WHO: Wanawake wengi hufa kutokana na utoaji mimba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,008
9,873
WHO na wadau wake wamefanya utafiti katika nchi 17 za Amerika ya Kusini na Karibea. WHO imeshirikiana na HRP yaani Human Reproduction Program ambacho ni chombo kikuu cha mfumo wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya utafiti katika uzazi wa binadamu ili kuboresha afya ya uzazi.

Nyongeza maalum ilitolewa hii leo Jumatano ambayo inaangazia kazi ya utafiti huu katika nchi 11 za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na katika Jarida la Kimataifa la Gynecology and Obstetrics (IJGO), inajumuisha nakala saba za utafiti na tahariri.

"Utafiti huu unaonesha safari tuliyonayo ili kuhakikisha huduma ya heshima na bora kwa wote baada ya kuavya mimba; pia inaonesha ni kiasi gani tunaweza kujifunza tunapojitolea kufanya kazi pamoja.” amesema Özge Tunçalp, Mshauri wa tiba wa WHO na HRP.
Taarifa zilizokusanywa kwa wanawake 23,000

Taarifa zilikusanywa kuhusu zaidi ya wanawake 23,000 wanaohudhuria vituo vya afya wenye matatizo yanayohusiana na uavyaji mimba katika nchi zilizofanyiwa utafiti.

Taarifa ya WHO imeeleza kuwa, “ingawa wengi wa wanawake hawa walikuwa na matatizo madogo au ya wastani yanayohusiana na utoaji mimba, bado kulikuwa na wengi ambao walikuwa na matatizo makubwa au ya kutishia maisha, hasa katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.”

Kutokana hali hiyo, nchi zimeshauriwa kuwa ni lazima zichukue hatua haraka ili kuhakikisha kuwa watoa huduma za afya na mifumo inaweza kutoa huduma bora kwa wasichana na wanawake.

Nchi ziongeze ufikiaji wa huduma bora za utoaji mimba katika ngazi zote huduma ya afya na kuhakikisha mbinu za kuboresha ubora wa huduma baada ya kuavya mimba zinatokana na ushahidi ili kuhakikisha kwamba: watoa huduma za afya wanatumia mbinu zinazopendekezwa; kukagua upatikanaji wa vifaa; na kufanya ukaguzi wa kimatibabu ili kuelewa vyema sababu za matatizo ya kiafya au matokeo mabaya.
 
Tofauti na kufa; utoaji wa mimba unasababisha watoto walemavu kama mimba ikijaribiwa kutolewa na ikakataa kutoka au ikijaribu kutolewa wakati kiumbe kimesha komaa, hapo mama mjamzito anakuwa ameshaharibiwa kinga za ujauzito kwa kuchezea/kujaribu kutoa kwa hivyo mtoto tumboni anakuwa ana maendeleo mazuri.

Unakuta mtoto anazaliwa mkono au mguu haupo sawa au macho haoni vizuri au mfumo wa upumuaji au sehemu flani flani haipo sawa katika mwili wakoe.. wadada/wamama hivyo sio vitu hata vya kujaribu
 
Back
Top Bottom