WHO na kesi dhidi ya mila za Rwanda za kuongeza Kisimi

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
VITA YA ‘WHO’ DHIDI YA RWANDA NA TAMADUNI YAO YA KUKUZA VISIMI KWA WANAWAKE.

Nchini Rwanda na Burundi na baadhi ya nchi kama Zimbabwe, kuna mila ya wanawake au wasichana kuchua visimi (Labia minora) kwa mtindo wa kikuvuta mbele ili kiwe kirefu. Mila hii ni maarufu na kubwa sana nchi Rwanda ukilinganisha na hizo nchi nyingine, Wanawake nchini Rwanda hutumia mitishamba kukuza visimi vyao tangu wakiwa watoto. Mtoto wa kike mama yake humvuta kisimi kwa taratibu kila siku anapomuogesha, na mtoto akifika umri wa miaka 10, huhimizwa kuendelea kuvuta kisima chake kwa muda wa kati ya dakika 10 hadi 15 kila siku, kwa mujibu wa taarifa, kisimi hufika hadi inchi tano (5). Kwa miaka dahari watu wa Rwanda wamefanya utamaduni huu, na lengo lake ni kuchochea hamu ya kufanya tendo la ndoa kati ya mwanamke na mwanaume, hasa zaidi humsaida mwanamke kufika kileleni mapema kuliko kawaida.

Wasichana wenye visimi virefu kufika kileleni mapema zaidi na pia inasemekana wanaume wanaokutana na wanawake hawa wanafurahia sana tendo. Ila kwa mujibu wa wizara ya afya, kitendo cha kukuza kisimi zinaweza kuleta madhara kifya, wakidai kuwa wakati unavuta kisimi basi maumbile ya ndani ya huvimba na kubabisha kuzuia uume kuingia vizuri wakati wa tendo. Pia wanadai ya kuwa, kuna uhusiano mkubwa kati ya maambuzi ya magonjwa ya zinaa na tabia ya kuvuta kisimi... Japo hili bado liko kwenye utafiti.

Hii ni mila ya kiafrika, na kila Jamii ina mila zake katika kuhakikisha tendo la ndoa linakuwa mujarabu baina ya watu wawili (wanandoa mke na mume). Kimsingi, sio kila mila ni nzuri na inapaswa kutukuzwa, na hakuna Jamii duniani tamaduni zao zote zinavutia au ni nzuri. kwa mfano, Nchi Spain wana tamaduni ya kuchezea chakula, huvuna nyanya nyingi sana na kuziharibu kwa kupigana (Tomato Festival), ni watu wangapi duniani wana shida ya nyanya/chakula?

Au Nchini Marekani huvuna maboga mengi na na kuyachezea kwenye sikukuu yao yao ya kitamaduni iitwayo Halloween. Watu wangapi wanakufa njaa kila uchwao? Vivyo hivyo, hata sisi Afrika sio kila aina ya mila inapaswa kutukuzwa, nyingine zina madhara makubwa sana kwetu na kwa wengine. Lakini wakati tunakemea mila hizi, ni lazima tufanye kwa uadilifu na kwa uangalifu mkubwa sana kuondoa taharuki au uvunjifu wa amani, kwa sababu siku zote mila huwa si mbaya kwa mwenye mila yake..

Inaendelea
 
Wengine wanavivutaaaa, wengine wanavikataaa duu!
Mila nyingi zinafanywa bila kuangalia/kujua madhara ya hapo baadae. Imefika kipindi cha kufuata mila zenye manufaa. Kuhusu visimi viwe vinaachwa tu kama vilivyoumbwa, hakuna haja ya kuvuta wala kukata! Magovi yakatwe!
 
Nimekusoma vizuri.

Ikiendelea tutakua pamoja.

Mila ni Nzuri kiukweli lakin shida inakuja katika jamii tumeishakua mchanganyiko wapenda (wafata) mila na wasio taka kabisa.

Mfano mzuri, wanawake wanao keketa ukiwapeleka kizimbani wajitete kwa nin wanakeketa mabinti huwezi kumzidi hoja na umfunge hata siku moja, wana sababu zao
 
Back
Top Bottom