Who is Mary Chitanda in Arusha Politics?

Kingo

JF-Expert Member
May 12, 2009
855
390
Wanajamvi, ningependa mwenye kufahamu anijuze hapa Mary Chitanda ni nani katika siasa za Arusha, CCM na Tanzania kwa ujumla.
 
Just some crooked-ribbed, riggid-necked funny blond, playing with a coin around the pit-latrine!
Hawajui vizuri wana-Apollo huyu mama!
Kuna mwingine anaitwa Thobias Andengenye...soon and very soon watapewa advertise na kukaribishwa Arusha.
 
Na Mwandishi wetu - Imechapwa 04 March 2009

makamba_5.jpg




Kazi ya Kamati ya Bunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushughulikia malalamiko na matamshi ya mbunge wa Mvomelo, mkoani Morogoro, Suleman Sadiq, sasa imekuwa ndogo.
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM, 10 Februari 2009, mjini Dodoma, Sadig alimtuhumu Mwekahazina wa chama hicho, Amos Makala akisema "anatumia vibaya fedha za chama."
Hata hivyo, wiki moja baada ya Sadiq kumtuhumu Makala, ameibuka tena na kukana kwamba hajawahi kutoa tuhuma hizo, jambo ambalo limezidi kumuingiza katika matatizo na chama chake.
Taarifa za ndani ya CCM zinasema uamuzi wa Sadiq kukana kauli yake aliyoitoa Dodoma umetokana na maelekezo ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba.
"Ndiyo ukiangalia utetezi wa Sadiq mara moja utabaini kwamba kuna mkono wa Makamba katika jambo hili," alisema kiongozi mmoja wa CCM.
Aliongeza, " Awali Sadiq aliwasilisha malalamiko yake, lakini baada ya Makala kumuandikia Makamba, ndipo Sadiq akajitokeza na kubadilisha kile alichokidai awali," alisema kiongozi mmoja wa CCM kwa sharti la kutotajwa jina.
Katika barua yake ya 14 Februari 2009 aliyoituma kwa Makamba, Sadiq amekana kwamba ametoa tuhuma hizo dhidi ya Makala.
Hata hivyo, MwanaHALISI linaushahidi kwamba Sadiq alimlalamikia Makala, na kwamba Makala tayari amechukua hatua ya kujibu tuhuma za Sadiq.
Inaelezwa kwamba katika mkutano huo Sadig alimtuhumu Makala kuwa amemgawa na wananchi wa jimbo lake, na kwamba tayari anafanya kampeni za kutaka kugombea ubunge wa jimbo hilo.
Aidha, Sadiq alimtuhumu Makala kuwa anatumia vibaya wazifa wake wa muweka Hazina kwa kusema ametumwa na CCM kugombea ubunge wa jimbo hilo na tayari ametoa misaada ya zaidi ya Sh. 180 milioni.
Tuhuma nyingine ni Makala kuanzisha kombe la mpira wa miguu linaloutwa Makala CUP katika jimbo lake. Anamtuhumu pia kumjengea uhasama kwa mkuu wa wilaya na viongozi wengine wa chama na serikali.
Katika barua yake ya utetezi, Sadiq anakana baadhi ya tuhuma ikiwamo Makala kutumia vibaya fedha za chama. Hata hivyo, Sadiq anakiri kwamba amewasilisha baadhi ya malalamiko katika kikao hicho. Hayajataji!
Katika kile kinachoweza kuitwa "kupanga kujiokoa," Sadiq anatupia lawama baadhi ya wabunge akisema wameanza kupungikiwa na maadili ya uongozi kwa kutoa nje ya vikao mambo ya ndani ya chama."
Anasema, "…Kwa bahati mbaya sana, baadhi ya sisi wanaCCM tumeanza kupungikiwa maadili ya uongozi kwa kutoa nje siri ya vikao vya chama kama ilivyotokea."
Aidha, mbunge Sadiq anakana kuandikiwa barua ya onyo na kumtaka Makala kuacha kile alichoita "kusema uwongo."
"Katibu Mkuu, naomba Makala aache kusema uwongo. Mimi sina barua ya onyo kama anavyoeleza kwenye gazeti la Majira. Vinginevyo athibitishe," anasisitiza.
Gazeti liliwasiliana na Makala kutaka kufahamu mkanganyiko wa kauli za Sadiq. Aligoma kuingia kwa undani, badala yake alijibu kwa kifupi sana.
"Sina cha kusema. Mimi si msemaji wa chama. Kama kuna kitu, wasiliana na wahusika," alisema Makala na kusisitiza kam kuna kitu chochote wa kuulizwa ni Sadiq au Makamba.
Naye Makamba hakupatikana kuzungumzia suala hilo. Simu yake ya mkononi ilipopigwa msaidizi wake alimtaka mwandishi kuwasiliana kwa simu yake nyingine ambayo nayo hadi tunakwenda mitamboni haikupatikana.
MwanaHALISI lilipowasilina na Katibu wa CCM mkoani Morogoro, Mary Chitanda kuhusiana na madai kwamba Sadiq aliwahi kuonywa kusambaza taarifa za uwongo na uzushi dhidi ya Makala, aligoma kuzungumza kwa kusema alikuwa katika msiba.
Alisema, "Niko kwenye msiba. Siwezi kuzungumza hilo tafadhari…". Alipoombwa atoke pembeni kidogo ili aweze kujibu swali juu ya maandishi ya Sadiq, Chitanda alisema, ". Samahani… niko kanisani."
Hata hivyo, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo katika ofisi ya CCM mkoani Morogoro, 20 Aprili 2007, Chitanda alimuandikia barua Sadiq yenye Kumb. Na. CCM/MMG/C/A.60/48/C/106 inayoelekeza kwa Sadiq kuacha kuendeleza makundi ndani ya chama hicho.
"Kamati ya Siasa ya H/Kuu ya Mkoa (Halmashauri Kuu ya mkoa), iliyokutana tarehe 29 Machi 2007 pamoja na mmbo mengine… imeridhika na wewe mwenyewe kwa wepesi wa kukiri mapungufu yaliojitokeza dhidi yako. Hivyo nimeagizwa nikuandikie barua ya kukuelezea mapugufu hayo ili uchukue hatua za kijirekebisha kama ulivyoahidi."
Barua inamuonya Sadiq kutokuwa mwenepesi wa kusikiliza maneno/majungu kutoka kwa wapambe bila kuchuja. Kwa kufanya hivyo, anaendeleza malumbano na mifarakano isiyokuwa na msingi. Mbunge mmoja mwandamizi wa CCM ambaye amekuwa akifuatilia kwa karibu mvutano wa Sadiq na Makala amesema hatua ya Sadiq kukana kile alichokisema kinaweza kumuweka mahali pabaya zaidi, kuliko angeamua kufuta kauli yake.
 
Just some crooked-ribbed, riggid-necked funny blond, playing with a coin around the pit-latrine!
Hawajui vizuri wana-Apollo huyu mama!
Kuna mwingine anaitwa Thobias Andengenye...soon and very soon watapewa advertise na kukaribishwa Arusha.
cousin, inaonekana unamjua

hebu toa insight zaidi basi maana sijaelewa hata chembe hapo
 
Just some crooked-ribbed, riggid-necked funny blond, playing with a coin around the pit-latrine!
Hawajui vizuri wana-Apollo huyu mama!
Kuna mwingine anaitwa Thobias Andengenye...soon and very soon watapewa advertise na kukaribishwa Arusha.

PJ - Punguza hasira : Christmass is around the corner!
 
CHENGE KUFURU TUPU, AMILIKI BILIONI 25 (Kayumba hana hata mia mfukoni)


Na Saed Kubenea
WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge anaogelea katika utajiri wa zaidi ya Sh. 25 bilioni zenye utata huku Rais Jakaya Kikwete akiendelea kumkumbatia, MwanaHALISI limegundua.

Chenge amekuwa mfanyakazi serikalini kwa karibu miaka 30 na hafahamiki kuwa mfanyabiashara.

Kiwango kinachotajwa ni pamoja na fedha zilizogunduliwa na makachero wa Uingereza katika akaunti zake za nchi za nje.

Fedha zilizoko kwenye akaunti yake ya nchini, Na. 011101006950 katika benki ya NBC Limited, ni Sh. 25,794,805.89 za Tanzania hadi Ijumaa iliyopita, tarehe 11 Aprili 2008.

Katika akaunti yake ya Uswisi, ambako ana akaunti ya fedha za kigeni, Chenge amehamishia dola za Marekani 467,000, sawa na zaidi ya nusu bilioni kwa fedha za Tanzania.

Fedha za Uswisi zimelimbikizwa katika akaunti Na. 030105000364. Zilihamishwa kutoka akaunti Na. 011105011782 ya kampuni ya TANGOLD Limited, tangu 22 Februari 2006 kupitia NBC Limited.

Taarifa za kuaminika ambazo MwanaHALISI imezipata zinasema Chenge ni Mkurugenzi wa kampuni ya TANGOLD Limited ambayo ina dola 12,997,950.84 sawa na Sh. 15 bilioni za Tanzania katika NBC Limited tawi la Makao Makuu.

Aidha, kampuni hiyo inahifadhi Sh. 1,379, 359,367.39 katika akaunti Na. 011103024852 tawi hilohilo la NBC Limited.

Habari tulizopata wakati tukienda mitamboni, zinasema kwamba makachero wa Uingereza wanafuatilia uhalali wa Euro 3 milioni (sawa na zaidi ya Sh. 8 bilioni za Tanzania) zinazodaiwa kuwa Chenge alizipeleka kwenye akaunti zake nje ya nchi.

Taarifa nyingine ambazo hatukuweza kuzithibitisha haraka, zinasema Chenge alihamisha kwa mkupuo dola 600,000 za Marekani kwenda kwenye akaunti ya ofisa mwandamizi mmoja aliyekuwa Benki Kuu miaka kadhaa iliyopita, na ambaye kwa sasa anaongoza shirika la umma nchini.

TANGOLD ni kampuni ambayo inadaiwa kumilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na ambayo inadaiwa pia kuwa ndiyo imerithi mali na madeni ya kampuni ya Meremeta Limited iliyokuwa ikijihusisha na uchimbaji madini, Buhemba, mkoani Mara.

Hata hivyo, kuna utata juu ya lini kampuni hiyo ilianzishwa nchini. Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi aliuambia Mkutano wa Tisa wa Bunge kuwa TANGOLD iliundwa mwaka 2006 kupitia Task Force maalum ya serikali, kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni ilianzishwa mapema 2000 au kabla.

Hiyo inathibitishwa na ukweli kwamba tarehe 1 Januari 2000 walikuwa na akaunti ambayo haikuwa hata na senti moja katika akaunti zake mbili hadi 29 Desemba 2005 zilipoingizwa dola 13,340,168.37.

Fedha hizo zilikuwa zinatoka Hazina kupitia Benki Kuu (BoT).

Kwa akaunti ya fedha za Tanzania, tarehe 1 Agosti 2005, TANGOLD Limited ilichota kutoka Hazina kupitia BoT, Sh. 4,703,221,229.08 kwa hundi Na. 241741 na kufanyiwa uhamisho wa haraka (special clearance).

Chenge, akiwa mkurugenzi, anahusika na uhamishaji, ulimbikizaji na ulipaji wa fedha kutoka akaunti za TANGOLD.

Wakurugenzi na waidhinishaji malipo wengine wa kampuni hiyo ni, Daudi Ballali, Gray Mgonja, Vincent Mrisho na Patrick Rutabanzibwa.

Ballali alikuwa gavana wa BoT, Mgonja akiwa Katibu Mkuu Hazina, Mrisho akiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu Maji na Umwagiliaji.

Matumizi ya fedha kutoka akaunti hizi ambako kuna mkono wa Chenge ndiyo yanaongeza utata.

Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.

Miongoni mwa waliolipwa ni viongozi wa CCM, waandishi wa habari na wengine ambao hawakuweza kutambulika. Muhimu ni kwamba karibu fedha hizo zote zililipwa wakati uchaguzi wa CCM mwaka jana ambapo Chenge aliwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Alishinda kwa kura nyingi.

Akaunti ya TANGOLD inaonyesha kutoingiza kiasi chochote cha fedha kwa miaka mitano, kati ya Januari 2000 na Desemba 2005.

Source : Mwanahalisi
 
dah... JF is the place

mama taratiiiibu anavuliwa nguo na arrogance yake
 
KIKAO cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake (UWT) kilichofanyika Dodoma wiki iliyopita, kiliishia kuwa cha matusi ya nguoni yaliyoongozwa na Waziri wa Utawala Bora, Sophia Simba.
Mlengwa mkuu wa matusi yaliyorushwa kwa siku nne mfululizo alikuwa Katibu Mkuu wa umoja huo, Husna Mwilima, MwanaHALISI limeelezwa.
Taarifa za ndani ya kikao zinasema wajumbe walimshambulia Husna hadi akaishiwa nguvu na kulazimika kukimbizwa hospitali kuu ya mkoa iliyoko mjini Dodoma ambako alilazwa kwa saa 17.
Imeelezwa kuwa Simba hakwenda hata kumwona katibu wake hospitalini.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, wasemaji wakuu na ambao walimvurumishia matusi Husna ni pamoja na Sophia Simba mwenyewe, Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, Asha Bakari Makame na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Bara, Amina Nassoro Makilagi.
Wengine walionukuliwa wakirusha matusi kwa Husna ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Catherine Peter Nao anayekabiliwa na tuhuma nzito za kutokuwa raia wa Tanzania na Mary Chitanda ambaye ni katibu wa CCM mkoani Arusha.
Wajumbe wengine kwenye orodha ya kutoa mashambulizi ya kauli ni Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Mariaga na wajumbe Amina Kanyogotwa na Nenburis Kimbele ambaye ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha.
Mvua ya kejeli, kebehi na matusi ilianza mapema wakati wa ufunguzi wa kikao, asubuhi ya tarehe 16, Jumatatu iliyopita wakati Simba akifungua kikao.
Katika hotuba yake Simba alisema hana msaada wowowte kutoka kwa Katibu Mkuu. Alisema, "…maandalizi yote ya mkutano huu mnayoyaona ni kazi ya naibu wenu, Amina Nassoro Makilagi. Makbrasha yote ni Amina, fedha za mkutano ni Amina."
Baada ya kumwaga sifa kwa naibu katibu, mtoa taarifa ameeleza, Simba aliuliza wajumbe, "Sasa mnataka nini?" Kama vile wamepangwa, sauti zikasikika, "Mpe ukatibu. Anafaa huyo…"
Huku baadhi ya wajumbe wakiwa bado wamepigwa na butwaa, Simba aliendelea kuporomosha vijembe kwa kusema, "Umegawa kadi za harusi ya mwanao kwa kila mtu. Unataka kila mtu akuchangie. Mara wakuchangie. Arusha wakuchangie. Iringa wakuchangie. Acha hizo!"
Kama anayemfunda Husna, Simba ameripotiwa kusema, "Wewe Husna unavaa sana. Unajipenda. Unataka kufanana na Mama Salma Kikwete. Mama Salma akivaa kilemba na wewe uvae. Sisi wenzako aka… Tunajipendekeza?"
Mtoa taarifa amemnukuu Simba akisema, "…harusi ni kati yako na mumeo. Unataka kutumia UWT kutafuta umaarufu. Ondoka hapa." Wakati wote Husna alikaa kimya akitafakari yote haya yametoka wapi, ameeleza mtoa taarifa.
Kikao cha baraza kuu kilikuwa cha siku moja kilichohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba. Ilikuwa mwishoni mwa kikao hicho, taarifa zimeeleza, tena baada ya kikao kufungwa, Simba alileta hoja ya kumtuhumu katibu mkuu kuwa hana ushirikiano naye na kwamba katibu hamsikilizi.
Alinukuliwa akisema kuwa hawezi kufanya kazi na Husna na hivyo kuwaomba "wamuondoe."
Baadhi ya wajumbe walisimama na kumwambia Simba kuwa hoja yake haikuwa imeanzia kwenye kamati ya utekelezaji, hivyo pale hapakuwa mahali pake.
Mtoa taarifa anasema ndipo Simba aliamua yaishe kwa siku hiyo na kesho yake akaitisha kikao cha kamati ya utekelezaji, chini ya usimamizi wake na kuorodhesha tuhuma 12 dhidi ya katibu mkuu.
Miongoni mwa tuhuma dhidi ya Husna ni kutomtii mwenyekiti, matumizi mabaya ya fedha, kujivuna na kutomfuata mwenyekiti ofisini kwake na badala yake kuta yeye ndiye afuatwe.
Siku tatu zilizobaki zilikuwa za semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Tume ya Haki za Binadamu na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).
Kwa mujibu wa taarifa, katibu mkuu alikabidhiwa tuhuma siku ya pili ambayo ilikuwa siku ya kwanza ya semina na kutakiwa kuzijibu palepale.
Hata kabla Husna hajaweza kujibu tuhuma, baadhi ya wajumbe wakaamsha mikono wakitaka kuchangia na kuruhusiwa na mwenyekiti.
Alikuwa Catherine Nao aliyenukuliwa akisema, "Mheshimiwa mwenyekiti, huyu Husna anaringa sana. Namshangaa. Huyu nani kwani? Huyu si boi tu… Anaringa nini…?" huku baadhi ya wajumbe wakishikwa na butwaa.
Catherine alifuatiwa na Mary Chitanda ambaye alisema, "Mwenyekiti wewe ndiye umetuletea huyu mtu… sijui ulimwokota wapi halafu ukamleta humu ndani. Tuondoshee huyu hatumtaki."
Chitanda amenukiliwa akisema, "Yeye … kujipamba tu, hana jingine. Hajui kazi, hana lolote analolijua zaidi ya umbea na kutuibia fedha zetu. Tupishe bibi tufanye kazi zetu."
Taarifa zinasema Chitanda alifika mbali zaidi na kusema, "Hata kama watu watapeleka ujumbe kwa ‘bwana mkubwa,' kikao hiki ni cha mwisho, hakuna mwenye uwezo wa kutuingilia."
Ujumbe kwa "bwana mkubwa" umeelezwa kuwa ni ujumbe wa simu ya mkononi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambao haikuwezekana kuthibitishwa.
Imedaiwa kuwa wakati wa kuporomosha matusi kwa Husna, kuna aliyepeleka ujumbe kwa Kikwete kueleza hali ilivyo ukumbini. Imedaiwa kuwa Kikwete aliandika juu ya ujumbe huo maneno, "Mtendeeni haki Katibu," na kuupeleka kwa kiongozi mmoja wa CCM.
"Mimi ninao hapa, lakini siwezi kukuachia unukuu. Unajua ninyi waandishi mna mengi," ameeleza mmoja wa wajumbe. Imeelezwa kuwa mmoja wa maofisa wa umoja huo aliusambaza kwa wajumbe wengi.
Baadhi ya wanaotajwa kusambaziwa ujumbe huo ni pamoja na Simba, Mary Chitanda, Catherine Nao na Nenburis Kimbele, mjumbe wa Baraza kutoka Arusha.
Hata hivyo Chitanda amenukuliwa akisema, "Haya mambo ni yetu sisi. Watu wanapeleka umbea kwa bwana mkubwa. Baraza hili ndilo lenye uwezo na mamlaka ya mwisho ya kuamua nini kifanyike, mwenyekiti muondoe huyu mtu…"
Ilikuwa baada ya mashambulizi haya, Husna aliomba kujibu tuhuma. Kwa mujibu wa mtoa taarifa, naye alianza kwa jazba akishambulia wenzake, lakini mjumbe Zaria Madabida ndiye amenukuliwa akisema, Husna "Anasakamwa kwa mambo yasiyokuwa ya msingi."
Alisema haoni kosa lolote na bali anaona kuna njama zilizopangwa na baadhi ya watu kwa malengo binafsi.
Wengine waliomtetea Husna ni Zainab Vulu, Dk. Zainab Gama, mwenyekiti wa UWT Manyara ambaye amejulikana kwa jina la Maria na Amina Masenza, mkuu wa wilaya wa Shinyanga.
Maria alisema, "haiwezekani mtendaji mkuu akashambuliwa na watu tukakaa kimya."
Kauli ya Maria iliungwa mkono na Amina Masenza, ambaye alimtaka Simba kuachana na njama za kumsakama katibu wake.
Alhamisi ya tarehe 19, baada ya wajumbe wengi, mmoja baada ya mwingine, kushambulia katibu mkuu, na yeye akiwa amesimama akitaka kusoma utetezi wake, Asha Bakari Makame, Makamu mwenyekiti UWT Zanzibar alimrukia na kudai kuwa siyo utaratibu kwa mtuhumiwa kusoma utetezi wake.
Ndipo Simba akasoma utetezi wa Husna ambamo alikana tuhuma zote. Aliamriwa kutoka nje wakati wanajadili na kupitisha maamuzi ambao imefahamika kuwa ni "onyo kali."
Habari za ndani ya UWT zinasema chanzo cha ugomvi kati ya Husna na Simba ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT, Tanzania Bara, Amina Makilagi, ambaye inadaiwa anatamani nafasi ya Husna. Amina hakupatikana …
Makamu mwenyekiti Zanzibar Asha Bakari Makame alipoulizwa kuhusu sakata hili na hatua gani zimechukuliwa dhidi yake, alisema hawezi kuongea na waandishi wa habari mmojammoja. Alisema angeongea na vyombo vya habari jana.
Naibu katibu mkuu Zanzibar Salama Aboud amesema yuko kwenye kikao na kwamba asingeongea lolote kuhusu suala hilo.
Naye Sophia Simba alimwambia mwandishi wa habari hizi kwa maneno mawili ya Kiingereza, "No comment" – sina la kusema.
Simu ya Mary Chitanda iliita bila kupokelewa; naye Amina anayedaiwa kutaka nafasi ya Husna, hakuweza kupatikana. Simu yake iliita bila kupokelewa.
Husna alipotakiwa kuzungumzia sakata hili, alisema ni kweli alituhumia lakini akaongeza, "Sijawa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hili."
Hata hivyo, kikao cha baraza kuu hakina uwezo wa kumvua madaraka katibu mkuu bila kurejea kwenye Kamati Kuu ya CCM.
Katika kipindi cha wiki tatu, Simba amemsifia aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa kuwa ni "mwanaume wa shoka" na amewaparura Mzee John Malecela na mkewe Anne Kilango kwa madai kuwa wamewahi kufadhiliwa na Jeetu Patel ambaye sasa ni mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi nchini.
Katika kipindi hichohicho, Simba ametangaza kuwa katika CCM hakuna aliye safi.
Mashambulizi ya sasa dhidi ya Husna yanachukuliwa kuwa mwendelezo kwa wale ambao haafikiani nao.
Gazeti toleo na. 164
 
Back
Top Bottom