WHO lalalamika ukosefu wa ushirikiano kutoka Tanzania kuhusu uwezekano wa uwepo wa visa vya Ebola

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,587
9,665
(Mods tafadhari msiunganishe uzi huu na ule mwingine wa propaganda unaodai WHO wamesema hakuna ebola nchini)

Kwa mujibu wa BBC na taarifa rasmi ya WHO:
Shirika la afya duniani limelalamikia ukosefu wa ushirikiano kutoka serikali ya Tanzania katika utoaji taarifa kuhusu visa vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola nchini.

Katika taarifa yake ya malalamiko, shirika hilo limeeleza kwamba uwazi na kasi katika kukabiliana na virusi vya ugonjwa huo hatari ni muhimu katika kudhibiti mlipuko ambao tayari umetajwa kuwa janga la afya duniani.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa Jumamosi, WHO limeeleza kwamba kufuatia taarifa zisizokuwa rasmi kuhusu visa vya ugonjwa na jitihada zake kupata taarifa kutoka kwa idara husika Tanzania kuhusu hali nchini humo, mpaka sasa hawajapokea data za kliniki, matokeo ya uchunguzi, mawasiliano na watu husika na hata matokeo ya uchunguzi wa maabara waliofanyiwa wagonjwa hao wanaoshukiwa.

"Kufikia sasa jitihada zetu za kuifikia serikali ya Tanzania kutoa tamko kuhusu taarifa hii ya WHO hazijafuwa dafu"
WHO lilituma kundi la wataalamu kuchunguza kisa cha ugonjwa usiojulikana na ubalozi wa Marekani ulifuatilia hatua hiyo kwa kutoa tahadhari.
Hatua hiyo ilisababisha uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba ugonjwa huo hatari umeingia nchini Tanzania

Serikali ya Tanzania ilifutilia mbali uvumi kwamba kuna visa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Waziri wa afya nchini humo bi Ummy Mwalimu aliambia mkutano na wanahabari kwamba hakuna kisa hata kimoja cha ebola katika taifa hilo.

Alisema kwamba taifa hilo limejiandaa kukabiliana na mlipuko wowote wa ugonjwa na tayari limefanya majarabio ili kujua jinsi ilivyojiandaa huku ikiweka tayari vituo vya kuwatenga waathiriwa.

Shirika hilo la Umoja wa mataifa limeendelea kueleza katika taarifa yake kwamba lilifahamishwa mnamo Septemba 10 kuhusu kifo cha mgonjwa kilichotokea mjinia dar es salaam, na kuarifiwa kwa njia isiyo rasmi siku ya pili kwamba mgonjwa huyo alipatikana kuwa na Ebola baada ya kufanyiwa vipimo
Kadhalika WHO linaeleza kwamba liliarifiwa kuhusu visa vingine viwili vinavyoshukiwa kuwa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo. Mmoja kati yao, alikutikana kutokuwa na Ebola baada ya vipimo na hapakuwa na taarifa zozote kuhusu mgonjwa wa pili, imeeleza taarifa hiyo

''Nataka kuwahakikishia kwamba idara ya afya ilichukua sampuli na matokeo yake ni kwamba wawili hao hawakuwa na ugonjwa wa Ebola. Hakuna Ebola Tanzania na watu hawafai kuwa na wasiwasi'', alisema waziri wa afya Tanzania Ummy Mwalimu wiki iliyopita kuhusu uvumi wa visa hivyo.

Kufanya vipimo tena vya homa ya Ebola katika maabara inashauriwa sana ili kuthibitisha matokeo ya vipimo na hivyo kubaini aina ya virusi Ebola . WHO linasema kuwa limewapatia maafisa wa Tanzania ushauri huu.

Mgonjwa huyo ambaye inaarifiwa ni mwanamke alifariki tarehe 8 Septemba kwa mujibu wa WHO.
Tarehe 10 Septemba 2019, Shrika la Afya duniani WHO lilipokea ripoti ya taarifa ya kisa cha mambukizi ya Ebola mjini Dar es Salaam, Tanzania. Kisa hicho kinachoshukiwa kilimhusu mwanamke mwenye umri wa miaka 34 ambaye alikuwa akisomea nchini Uganda.

Aliwasili nchini Uganda akitokea nchini Tanzania tarehe 08 Agosti 2019.
Taarifa hiyo inasema kwa kuanzia tarehe 08 hadi 22 Agosti, alikuwa katika eneo la kati la Uganda, akiishi katika hosteli ya kibinafsi karibu na mji mkuu Kampala.

chanzo cha taarifa: WHO na BBC
soma zaidi hapa
 
Shirika la afya duniani WHO limeishtumu serikali ya Tanzania kwa kushindwa kutoa taarifa za wasiwasi wa kuwepo kwa maambukizi ya Ebola nchini humo, suala ambalo linarudisha nyuma vita dhidi ya ugonjwa huo.

WHO katika taarifa yake imesema ilipata taarifa kuwa, tarehe 10 mwezi Septemba kesi ya Ebola iliripotiwa katika jijini la Dar es salaam baada ya mgonjwa aliyekuwa anashukiwa kugundulika kuambukizwa.

Licha ya kuomba taarifa rasmi, WHO inasema haijapata majibu yoyote kutoka kwa serikali ya Tanzania kuhusu madai ya kuwepo kwa maambukizi hayo.

Hata hivyo, serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya afya siku kadhaa zilizopita, ilikanusha kuwepo kwa Ebola nchini humo lakini ikatoa tahadhari kwa raia wake kuwa makini.

Taarifa hii ya WHO imekuja, wakati huu mataifa ya Afrika Mashariki yakiwa katika hali ya tahadhari kutokana na maambukizi ya Ebola Mashariki mwa Jamhuri ya Kidmekrasia ya Congo, ambako watu 2,103 wamepoteza maisha kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Nchini Uganda, watu wanne waliripotiwa kuambukizwa wote waliokuwa wamevuka mpaka kutoka DRC lakini baadaye wakapoteza maisha.

 
Si jana Ndungulile alikuwa anatuambia kuwa wamepeleka sampuli na zimepimwa na akaja na majibu! Sasa hapa tuamini kipi?
 
Hao wanataka kutuharibia tu na homa lao la kutengeneza hili,,watuache kwanza tumalize miradi yetu mikubwa kisha waanze kutuua na kupiga pesa.Congo hawajatosheka,Uganda hakuna pesa,sasa target Tz,,,aah!!
 
Hao bebelu hao, wanataka kutukwamisha, ndege zetu zisipate watalii. Ccm yaani Bora raia wateseke ila wawekezaji washawishike?
 
WHO njooni muonyeshe hao wagonjwa wako wapi. Terrible namna mnavyofanya mambo. Nakosa kabisa imani na hawa jamaa. Mnataka kusambaza Ebola?
 
Ni kweli lazima sote tusikilize na kuamini kauli za mamlaka husika katika masuala kama hili la ugonjwa hatari wa Ebola.

Lakini kwakuwa tabia ya "mendacity" imeota mizizi katika siasa zetu hasa miongoni mwa wenye nguvu; dalili zinaonyesha hili jambo nalo linashughulikiwa kisiasa!

Tukiendelea hivi dunia itatushangaa kwa kucheza na roho za watu kwa mambo ya kisiasa.

Tusijifanye mbuni katika hili. Wala tusitafute mbuzi wa kafara miongoni mwetu.
 
Ebola sio kitu cha kufichwa, hufagia hata wauguzi na madaktari, acheni uzushi, ni wazi kuna kitu kinasukwa na mabeberu, wamekosa pakuingilia.
 
Sina utaalam wa tiba ni vizuri kwa hili tusisalitiane na tusiingize neno la kejeli kwa maslahi mapana ya taifa letu changa la Tanzania.
 
Shirika la afya duniani limelalamikia ukosefu wa ushirikiano kutoka serikali ya Tanzania katika utoaji taarifa kuhusu visa vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola nchini.

Katika taarifa yake ya malalamiko, shiriki hilo limeeleza kwamba uwazi na kasi katika kukabiliana na virusi vya ugonjwa huo hatari ni muhimu katika kudhibiti mlipuko ambao tayari umetajwa kuwa janga la afya duniani.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa Jumamosi, WHO limeeleza kwamba kufuatia taarifa zisizokuwa rasmi kuhusu visa vya ugonjwa na jitihada zake kupata taarifa kutoka kwa idara husika Tanzania kuhusu hali nchini humo, mpaka sasa hawajapokea data za kliniki, matokeo ya uchunguzi, mawasiliano na watu husika na hata matokeo ya uchunguzi wa maabara waliofanyiwa wagonjwa hao wanaoshukiwa.

Kufikia sasa jitihada zetu za kuifikia serikali ya Tanzania kutoa tamko kuhusu taarifa hii ya WHO hazijafuwa dafu.

=================================================

The World Health Organization accused Tanzanian authorities of withholding information about suspected Ebola cases in the country this month, potentially hampering the containment of the deadly virus.

The U.N. agency’s statement Saturday was its most pointed rebuke toward any government yet during the outbreak that has ravaged nearby eastern Congo for more than a year, killing more than 2,000 people.

The WHO was made aware of the suspected cases in Tanzania shortly after one appeared this month in Dar es Salaam, the East African country’s massive capital. After that, the international organization was shut out of blood sample testing and told by the government that Ebola had been ruled out, it said.

Tanzanian authorities have not offered alternative diagnoses.
“The limited available official information from Tanzanian authorities represents a challenge,” the WHO said. “Clinical data, results of the investigations, possible contacts and potential laboratory tests performed have not been communicated to WHO.”
 
Bado tu wanatubembeleza tukubali kwamba tuna huo ugonjwa nchini tanzania./ mbona walishachukuwa sampuli na kuona haokuwa ebola
 
Bado tu wanatubembeleza tukubali kwamba tuna huo ugonjwa nchini tanzania./ mbona walishachukuwa sampuli na kuona haokuwa ebola
Wewe nae, hiii taarifa inakizana na uhalisia maaana who wenyewe walishakuja wakachukua sampuli wakapima wenyewe wakatoa tamko kuwa Hakuna Ebola sasa hiii inakujaje au ni who nyingne?
 
Tuombeane mungu jaman.mimi binafsi huyo dr calister alikufa 8tarehe ni ndugu yetu.msishabikie jaman tunavyopanda daladala wengi hivi ni noma
Ni kweli lazima sote tusikilize na kuamini kauli za mamlaka husika katika masuala kama hili la ugonjwa hatari wa Ebola.

Lakini kwakuwa tabia ya "mendacity" imeota mizizi katika siasa zetu hasa miongoni mwa wenye nguvu; dalili zinaonyesha hili jambo nalo linashughulikiwa kisiasa!

Tukiendelea hivi dunia itatushangaa kwa kucheza na roho za watu kwa mambo ya kisiasa.

Tusijifanye mbuni katika hili. Wala tusitafute mbuzi wa kafara miongoni mwetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom