WHO: Vifo milioni 7 vyatokana na uchafuzi wa hewa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Shirika la Afya Duniani, WHO leo limeimarisha miongozo yake ya ubora wa hewa, likisema uchafuzi wa hewa kwa sasa ni moja ya kitisho kikubwa cha kimazingira kwa afya ya mwanadamu.

Shirika hilo limesema uchafuzi wa hewa unasababisha vifo milioni saba kwa mwaka na kwamba hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kupunguza uchaguzi huo.

Miongozo hiyo ina lengo la kusaidia kuwalinda watu na madhara ya uchafuzi wa hewa na inatumiwa na serikali kama kumbukumbu ya makubaliano yanayopaswa kutekelezwa.

Mara ya mwisho WHO kutoa miongozo kuhusu ubora wa hewa ilikuwa 2005, ambazo zilikuwa na matokeo mazuri katika sera za kupunguza uchafuzi wa hewa ulimwenguni.

Hata hivyo, WHO imesema katika miaka hiyo 16 ushahidi mkubwa umeonesha jinsi uchafuzi wa hewa unavyoathiri afya, kuliko ilivyoeleweka awali.

Chanzo: DW Swahili
 
Covid 19 mpaka leo imeua watu 4.7m! Uchafuzi wa hewa unaua watu 7m na watu wako busy corona business!
 
Nashukuru sana Shirika la Afya WHO kwa kutuoa muongozo na data nzuri kuhusiana na hii ishu ya Air Pullotion.

NEMC huu ndio wakati wenu sasa wakuacha kusinzia na kuanza kupambana na ishu ya uchafuzi wa Hali ya hewa kwa kutumia Environmental laws and Regulations. Kwa maana Viwanda vya Wahindi vinachafua mazingira kama Gari moshi la makaa ya mawe. Hili Tanzania pawe sehemu salama kwa kuishi kwa kizazi cha sasa na kijacho.
#ZeroEmission
 
Back
Top Bottom