#COVID19 WHO: Kirusi cha Omicron ni hatari, chanjo ni muhimu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeonya kuwa aina mpya ya kirusi cha corona Omicron c ina hatari kubwa ya maambukizo kuongezeka kote ulimwenguni.

Aina hiyo inaweza kusababisha athari mbaya katika baadhi ya maeneo ya dunia , WHO ilisema Jumatatu.

Mkuu wa shirika hilo, Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus, alitoa wito upya wa kushinikiza jamii ya kimataifa kutoa chanjo kwa mataifa maskini.

Covid-19 "hajamalizana nasi" bado, alionya.

Aina hiyo ya kirusi iligunduliwa nchini Afrika Kusini mapema mwezi huu huku ushahidi wa awali ukionyesha kuwa ina hatari kubwa ya maambukizo. Afrika Kusini imesifiwa kwa kuripoti kwa haraka kirusi hicho.

"Omicron ina idadi isiyokuwa ya kawaida ya mabadiliko ambayo mengine yanaweza kuwa athari kubwa katika mwelekeo mwingine wa janga," WHO ilisema.

Akizungumza Jumatatu, Dk Tedros alisema wanasayansi kote ulimwenguni wanafanya kazi ili kugundua ikiwa aina hiyo mpya inahusishwa na maambukizi ya juu, hatari ya kuambukizwa tena na jinsi inavyoitikia chanjo.

"Dharura ya Omicron ni ukumbusho mwingine kwamba ingawa wengi wetu tunafikiria kuwa tumemaliza Covid-19, janga hilo halijamalizana na sisi," alisema.

Aliongeza kuwa hakuna vifo ambavyo vimehusishwa na aina hiyo mpya ya kirusi cha Covid.

Visa tayari vimeripotiwa katika nchi kadhaa zikiwemo Canada, Uingereza, Ureno, Ubelgiji na Uholanzi.

Omicron imesababisha Uingereza, EU na Marekani kutoa marufuku ya kusafiri kwa nchi za Kusini mwa Afrika - uamuzi ulioshutumiwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Japan imetangaza kufunga mipaka yake kwa wageni wapya kutoka usiku wa Jumanne, wakati Australia imesitisha mpango wake uliosubiriwa kwa muda mrefu wa kupunguza vizuizi vya mipaka.

Kusafiri hadi Australia kwa wanafunzi wa kimataifa na "wafanyakazi wenye ujuzi" wanaoshikilia visa kulikusudiwa kuanza tena Jumatano lakini sasa kumeahirishwa hadi 15 Desemba.

Israel pia imepiga marufuku wageni kuingia nchini humo.

th

Huko Uingereza, chanjo za ziada za Covid zinatarajiwa kutolewa kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 18 ili kusaidia kusimamisha wimbi jipya linaloendeshwa na Omicron.

Marekani pia imefuata mkondo huku rais Joe Biden akiwaambia Wamarekani "nendeni mkachukue nyongeza ya chanjo ". Pia aliwataka watu kuvaa barakoa ndani ya nyumba.

Lakini Bw Biden pia alisema hatarajii vizuizi vyovyote vya kusafiri vya Amerika au marufuku ya kutoka nje wakati huu.

Kumekuwa na visa zaidi ya milioni 261 na vifo milioni tano kote ulimwenguni tangu janga hilo lilipoanza mnamo 2020, kulingana na data kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins
 
Kama kirusi kimejibadili na jina, kuchanjwa ni kujichosha tu, chanjo siyo ya Omnicron.

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Baandika ugari mboga inakuja Sasa hivi🤔.
Beberu anatuchanganya tutishike, South African variant anaita DEADLY, ikaja Indian variant, tuliokuwa tunakunywa juisi za pilipili kichaa tukaacha, maana kama wahindi wanaokula pilipili kama pipi wanakufa ikawa dhahiri pilipili siyo dawa, ikaja Delta, sasa Omnicron, zote DEADLY tena ukisikiliza BBC unaweza kuamua kuacha kuvuta pumzi kabisa.

BBC wakielezea coron unaweza tamani usitoke nje
 
Ahsante Kwa taarifa...

Na sisi tugundueni kirusi chetu...
Alafu tunakiita kidimbwi...
Tunakipigia promo tunaunza chanjo zetu...
 
Uingereza wakiacha kujazana uwanjani kama wanavofanya sasa, ntaamini hiyo omnicrom!..kwa sasa acha tuendelee kula hewa ya mungu for free
 
Beberu anatuchanganya tutishike, South African variant anaita DEADLY, ikaja Indian variant, tuliokuwa tunakunywa juisi za pilipili kichaa tukaacha, maana kama wahindi wanaokula pilipili kama pipi wanakufa ikawa dhahiri pilipili siyo dawa, ikaja Delta, sasa Omnicron, zote DEADLY tena ukisikiliza BBC unaweza kuamua kuacha kuvuta pumzi kabisa.

Everyday is Saturday................................:cool:
Mkuu,kula zako tizi ukipata muda,kula balanced diet,pumzika vizuri...Then kula maisha to the fullest,usiwaskilize hawa ma beberu na story zao za covid Variant,mimi nilishaacha kuwaskiliza,wanapanikisha tu watu..
 
Back
Top Bottom