Mkuu tukiangalia hapo kwenye RED , ina maana JK naye anamwandaa Ngeleja kushika uongozi maana alimpandisha haraka haraka hadi kuwa waziri kamili kwenye wizara nyeti ????Kikwete "aliandaliwa" kushika position ya juu kwenye Uongozi wa nchi mara tu Mzee Mwinyi alipopata nafasi ya kuwa Rais. Utakumbuka namna alivyopandishwa vyeo haraka na kuwa Waziri kamili (tena wa Wizara nyeti) baada ya muda mfupi. Kikwete hakuwahi kuwa chaguo la Mwl. Nyerere (kama ilivyokuwa kwa Mzee Mwinyi), na ni wazi alionekana mtu "sahihi" na "rahisi" "kumtumia" kubadili mfumo na kulegeza misimamo ya kizalendo ya awamu ya kwanza.
Mzee Mkapa "alisaidia" kum-expose Kikwete kwenye "siasa" na "fitna" za kimataifa wakati alipomteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje (huko bila shaka waliokuwa wanamwandaa walipata fursa ya kumwahidi misaada yao na kupata ahadi ya "kutimiziwa" mahitaji yao baada ya kupata U-Rais).
Mambo yanafunguka sasa na wa kulaumiwa ni sisi kwa kutokuwa "wasikivu", na bahati mbaya kuwa na utaratibu usiokidhi haja wa kuwapata viongozi wakuu.
Nimesoma hizi Wikileak diplomatic cables na kuona JK anavyoingizwa sehemu mbalimbali na kujikuta ninajiuliza hilo swali. Sijui wengine mmeona pattern fulani au mmejiuliza swali au kupata majibu ya swali hilo?
Inashangaza zaidi kwamba huyu mkulu alikuwa minister wa foreign affairs for 10 years of which hata kama alikuwa mzembe mzembe before, basi angejifunza mambo mengi kuhusu diplomacy!!!!!!!
Lakini mkuu mm wala sishangai na mbaya zaidi the guy has role-modelled plenty. Kwa hiyo huko mbele tutegemee even some worse reckless leaders kuliko hata yeye!!!! The trend and pattern that I see kuhusu taifa letu ni kuporomoka kwa maadili, kukosekana uwajibikaji, kukumbatia ujanja ujanja etc. Imagine juhudi kubwa mno zimefanyika kupindisha ukweli, to lower the leadership bar, and to convince the masses that what we have and what we are is the best. Na watu aina ya JK eti ndiyo tunaambiwa wanafaa kuongoza taifa hili. Cry my beloved country.
Kwa upande wangu hao jamaa hawahusiki na huyu jamaa kuingia madalakani kwake,huyu mkuu aliingia madalakani kwa mfumo wetu na jamii yetu ilivyojipanga na kwa msaada wa Rais wa awamu ya PILI kumjenga na kwa kuwa na bashasha la kupendwa [Charismatic=A person attracts, influences, and inspires people by their personal qualities.-].
Kidogo historia ya kule alikopita na malezi pia ni athari ambazo zinachangia kutoa zana mpya [Thsesis],na pia upenzi binafsi juu ya aina fulani ya life style.Mfano ukiweka aina mbili ya life sytle kati kuchagua uchina au umarekani hakika kwa mhusika atachagua umarekani kwa sababu ya haiba yake [personality].
Hivyo Tangu alipopata ufahamu na kwa kuwa mwanzoni enzi ya ujana wake,alipenda sana style ya uchina yaani ukomledi,lakini kadri alivyokuwa anakuwa na kukutana na changamoto nyingi za mabadiliko ya jamii na tabia za wakuu wake zikiwemo kuathiliwa kisaikolojia kama kweli lille tendo la Monduli lilikuwepo [ambalo kwa zama zile ilikuwa ni aina ya uzalendo kisha uzalendo wake unawekwa wazi kwa wahusika,na kwa kuwa yeye ni kijana mdogo wakati ule, pata picha alivyopona kwenye mtafaruku ule na wazee wale hakika,kwa kijana yoyote angejenga hasira za ndani kwa ndani na mfumo huo,
Kwa hiyo hawa wadau kawajua na kujihusha nao sana na kuvutiwa na style yao ya maisha,baada ya kuwa waziri wa mambo ya Nchi za Nje,lakini si vinginevyo.
Huyo mkuu ni mpenzi wa kinamama. Wanamuita "handsome" tabasamu lake endelevu linawamaliza wakinamama. Sasa kwa kuwa wengi wa wapiga kura ni wakina mama hayo ndiyo matokeo kwamba ameweza kupeta katika kipindi cha kwanza na hata cha pili ingawa ukweli ni kwamba utendaji wake katika kipindi cha kwanza tu ungeweza kumnyima kuendelea na kipindi cha pili lakini kwa kuwa wapiga kura wengi ni wakinadada na wao hawajui juu ya utendaji ingawa ndiyo wanaobeba mandoo ya maji mabarabarani kusaka maji, ndiyo wanaopika kwenye giza na balaa zingine zote bado wakati wa kura wanaangalia u-handsome na bahati mbaya hata kwa "population" ndiyo wengi kwa hiyo kama jamaa angekuwa na kipindi cha tatu bado angepita kwa sababu akitabasamu tu wakinadada wote taabani wanatoa kura bila kujijua. Inabidi somo la nguvu lipite kwa wanaume ili uchaguzi ujao wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura na pia wawaelimishe madada juu ya hatari ya kuvutiwa na tabasamu na u-handsome pasipo kuangalia uwezo wa mtu.
Nimesoma hizi Wikileak diplomatic cables na kuona JK anavyoingizwa sehemu mbalimbali na kujikuta ninajiuliza hilo swali. Sijui wengine mmeona pattern fulani au mmejiuliza swali au kupata majibu ya swali hilo?
Mkuu tukiangalia hapo kwenye RED , ina maana JK naye anamwandaa Ngeleja kushika uongozi maana alimpandisha haraka haraka hadi kuwa waziri kamili kwenye wizara nyeti ????
Afadhali umeuliza wewe maanake wengine tukisema itaonekana tuna wivu, Wajamaa na wasiopenda maendeleo.Nimesoma hizi Wikileak diplomatic cables na kuona JK anavyoingizwa sehemu mbalimbali na kujikuta ninajiuliza hilo swali. Sijui wengine mmeona pattern fulani au mmejiuliza swali au kupata majibu ya swali hilo?
Msamehe bure FaizaFoxi, hili swala huenda analitazama kiimani zaidi na inamfanya apuuze na kucheka, hukumbuki Kiongozi wa dini aliyesema Kikwete anaandamwa kwasababu ya dini yake tuu na si kwamba ni kiongozi mbovu?
Wamarekani walianza hii effort kwetu in fifties.... it will take us 100 years kureverse walichofanya
FYI, hata rais ajaye atatoka kwenye "pot" yao tu... tutake tusitake
MTM
kichwa kidogo!kichwa cha habari na habari ni vitu viwili tofauti, huu ni ule uandishi wa ya magazeti ya nanihii.
<br />Unapenda sana kuchekacheka FF sijui kwa nini? issue sensitive kama hii wewe unacheka,umezisoma hizo cables MM anazozisema?Inasikitisha sana dada'etu,kama haujazisoma tafuta muda uzisome(hata kama zinakukera), utafakari....Utaelewa kwa nini MM kaanzisha huu uzi
Ni Mkapa! Alikuwa na rais & mwenyekiti wa chama na angeweza kumpiga chini kama angeamua. Kwanza alimpa wizara rahisi (mambo ya nje kwa miaka 10). Angepewa wizara ngumu kwa muda wa kutosha udhaifu wake ungeonekana mapema