#COVID19 WHO: Zaidi ya 85% ya visa vya Covid-19 Afrika havijagunduliwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Visa sita kati ya kila visa saba vya ugonjwa wa korona havingunduliwi barani Afrika, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema.

Imefanya hesabu kulingana na fomula ambayo inaangalia vifo vilivyorekodiwa na viwango vya vifo vya visa vya ugonjwa huo.

Kufikia sasa ni visa milioni nane tu vya Covid vimerekodiwa lakini WHO sasa inakadiria kuwa takwimu halisi ni milioni 59.

Kwa jumla, watu pekee ambao wanapimwa ni wale wanaojitokeza kwenye vituo vya afya na dalili na wale wanaokusudia kusafiri nje ya nchi. Hii inamaanisha kuwa idadi kubwa ya visa vya watu wenye dalili ambazo hazionekani ipo na kusababisha maambukizi zaidi.

Ili kukabiliana na hili, WHO iinapendekeza ukaguzi zaidi wa kijamii katika nchi nane zinazolenga kufikia watu milioni saba na upimaji wa haraka katika mwaka ujao.

"Pamoja na upimaji wa kiwango cha chini , bado tunapofuka katika jamii nyingi sana barani Afrika ... Upimaji zaidi unamaanisha kutengwa kwa haraka, maambukizi kidogo na maisha zaidi kuokolewa kupitia hatua zinazolengwa," alisema mkurugenzi wa WHO wa Afrika Dr Matshidiso Moeti.

Burundi, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Guinea Bissau, Msumbiji, Congo-Brazzaville, Senegal na Zambia zitashiriki.

Kumekuwa na upungufu wa visa vipya vilivyorekodiwa hivi karibuni, na WHO inasema kwa sababu ya viwango vya chini vya chanjo,Covid bado ni tishio kwa wengi.

BBC Swahili
 
Ukiishi Africa ujue tayari una Kinga ya Asili kwa zaidi ya 50%. Hao waliosema COVID-19 itaua mpaka mizoga itapakae hawajatwambia kwa nini hiyo mizoga haionekani badala yake wanaleta episode za kuandaa mazingira ya biashara ya chanjo.
 
Katika hili naungana na Hayati magufurui. Hawajamaa kila siku wanatutafuta na kutuwwkea data ionekane africans ndo wagonjwa, kama tunaambukizwa na kupoma bila kujua kinawauma nini
 
Visa sita kati ya kila visa saba vya ugonjwa wa korona havingunduliwi barani Afrika, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema.

Imefanya hesabu kulingana na fomula ambayo inaangalia vifo vilivyorekodiwa na viwango vya vifo vya visa vya ugonjwa huo

Kufikia sasa ni visa milioni nane tu vya Covid vimerekodiwa lakini WHO sasa inakadiria kuwa takwimu halisi ni milioni 59.

Kwa jumla, watu pekee ambao wanapimwa ni wale wanaojitokeza kwenye vituo vya afya na dalili na wale wanaokusudia kusafiri nje ya nchi. Hii inamaanisha kuwa idadi kubwa ya visa vya watu wenye dalili ambazo hazionekani ipo na kusababisha maambukizi zaidi.

Ili kukabiliana na hili, WHO iinapendekeza ukaguzi zaidi wa kijamii katika nchi nane zinazolenga kufikia watu milioni saba na upimaji wa haraka katika mwaka ujao.

"Pamoja na upimaji wa kiwango cha chini , bado tunapofuka katika jamii nyingi sana barani Afrika ... Upimaji zaidi unamaanisha kutengwa kwa haraka, maambukizi kidogo na maisha zaidi kuokolewa kupitia hatua zinazolengwa," alisema mkurugenzi wa WHO wa Afrika Dr Matshidiso Moeti.

Burundi, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Guinea Bissau, Msumbiji, Congo-Brazzaville, Senegal na Zambia zitashiriki.

Kumekuwa na upungufu wa visa vipya vilivyorekodiwa hivi karibuni, na WHO inasema kwa sababu ya viwango vya chini vya chanjo,Covid bado ni tishio kwa wengi.

BBC Swahili

Watakuwa wana watulenga sote tunaokata moto ghafla.

Kwa hakika tangia March 2020 walioondoka hivyo idadi yao si ndogo.
 
Back
Top Bottom