Who is Hussein Mohammed Bashe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Who is Hussein Mohammed Bashe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamalunde, Jun 17, 2009.

 1. M

  Mwanamalunde New Member

  #1
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari za hapa Jamvini wanzengu nimekuwa mgeni kwa mara ya kwanza leo nimeingia hapa na nimejikuta naingia baada ya kupewa ushauri na jamaa zangu hapa mjini kuwa kama unataka taarifa za uhakika angalau kwa asilimia 70 basi jiunge na mtandao unaoitwa jamii forums.

  Ushauri huu nimepewa baada ya mimi kutoka ktk mkoa wa Tabora kikazi na katika pitapita yangu nilifika wilaya inayoitwa Nzega na katika shughuli nikauliza maswala ya kisiasa na kumuongelea Mbunge Lucas Selelii, hapo nilistuka nilipoambiwa 2010 ana nafasi ndogo sana ya ushindi kwani kuna kijana anaitwa Huseni Bashe wa UVCCM ambaye anapewa nafasi kubwa na amembana sana kamanda wetu.

  Namevutiwa/nimestuka na jambo hilo nikona nije hapa niweze kumfahamu kama kuna watu wanamfahamu wanieleimishe na kufahamu huyu mtu anatoa wapi hizo nguvu za kuweza kufikia hapo.
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Kumbe taarifa unazo sasa umekuja kupima maji sio?

  Wapiga kura wa Nzega wataamua kama "kamanda" wako amebanwa au laa
   
 3. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hussein Bashe ni kujana wa kisomali lakini anajiita mnyamwezi wa Nzega.

  Kwa sasa anaishi Dar na ni kijana wa karibu sana wa Rostam Aziz ambaye ndiye anamfadhili kuhakikisha anamng'oa Selelii ambaye ameonekana kuwa mwiba wa mafisadi. Na sasa hivi anafanya kazi New HABARI (2006) Limited inayomilikiwa na Rostam kama meneja fulani.

  Ni kijana mdogo kwa umri na anapenda sana siasa. Babaye nasikia ni shehe huko nzega.
   
 4. TreasureFred

  TreasureFred Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwanamalunde karibu jamvini

  Hussein Bashe ni kijana mwenye asili ya kisomali mwenye umri usiozidi 30 ambaye ni mjumbe wa baraza kuu la uvCCM taifa na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa, pia mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa tabora akiwa ni muwakilishi wa wilaya ya Nzega, na nasikia ana cheo kingine kwenye kata n.k kama kawaida yao CCM, mwaka jana alikuwa mgombea wa nafasi ya umakamu wa mwenyekiti uvCCM taifa akashindwa na Beno Malisa.

  Bashe 2005 akiwa ametoka chuoni aligombea kura za maoni ndani ya CCM akawa ni mtu wa pili kati ya wagombea tisa kwa tofauti ya kura 36 kama sijakosea akiwa amezidiwa na Selelii, katika siasa za mkoa wa Tabora hasa wiliya ya Nzega si ajabu kuwa na taarifa ya namna hiyo kwamba amembana Selelii, kwani hata 2005 ambapo Selelii alikuwa ni mtu wa karibu na mafisadi wa leo ambao wakati ule walikuwa ni watu wema Bashe alimbana sana Selelii mpaka kufikia uchaguzi mkuu ufunguzi wa kampeni CCM kushindwa kuzindua kampeni na kumuomba kijana huyo aje kufungua kampeni na kumsaidia Selelii.

  Hayo ni ya haraka haraka ngoja nikafanye home work yangu
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Hussein Bashe? mzee achana na habari hizi, kama uanakitu unataka kuteleza just come clean, kwani nashangaa unawezaje kujua majina matatu ya mtu ambaye mara zote hutajwa kwa majina mawili? ulipita Nzega lakini ukasubiri kuja JF ndio uulize sifa zake tutake radhi, au nenda kajipange upya hiyo ni very low kwa standard za JF...aaaaaaaaaagggggghhhhrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Uko makini B....
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Exactly! mtu kapita huko jimboni asitafute habari za Bashe anakuja uliza jf!
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Duh, kuuliza ni ujinga? yeye ame centre swali lake kwenye anatoa wapi hizo NGUVU?

  Kama hamujui kaeni kimya sio kumsakama.
   
 9. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo baadhi ya watu wanajua nafasi za ubunge ni kwa ajili ya wastaafu! huyu anayeuliza kiini cha swali lake ni pale alipouliza anapata wapi nguvu? binafsi namjua Bashe kama kijana mmoja makini sana ambaye mara nyingi husimamia kila anachokiamini bila kujali kama kuna mtu atakereka na msimamo huo, msomi mzuri, mcheshi na mpenda watu aligombea Nzega 2005 na alifanya kampeni kwa muda wa wiki 2 tu lakini alichachafya wazee, ni kijana ambaye ni mpenzi sana wa vijana wa Nzega, kina mama wa Nzega na wapenda maendeleo wote wa Nzega ,ni kweli kuwa kam-bana sana Seleli si dhambi kumbana mtu kwani katiba ya chama inaruhusu uchaguzi wa nafasi za ubunge vinginevyo wabunge wangekuwa wanateuliwa tu na kamati za chama bila kufanyika uchaguzi wowote so keep it up Bashe1
   
 10. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Karibu Mwanamalunde! Kwanza unapoingia sehemu ukiwa mgeni jambo la kwanza ni kuulizia taratibu na destuli za mahali husika, kwa hapa JF utaratibu wa jinsi ya kulitumia jamvi umewekwa kwahiyo ilikua ni jukumu lako kwanza kusoma halafu ndio uje na swali lako! Kwanza ungepitia kwenye jukwaa la utambulisho halafu ukishajitambulisha ungeenda kwenye Celebrities forum kwa ajili ya hili swali lako, sawa mkuu! hapa (Jukwaa la Siasa) hajujadili watu tunajadili hoja mbalimbali! kwa mara nyingine karibu sana.
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo kama bashe ameandaliwa kumtoa selelii....kazi ipo mafisadi kwelii wana nguvu ndio maana babu wa watu anatapatapa....sijui itakuwaje ngoja tuone mwisho wake......ila fitina siasa za tz na hatma ya nchi
   
 12. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Seleli atapimwa na wananchi wa nzega kwa maendeleo aliyopeleka huko na si kwa kumbana Rostam na mafisadi pekee. Seleli amekuwa mbunge wa nzega kwa muda mrefu sasa (nadhani hii ni term yake ya tatu), ni hivi karibuni ameonekana kuwa mwiba kwa serikali na mafisadi. Sina hakika kama inamsaidia sana. Kuwabana mafisadi ni jambo zuri lakini upande wa pili wapiga kura wanataka maendeleo pia.

  Je mnamkumbuka bwana Simpasa alikuwa mbunge wa Mbozi, alikuwa msemaji sana. Sasa hivi yupo wapi? Alitoswa na wapiga kura kwa sababu hakupeleka maendeleo jimbo kwake.

  Seleli wabane mawaziri kisawasawa ili upeleke maendeleo nzega, kwa kufanya hivyo utakuwa na nafasi kubwa kuliko huyo bwana Bashe.
   
 13. u

  urassa Member

  #13
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni mwanzo wa kupata umaarufu, Selelii has to step down and leave young blood kufanya vitu vyake.
  Hizo ni nguvu zake binafsi, kwani hata 2005 hakuwa na support yoyote ya unavyowaza kwani Selelii alikuwa ameshikamana kisawa sawa na hao mnaowaita mafisadi na ndio hao waliomwezesha selelii kupata Ubunge wakati Bashe anapambana alone,
  Hadi leo yuko kivyake vyake yeye naturally ni MPAMBANAJI ana kipaji na uwezo mkubwa wa kupambanua hoja inayokuja mbele yake.MWACHENI
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Haitashangaza ikiwa aliyepost thread hii ni Bashe mwenyewe kwa lengo la kujipima -- yaani ajue anajulikana kiasi gani na kwa yapi. Kama ni madhambi ajue umma unayajua yepi na kwa kiasi gani, ili anapojitosa kumn'goa Selelii awe ana uhakika anasimamia wapi.

  Vinginevyo aliyeweka thread hii ni Selelii mwenyewe kwa malengo kwamba wenye kujua madhambi ya Bashe wayatoe ili apate nyenzo za kumsagasaga. Kumshinda Selelii katika uchaguzi Bashe atategemea fedha za RA (i.e za wananchi alizokupua) na si charisma au uwezo wake -- vitu viwili ambavyo hana kabisa.

  Nimesoma kwenye post ya thread moja hivi karibuni kwamba Bashe ameshindwa kabisa kuongoza kitengo cha usambaji wa magazeti ya Habari Corp, mahali alipo, na kusababisha kuporomoka kwa mauzo ya magazeti.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Jee una ushahidi wowote wa RA ku ''kupua'', au na wewe ni katika wale wenye agenda za siri, akina Mwanakijiji?
   
 16. GreatConqueror

  GreatConqueror Member

  #16
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kuna watu siku hizi wanaitumia JF kupima upepo wa kisiasa na kijamii. Haingii akilini ufike Nzega halafu usipate taarifa za Hussein.

  Anyway binafsi siasa za mkoa wa Tabora nimejaliwa kuzijua japo kwa kiasi fulani. In short ni kijana mpenda sifa na yuko tayari kushirikiana na mtu yeyote ili afikie malengo yake kisiasa.

  In short hajawahi kumbana Seleli kwenye uchaguzi wowote! Matokeo ya kura za Maoni jimbo la Nzega mwaka 2005 ni ifuatavyo:-

  1.Lucas Seleli 407


  2.Abdallah Nasoro 150

  3.Hussein Bashe 90.

  Kwa mujibu wa ofisi ya CCM Nzega.

  Mtu pekee aliyewahahi kumbana Seleli ni Abdallah Nasoro mwaka 2000 aliposhinda kura za maoni lakini alienguliwa na NEC. Kama kuna mtu ana matokeo tofauti na haya ni PURE FABRICATION.

  Nimeamua kutoa takwimu hizi ili kuweka kumbukumbu sawa. Wana JF jioneeni tofauti ili mjue nani alibanwa 2005.

  Sifa nyingi anazopewa humu JF ni tofauti kabisa ni jinsi tumjuavyo.

  Nawasilisha.

   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Karibu sana
   
 18. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Kaazi kweli kweli .. Seleli vs Bashe na Conqueror vs Treasure - ni mwendelezo wa vita dhidi ya Ufisadi ? Ngoma nzito... the wazalendo vs the wakuja ??
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Upo upande gani hapo..?
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dar es Salaam:

  Ushahidi wa kimazingira kibao, unless ulikuwa husomi posts zaidi ya 1,500 za humu JF kuhusu RA na ukwapuaji wa Kagoda. Lakini kikubwa ni kwamba waendesha mashitaka hawataki kufanya upelelezi hasa katika kutafuta ukweli hela za kagoda zilizoingia katika matawi ya CRDB katika akounti 6 zililipwa kwa nani, na mkondo wake, kama ulifuatiwa na hao "wapelelezi" wetu ulionyesha ni nani last beneficiary, kama siyo RA. Basi watu-provie kama siyo yeye kwa kumtaja huyo beneficiary mwingine.

  Lakini Mkuu, haya na mengineyo yanayomnyooshea kidole RA tunayarudia tu hapa, yamezungumzwa sana, unayaleta tu kwa kuendeleza ubishi.
   
Loading...