Who is MZUNGU?

Mtu mweupe wa ngozi tena wa bara la ulaya. Kwa hiyo sifa hizo 2 ni za lazima.
 
Naomba kusaidiwa hili;
MZUNGU NI NANI?
Neno Mzungu (Mizungu) , lilikuwa likitumika kwa kumaanisha watu wa ajabu au waovu, Mizuka au mashetani...! Walipokuja watu kutoka uropa (Europe), walikuja na vitu ambavyo Waafrika walikuwa hawavijui, hususani Bunduki na baruti....! Na Matendo mengi ambayo Waafrika awakupendezwa nayo, ikapelekea watu hawa Weupe kutoka uropa kupewa jina ili la Mzungu... Wakimaanisha watu wa ajabu au Mizuka. Lakini baada ya kuzoeleka, linaonekana kama jina la kawaida, wakimaanisha watu Weupe kutoka Europe!
 
Mtu mweupe wa ngozi tena wa bara la ulaya. Kwa hiyo sifa hizo 2 ni za lazima.

kwa hiyo mmarekani au kaburu wa south africa si mzungu.au tuseme mtu kama jing sung park(wa man U) naye ni mzungu?
 
Neno Mzungu (Mizungu) , lilikuwa likitumika kwa kumaanisha watu wa ajabu au waovu, Mizuka au mashetani...! Walipokuja watu kutoka uropa (Europe), walikuja na vitu ambavyo Waafrika walikuwa hawavijui, hususani Bunduki na baruti....! Na Matendo mengi ambayo Waafrika awakupendezwa nayo, ikapelekea watu hawa Weupe kutoka uropa kupewa jina ili la Mzungu... Wakimaanisha watu wa ajabu au Mizuka. Lakini baada ya kuzoeleka, linaonekana kama jina la kawaida, wakimaanisha watu Weupe kutoka Europe!

kama sikosei historia inaonyesha watu kutoka asia "waarabu" nao walikuja kiajabuajabu na walikuja na mambo yao ya ajabu,mbona wao hawakuitwa wazungu?
 
kwa hiyo mmarekani au kaburu wa south africa si mzungu.au tuseme mtu kama jing sung park(wa man U) naye ni mzungu?
Hawa si wazungu japo kimazoea watu wanaita pia wazungu kwa vile ni weupe. Lakini kiuhalisia hao si wazungu. Wanaitwa kwa majina ya utaifa wao tu, mf. wamarekani, wakanada, wajapani, wakorea, nk.
 
Hawa si wazungu japo kimazoea watu wanaita pia wazungu kwa vile ni weupe. Lakini kiuhalisia hao si wazungu. Wanaitwa kwa majina ya utaifa wao tu, mf. wamarekani, wakanada, wajapani, wakorea, nk.

unasemaje kuhusu waingereza,wajerumani, wareno n.k hawana haki ya kuitwa wazungu?
 
unasemaje kuhusu waingereza,wajerumani, wareno n.k hawana haki ya kuitwa wazungu?
Hao ndo wazungu sasa!! Si ndo watu wa uropa (ulaya). Kumbe mbali na majina yao ya utaifa wana jina common ambalo ni uzungu.
 
Ukitaka kumchambua mzungu ni nani kuna mambo mengi ndani yake ikiwa ni pamoja na nasaba yake, lugha, mila na dasturi. Kwa nasaba mzungu ni mtu mwenye nasaba ya kuzaliwa na wenyeji wa asili wa ulaya ambao aghalabu wanatambulikwa kwa rangi ya ngozi zao, nywele na macho. Wamarekani weusi si wazungu kwani wana nasaba ya afrika. Makaburu ni wazungu kwa sababu wao nasaba yao ni ulaya. Mmakonde anayeiga mila na dasturi za kizungu hawezi kuwa mzungu atabaki mmakonde.
 
Hao ndo wazungu sasa!! Si ndo watu wa uropa (ulaya). Kumbe mbali na majina yao ya utaifa wana jina common ambalo ni uzungu.

kuwa wazi babu, kama uzungu ni kuwa mtu wa bara uropa au kuwa mweupe bila kujali unakotoka.hivi kwa nini the so called 'mwarabu' aliyezaliwa bara uropa haitwi mzungu?
 
Kuhusu asili ya neno mimi nimesikia yafuatayo (lakini siwezi kuyathebitisha):
Wazungu wa Kwanza Afrika ya Mashariki walikuwa Wareno lakini hawakuitwa "wazungu".
Neno hili limetokana na hao wapelelezi wa Afrika na tabia yao ya kuzunguka kote bila kukaa mahali pamoja. Yaani watu hao kama Livingstone, Burton, Speke na wengine.
Labda pia wa sababu kutokana na kuzunguka kwao walionekana kama watu wenye hali ya kizunguzungu?
 
kuwa wazi babu, kama uzungu ni kuwa mtu wa bara uropa au kuwa mweupe bila kujali unakotoka.hivi kwa nini the so called 'mwarabu' aliyezaliwa bara uropa haitwi mzungu?
Mwarabu ni mweupe? Mzee mwarabu si mweupe kama unavyofikiri. Mwarabu wazungu (weupe wa uropa) wanamwita coloured, yaani mtu mwenye rangi. Siyo mweupe huyo. Kwetu sisi weusi ndo tunamwona mwarabu ni mweupe, lakini wazungu hawamwoni mweupe (white), bali wanamweka kati ya watu weusi au tuseme coloured.
 
Kuhusu asili ya neno mimi nimesikia yafuatayo (lakini siwezi kuyathebitisha):
Wazungu wa Kwanza Afrika ya Mashariki walikuwa Wareno lakini hawakuitwa "wazungu".
Neno hili limetokana na hao wapelelezi wa Afrika na tabia yao ya kuzunguka kote bila kukaa mahali pamoja. Yaani watu hao kama Livingstone, Burton, Speke na wengine.
Labda pia wa sababu kutokana na kuzunguka kwao walionekana kama watu wenye hali ya kizunguzungu?

nashukuru,kwa maana hii tunaweza kusema 'mzungu ni mtu mweupe kutoka bara uropa mwenye tabia ya kuzunguka' hapa najaribu kuwaondoa wale watu weupe ambao hawajawahi kutoka nje ya bara uropa.au tuseme wazungu ni wale walioitwa Explorers tu,kwa kusema hivyo dunia ya leo haina wazungu.
 
Mtu mweupe wa ngozi...
Hebu tujiulize kidogo. Hivi kuna watu wenye rangi nyeupe? Manaake kwa uzoefu wangu wa uchoraji rangi nyeupe ni kama maziwa, sukari au chokaa. Sasa hawa tunaowaita weupe niaje? Ngozi ya mzungu siyo nyeupe bana. Wamejipa nasi tunakubali, na mbaya zaidi wengi wetu tunaitukuza kutokana na kasumba nzito!

Nachangia tu. Msinizabe kibao!
 
Jamii zetu nyingi za Kiafrika zina maneno yenye mzizi 'zungu' yanayotumika kumwongelea Mzungu. Ila huko kwa Waakan wa Ghana neno linalotumika ni Oburoni. Kuna cha kujifunza hapo kujua kwa nini Waafrika waliamua kutumia majina hayo kuwabainisha watu wa aina hiyo.
 
Hao waliyowaita wazungu wazungu walishakuwa na mawasiliano na waarabu kwa karne nyingi sana kabla ya kuja wazungu, kubuka waarabu au watu wenye rangi za kiarabu, hapa Afrika huwezi kusema ni wageni au walikuja, kwani wengi wao wako katika hili kontinenti linaloitwa Africa kuliko huko tunakokuita uArabuni, nadhani hata neno Africa linatokana kwenye lugha ya kiarabu seuse Dar es Slaam na hata neno Tanganyika ambalo hata Nyerere alishawahi kusema "hajui" limetokea wapi nalo pia lina asili ya kiarabu.

Huko tunakokuita uarabuni na hii Afrika yetu kulikuwa hakuna mpaka wa kutenganisha watu wasifike, utenganisho uliletwa na wazungu baada ya kuchimba mfereji wa kanali.

Kwa hayo, waarabu si wazungu na wa Afrika hawakuwa na sababu ya kuwaona ni mizuka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom