beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema idadi ya wagonjwa na vifo vitokanavyo na COVID-19 vimeendelea kupungua ulimwenguni katika wiki iliyopita.
WHO imesema leo kuwa zaidi ya visa milioni 3.6 na chini ya vifo 60,000 vimeripotiwa kati ya Septemba 13 na 19. Kupungua kwa kiasi kikubwa cha visa hivyo kumeripotiwa kwenye nchi za Mashariki mwa Mediterania na Kusini Mashariki mwa Asia.
WHO imesema idadi kubwa ya vifo vipya imeripotiwa Marekani, Urusi, Brazil na Mexico. Wakati huo huo, India imesema itaanza kutoa chanjo ya virusi vya corona kwa watoto wenye umri wa miaka 12 au zaidi kuanzia mwezi ujao.
Urusi kwa upande wake imetangaza kuwa takriban watu milioni 40 nchini humo wamepata chanjo kamili ya COVID-19.
Chanzo: DW Swahili