WHO: Nchi za dunia ziige Iran katika kutoa huduma za afya

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,869
WHO: Nchi za dunia ziige Iran katika kutoa huduma za afya


Shirika la Afya Duniani WHO limeziasa nchi nyingine duniani kuwa na mfumo mzuri wa tiba na huduma za afya kama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hayo yalisemwa jana Jumapili hapa Tehran na Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO ambaye amesisitiza kuwa, "Irada ya kisiasa ya Iran ya kutoa huduma nzuri za afya kwa wote inapaswa kuigwa na nchi nyinginezo duniani."

Mkurugenzi Mkuu wa WHO amesema hayo katika mazungumzo yake na Waziri wa Afya wa Iran, Said Namaki kabla ya kuanza Kikao cha 66 cha Kamati ya Kieneo ya Mashariki mwa Mediterranean (EMRO) ya shirika hilo la afya ulimwenguni.

Wakati huohuo, Waziri wa Afya wa Sudan ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.

Akram Oltum aliyasema hayo jana Jumapili katika mazungumzo yake na Waziri wa Afya wa Iran na kubainisha kuwa, "Iran imepiga hatua kubwa katika kutoa huduma bora za afya zenye viwango vya kimataifa kwa watu wake. Hili ni jambo la kupongezwa."

Kikao cha 66 cha Kamati ya Kieneo ya Mashariki mwa Mediterranean (EMRO) ya Shirika la Afya Duniani WHO kinafanyika hapa nchi Iran mwaka huu.

Chanzo: ParsToday
 
Maendeleo yao tutayapiga mabomu waanze upya Kama Iraq Ni swala la muda taifa la Mungu israel litafanya yake mark my words
 
Back
Top Bottom