa na jibu!!
 
Nadhani Prof. Mlawa alishafanya utafiti kuhusu hii hali, na kama sikosei sababu moja kubwa ya Watanzania kutokuwa na tabia ya kufanya ukarabati ni urithi wetu wa zamani wa kujenga nyumba za msimu. Siku za zamani vijijini watu walijenga nyumba za udongo zilizoezekwa kwa nyasi na mara nyingi hizi hazikuwa madhubuti sana. Baada ya muda zilichakaa na kudondoka. Jambo hilo halikuwa shida sana kwa vile kulikuwa na malighafi za kutosha na maeneo mengine ya kutosha kujenga. Kama kibanda kilidondoka, basi mwenye nyumba alisogea hatua chache tu na kujenga kingine. Kwa hiyo sababu kubwa ilikuwa ni urahisi wa kujenga.

Hata hivyo labda kuna sababu zingine zaidi.
 
Kuna rafiki yangu Mmarekani alikuja Tanzania miaka ya 80 wakati hali ya nchi ikiwa taabani kabisa na mabarabara yote yalikuwa mabovu sana. Aliniambia kuwa utafiti wake wa haraka haraka aligundua kuwa katika Kiswahili kuna neno "Tengeneza" lakini hakuna neno la Kiswahili la "Maintenenance". Kwa kiasi fulani nakubaliana naye. Maneno kama kukarabati, kukarafati, yalianza kujitokeza miaka ya 90 lakini bado nadhani hayana maana ya "Maintenance"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom