Who is Nimrod Mkono?

kaka mtu

Member
Nov 15, 2010
17
0
Wadau nisaidieni, huyu mtu (NM) amekuwa akihusishwa na tuhuma nyingi hasa zile za kimataifa kwa kutumia taaluma yake ya sheria.
 

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,198
2,000
So what do you want to know here!!

1. Who is he? or
2. Why is he connected with scandals?

Be specific then u will be assisted

Cheers
 

kaka mtu

Member
Nov 15, 2010
17
0
So what do you want to know here!!

1. Who is he? or
2. Why is he connected with scandals?

Be specific then u will be assisted

Cheers

Nilisikia kwamba aliwahi kufukuzwa nchini na baba wa taifa JKN miaka ya tisini, na JKN alipofariki dunia ndipo akarudi nchini. Pia juzi kwenye SAGA la DOWANS nimesikia amehusika ktk kesi ya DOWANS kwa kuipeleka kesi hiyo ICC. Nisaidieni wadau huyu m2 binafsi simfaham.
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,522
2,000
Hapana. Hajawahi kufukuzwa nchini. Kuna rumours kuwa baba wa taifa alitaka kumweka kizuizini kwa ufisadi. Akatonywa na watu waliouwa karibu na Mwalimu na akajificha.
 

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,198
2,000
Ni Mbunge wa Musoma vijijini na advocate. He runs a very successfull advocacy firm.
Infact ni tajiri mkubwa ila pesa zake kapata kwa mbinu mbinu hivi through BOT etc.

By the way wapiga kura wake wana mpenda sana kwani amewapelekea maendeleo katika huduma za jamii kama shule, maji na hospitali. That's all I know about him mwenye la zaidi atakusaidia.
 

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,225
Anamiliki Tubenki mmoja tuitwao Bank M. Ana lawfirm yake mmoja inafanya kazi PPF tower inashughulika na dili kubwa kubwa tu. Moja wapo ya dili ni la BOT ambapo jamaa alikuwa akilipwa $5,000 kwa kila saa anayoitumia kushughulikia hiyo kesi. Aliwahi kupakia Range Rovers kadhaa ndani BA kutoka kwa bibi akaziimport kwa ndege mpaka Dar. Wengine wataendelea utaona jinsi jamaa alivyo na vijisenti tu vidogo vidogo hapa mujini Dar-es-salaam.
 

RAJ PATEL JR

JF-Expert Member
Sep 8, 2010
743
0
We are in for another 5!!
Nimrod is a good buddy and corrupt-free. If you have anything against him you either go see TAkukuru or Die!!
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,521
2,000
akiingia supermarket seacliff kuacha 1m kwa shopping ya vijuice toilet paper etc ni kawaida kwake!wahindi hubeba mifuko yake mpaka kwenye gari
 

mkibunga

Senior Member
Nov 17, 2010
196
0
jimboni kwake hatumpendi ila anatumia visenti vyake kuwahonga walalahoi kupita bila kupingwa kama alivyofanya mwaka huu kuhusu maendeleo anawadanganya watu anawasaidia kijijini kwake amekarabati shule mbili akaita waandishi njaa wakapiga picha wakazirusha na kujifanya kuwa shule za jimbo lake zote ziko vile no ebu nenda kata nyingine za jimbo lake hakufai kuna shule inaitwa Buko wanafunzi hawajasoma masomo ya sayansi maths,biol,chem,phys miaka mitatu sasa hakuna hata mwl wa dawa wa masomo hayo hayo ndo maendeleo au amepaka rangi tu majengo
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
Hivi uliulizia juu ya Ndugu Nimrod Mkono?

Huyu baba nadhani namfahamu kiasi fulani hivi. Ni baba moja mweusi sanaa, mwembamba, mrefu wa wastani tu. Ni miongoni mwa Wa-Tanzania wachache wanaotumia gari la kifahari aina ya Range Rover (Vogue) yenye rangi za kijani kibichi na uesi wa kutafutiza tu kwa ajili ya kuendelezea shughuli zake za KILIMO KWANZA kwenye mashamba yake makubwa sana sehemu nyingi tu nchini iliwa ni pamoja na kule Ujerumani (yaani Lushoto).

Kitaaluma, huyu baba ni fundi mchundo ma maswala ya sheria. Kwa wale wanaomfahamu wanadai anaweza kufanya mazingaombwe kwenye karatasi akipewa na ndowano atakazozitia katika mikataba yoyote atakayosuka, maumivu yake huanza kwa wananchi baadaye sana kama miaka mitano hivi na kuendelea lakini matunda yake hayachelewi sana kwa wanaoomba msaada wake. Wala mtu usijisumbue kumtishia uwaziri huyu baba maana hawezi kukubali hata siku moja hizo kazi. Yeye mwambie kwamba mkataba tata wa kimataifa uundwe kwa ufundi mkubwa ndani ya muda mfupi tu na hata usiku wa maanane utasikia watu tayari washamwaga wino na dili KUCHUKUA MIMBA hapo hapo. Wengine huongezea kwamba huyu baba hulipwa Dola za kimarekani 1,500 kwa saa. Hii ina maana kwamba huyu baba akikupa muda wake wa walau masaa 3 tu ni sawa na kusema utamlipa hizi hela zetu za kudunduliza (Tsh 6,750,000/-) mara idadi ya watu wanaomtembelea kutwa ofisini kwake.

Sasa kwa mantiki hiyo ujiulize ni akina nani humtembelea na kwa matarajio gani pindi wanafunga mlango wake kwa nje??? Muuliza swali JF, kidogo huyu ndiye Nimrod Mkono Mbunge (Back-Bencher) ambaye ni zaidi ya Waziri na mwenye 'Ukarimu' wa kujengea kijiji kizima shule zaidi ya Tanganyika International School na kuwakabidhi funguo zote bila kuomba hata ka-mfuko wa simenti toka kwa wanakijiji wenzake.
 

Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
533
225
Huyu jamaa kwa upande mwingine wa shilingi ametajirika sana wakati ule ambao mzee wa vijisent alikua mwanasheria mkuu wa serikali.
Hapo ndipo alipopata tender nyingi za kushughulikia kesi za serikali ikiwemo ile ya city water katika anga za kimataifa. Baada ya hapo alikua akiidai serikali hela nyingi sana kwa muda mrefu ambayo kutokana na kucheleweshewa malipo yake aliamua kutumia taaluma yake ya sheria akisaidiana na mtajwa hapo juu na kuweka madeni yake au ku convert madeni yake katika tressury bills ili yasishuke thamani kwa hiyo madeni yake yanazidi kukua kila siku kulingana na faida anayoipata kwenye tressury bills ambayo kwa sasa nadhani yatakua yashapita hata garama za kulipa DOWANS mara 10.
HUYU JAMAA KUJENGA PRIMARY AU SEKONDARY MOJA JIMBONI KWAKE SIYO ISSUE KWAKE.....NI SAWA NA WEWE KUMTOA GIRL FRIEND WAKO OUT.
 

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,578
0
Nilisikia kwamba aliwahi kufukuzwa nchini na baba wa taifa JKN miaka ya tisini, na JKN alipofariki dunia ndipo akarudi nchini. Pia juzi kwenye SAGA la DOWANS nimesikia amehusika ktk kesi ya DOWANS kwa kuipeleka kesi hiyo ICC. Nisaidieni wadau huyu m2 binafsi simfaham.

Nafikiri utakuwa ni uwongo maana JKN aling'atuka 1985, sasa sidhani kama miaka ya tisini alikuwa na uwezo wa kumfukuza mtu. Fanya homework tena.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
Nimroda Mkono ana mkono katika mengi sana yanayotuliza bila kituo ndani ya nchi hii.

Laiti ufalme wa mbingu ungekua unanunulika ndugu Mkono angediriki kufanya mazingaombe zake hata pale pale getini kuelekea paradiso. Nadhani cha msingi kwake huenda ikawa ni pesa zaidi, professional ethics na uzalendo baadaye.

Lakini bado ni rafiki wa mahakama, kipenzi cha HAKI na msomi wa hali ya juu vile vile japo kwa kodi ya wakulima.
 

Jituoriginal

JF-Expert Member
Feb 8, 2010
363
225
Mkono Nimrod,ni mtu ambaye akikutana na akina matonya barabarani pesa za kuwapa hana muda wa kuhesabu anaingiza mkono kwenye kapu bila kutazama itoke milioni ,malaki hajali,pia ndugu zetu maaskari wa usalama barabarani wakiona VOGUE yake hupagawa ukimpigia saluti siku yako njema,na wewe kama akina matonya anakuchotea manoti.
 

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,885
2,000
Yupo kwenye orodha ya mafisadi iliyosomwa na dk Slaa mwembeyanga,2007.Ni mwizi wa mali ya uma.Ni mmoja kati ya watu wanaosababisha tuendelee kuwa maskini wa kutupwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom