Who is this Shitambala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Who is this Shitambala?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gottee, Nov 2, 2010.

 1. Gottee

  Gottee Senior Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wana JF,

  Taarifa nilizonazo ni kuwa CCM imetwaa Majimbo mawili ambayo CHADEMA ilikuwa ikitegemea kuyatwaa. La kwanza ni lile la Mbeya Vijijini ambalo lilikuwa linagombwa na Shitambala (CHADEMA) na Mchungaji Mwanjali (CCM) Mchungaji Mwanjali amefanikiwa kutetea kiti chake. Lingine ni lile lililokuwa likigombwa na Siame, inasemekana nalo CCM (Siame) wametwaa.

  Kinachowashangaza wengi hapa ni ujio wa Kingunge Ngombale Mwiru wa ghafla hapa Mbeya. Habari zingine zinasemwa Shitambala ameuza Jimbo hilo kama alivyofanya kwenye ule uchaguzi mdogo. Habari zinaendelea kusema 'Wazito' wa CCM pia walikutanishwa na Mr Sugu na kuahidi kumfungia donge nono, Mr Sugu aidha kwa kusoma alama za nyakati au kwa uzalendo wake aliwatolea nje. Jana tumeshuhudia Mabomu ya Machozi zaidi ya 50 yakivurumishwa na mengine yameendelea kusikika hata leo asubuhi.

  Ninachojiuliza kuna haja ya kusema Kikwete atapoteza Urais wake au ni kutaka kujua Asilimia atakazoshinda? 45 au 60 au 80 au 100 kabisa?

  Yale niliyokuwa nayafikiria ndiyo haya. Watanzania tujiandae kukaa bila Utawala kwa miaka mingine mitano.

  Nyerere uko wapi? Machozi ya samaki yamekwenda na maji!
   
 2. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Very sad....
   
 3. v

  valour Senior Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mambo ya kusingizia watu wanauza majimbo wanaposhindwa bila ushahidi wa kutosha ni kitu kibaya sana. Mtu mmoja alikuwa humu na kusema Lema kauza jimbo angeshindwa ingekuwaje. Hebu tuwe na subira na kuchangia positive threads sio lazima tuandike kama hatuna cha kuandika kuna threads nyingi humu ndani za kuchangia.
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!inasikitisha sana!!
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Namjua sana Sambwee Shitambla, maana nimekua nae toka utotoni!...Ni kijana jasiri sana kwa kauli, japo kiroho ni siri yake!...Sambwee amekuwa kama alivyo Mnyika pale Ubungo!...

  Kwa walioona mdahalo wake wa TBC, watakiri kuwa yule dogo anapendwa mno na wanaMbeya!...

  Lakini amekuwa mzalendo sana na mtu anayeheshimika sana na watu wa kabila la kwao Usafwani, hasa inaposemekana kuwa wakati fulani kwa nafasi yake ya uwakili alimtetea kiongozi mmoja wa kijadi ambaye ilikuwa afungwe jela , pale alipoingilia kati na kueleza kuwa ni makosa makubwa kumweka ndani kiongozi wa kijadi, maana unaweza kusababisha unrest katika jamii na kusababisha vita za Koo!

  Napata kigugumizi sana kuamini kuwa Shitambala anaweza kuisaliti jamii yake inayomheshimu kiasi kile kwa kupokea hongo za senti!

  Lakini anyway, siusemei moyo wake, he knows himself better!
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu PJ mimi namuamini sana Shitambala na Kwa kweli Amemsaidia sana Sugu kuchukua Jimbo la Mbeya hasa katika maeneo ya Wasafwa Ambako ndiko ilikokuwa Ngome ya Mpesya

  Kama Shitambala atashindwa ni kutokana na Mahudhurio madogo kwa Wapiga kura hasa wa Maeneo ya mijini ( namaanisha maeneokaribu na Mbalizi). Waliompa kura nyingi Mwanjala ni wale wa Vijiji vya Ndani kabisa ambako maisha ni duni na wao wanaona kuinyima Kura CCM ni kama Kuisaliti yaani wao na CCM hata kama wanaishi katika Nyumba za Mbavu ya Mbwa!
   
 7. Gottee

  Gottee Senior Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Valour,

  Hapa sio kumsngizia mtu. Hapa ni kujaribu kutafakari hali ya mambo inavyokwenda. Binafsi Shitambala hatufahamiani kabisa zaidi ya kupishana njiani. Mimi nilianza kumtilia shaka wakati ule wa Uchaguzi Mdogo. Akiwa mwanasheria anayeheshimika hapa Mbeya na labda hata nje ya Mbeya alishindwa kufuata maelekezo ya Tume ya Uchaguzi na kuikosesha CHADEMA kushiriki kwenye ule uchaguzi mdogo. Nimekutana na kundi la watu waliopigwa mabomu jana ambao hawa hawa walikesha kwenye vituo vya kupigia kura hapa Mbeya Mjini na Vijijini. Kimsingi Mbeya Mjini ilikuwa ngumu kuliko hata hiyo Vijijini.

  Kinachozua maswali ni hiki. Kwa nini matokeo ya Majimbo haya ambayo CHADEMA walikuwa na nguvu kubwa yalicheleweshwa? Huu ujio wa kina Kingunge hapa Mbeya una nia nzuri? Na lingine ni kuwa huenda wale waliokataa 'hela chafu' za CCM ndio hao wamevujisha siri. Ukweli ni kwamba kuna watu wanamsaka Shitambala huko aliko.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Duuu!
  Hivi hela za kuwauza nduguzo zinakuwa na utamu gani?....
  Kuna raha gani kuuza utu wa blood-brothers na blood sisters, na in exchange kupokea senti?
  I dont get it properly!
   
 9. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu usikurupuke na kuharibu image ya mtu bila kuwa na uhakika.

  Matokeo ya uchaguzi wa Mbeya Vijijini bado hayajatangazwa na so far ni 50-50; kuna fujo kubwa saizi zinaendelea mitaa ya Mbalizi, wafuasi wa Chadema wakidai wapewe ushindi wao kwa kuhakikiwa kwa matokeo ya kijiji kimoja ambacho kina wapiga kura 100 tu lakini mgombea wa CCM amepata kura 800 katika kijiji hicho.

  It's too close, tusubiri!!
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kuiba bila mahesabu!
  This is hopelessness, jamani hawa wanaccm ni threat kuwa nao mitaani!..
  Nimeambiwa pia kuwa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya wakati wa kampeni na siku nzima ya uchaguzi walikuwa wanamsaidia Mwanjali bila hata ya aibu wala woga!, how comes mwanaume mzima anamwogopa JK? kiasi hicho ...?..Bila yeye hutaishi?
  All in all, wanadhaalilika very soon hawa akina Mwakipesile!
   
Loading...