Geor Davie ni nani?

Kwanza kipindi cha kufundisha neno ni kidogo sana ktk ibada ni ka dk 15 tu, muda mwingi ni miujiza na blah blah, halafu ana injili ya vitisho ka vile usipotoa sadaka biashara yako itafilisika na vitu ka hivyo, na ktk mahubiri yake hujisifu sana na kutumia kauli ka Roho mtakatifu ni mbabe n.k kama unalijua neno ukisikiliza mahubiri yake utaguna mpaka ung'ate ulimi. Mbali na hayo ana kashfa nyingi sana za uzinzi na hadi kuna ndoa amezivunja na ushahidi uko, pia jinsi anavyowatreat wasaidizi ni vituko

Nilisikiliza mahubiri yake nikazima redio kwa haraka maana nilihisi ni shetani anahubiri....

Nafikiti kadiri siku zinavyokwenda huyu jamaa atajita mungu....

Kanisa lake ila linaanza kufa taratibu..
 
Huyu ndugu jina lake halisi ni George David Kasambale ni mwenyeji wa Singida mi nlianza kumfahamu miaka ya tisini alikuwa tarishi pale world vision, Arusha alikuwa pia mwanamziki wa nyimbo za injili ktk mikutano mbalimbali na alikuwa anasali ktk kanisa la Siloam Gospel Assembly lililokuwa linasali ktk shule ya msingi Uhuru Arusha.

Kwa kipindi hicho mi nlikuwa mwanafunzi wa primary tulikuwa tunamuita Nyakizanya kwa sababu ya wimbo wake maarufu ''Nyakizanya umeokoka'' ila alikuwa kijana wa kipindi kile na alikuwa ana mambo yake ya ujana ka kuvaa mabagi na kunyoa pushback kitu kilichomfanya asikubalike na wachungaji wengi wa kiroho hapa Arusha.

Si kumsikia tena hadi miaka ya kuanzia tisini na sita hivi alikuwa na studio ya nyimbo za injili iliyoitwa supreme na baadae ikawa radio station ila ilikuwa inasikika baadhi ya sehemu za Arusha. Ila kutokana na ujanja ujanja wake na ambitions yake aliweza kukutana na wazungu na kufungua kituo cha watoto wa mitaani ingawa alikuwa anao ka watano hivi wa kuzugia.

Kituo hichi kilikuwa majengo karibia na Sacon Opposite na kanisa la KKKT Burka, baadaye alihamia Kisongo baada ya kuwa na fedha, aliwaondoa wale watoto kwa namna mbaya sana mmojawapo ni rafiki yangu ni fundi TV, ndio ghafla tukasikia Nabii GeoRDavie, kanisa lake liko kisongo mnadani na ofisi zake ziko huko ktk mashamba yake maarufu ka ''mji wa Daudi'' kwa kweli huduma yake imejaa contrervasial saana maisha yake pia yana utata.

Means jinsi anavyiobehave pamoja na family life yake kwa ujumla watu wanaomfahamu tangu kitambo hawamuelewi. Ila hatuwezi kusema sana tusije tukakufuru ila kwa upande wangu mmhh.

Simkubali na hii ni kutokana na matunda yake yaani tabia huwezi kuwa na upako kiasi hicho afu matendo ni design ka yake ila sijui? Siwezi sema ni mtume wa Mungu au la ila kuna maswali mengi sana kuliko majibu.

Mkuu kwa maelezo uliyotoa na jinsi uyu mtu alivyo ni vilevile, nayasadiki 100%...ngoja nisiongeee hapa
 
Eti kuna mtu alimnyang'anya mke....Huyo anayedai alichukuliwa mke alikuwa wapi??? watu wengine wakipata wake wazuri kazi kuwapiga ovyo na kuwatesa...mwanamke ameamua kujishika kisawasawa na Mungu wake. oooh nimenyang'anywa!!! alifikiri mke ni kibega!! ulipokuwa unampiga na kumchoma moto na kumpeleka police ulifikiri ni mtumwa!!!!

Mkamate Mungu wako kisawasawa mama!!! acha waseme mpaka wafe!!! Tena huyo jamaa asipotubu cha moto atakiona manake Mungu huwa anaangalia penye haki. Hivi GeorDavie ni mtu wa kumchukua mke wa Mtu??? kwa taarifa yake hakunyang'anywa na GeorDavie alinyang'anywa na Mungu...ajifunze jinsi ya kumtunza mwanamke, kumhudumia na kumpenda kwa dhati, Haoni hata aibu??!!! Mwanamke ni almas baba! sifa ya mwanamke ni abembelezwe!!

Kama ameshajifunza vya kutosha amwombe Mungu amrudishie mke wake. Watu wanaongea na kumsema mtu wa Mungu vibaya wakati hawajui ukweli uko wapi! Kwa hiyo alikuwa anampiga akifikiri kwa kuwa anamjua Mungu ataacha kuondoka au ataacha kusali. Tena ninamshauri huyo mwanamke asije akaondoka kwenye hiyo huduma hata angemrudia huyo mume!

Mkamate Yesu mama wa Upako!!! Simama Imara, kishujaa maneno yasikurudishi nyuma. walitaka wakukute kwenye nyumba ya mganga wa kienyeji. Sugua goti mama sijawahi kumwona aliyemkimbilia Mungu akiaibika!

Ktk kusoma kwangu kote Bible from Genesis to Revelation sijawahi ona utumbo kama huu, ushabiki ni mbaya, unaacha kushabikia maneno mema ya Mungu unamsingizia Mungu kufanya ujinga huu, wakat ni tamaa ya miili yenu ninyi wanadamu, Nasema OLE wako!!Tena na Utubu maana na uhakika Mungu hawezi fanya iyo pumba
 
naona jamaa ameamua kutuma jeshi la kumtetea,wapi imeandikwa mume akikupiga ukimbilie ukalale na mtumishi wa mungu aka nabii na mtume na uhamie kabisa kwake?utelekeze na watoto?hiyo ni roho au unyama?hata biblia inasema NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE,nyie mnaotetea huu uchafu MUNGU anawaona.huu unafiki wa kilokole ndo nisioupenda,bora nibaki na biblia yangu niisome ndani kwangu nimwombe mungu wangu kuliko kujifanya mtu wa maombi na kulia mbele za watu kumbe unafiki mtupu.only GOD will judge me.

Mkuu ulokole si Unafiki ila tu Umevamiwa na wafanyabiashara wa injili Feki na watu wanafiki
 
Nahisi ni tapeli(GOD forgive me),imeandikwa siku za mwisho watajitokeza manabii wengi wa uongo,i think na ye ni mmoja wapo
 
NABII MKUU DR. GEORDAVIE ni nabii wa MUNGU anae fanya huduma yake ya kinabii nchini Tanzania , makao makuu yako (KISONGO) ARUSHA
Kuna watu wanasema eti ni anatumia nguvu za giza huo ni uongo kabisa.Anafundisha neno la MUNGU mfano (KUENENDA NA VIWANGO VYA SERIKALI. TUKUFU VYA UFALME WA MUNGU) pia anafungua watu weye vifungo mbalimbali ikiwemo magonjwa majini nk.Pia yeye ndie NABII WA KWANZA TANZANIA KUKEMEA WAGANGA WA KIENYEJI NA WACHAWI.
WENYE MATATIZO YOYOTE NGURUMO YA UPAKO NDIO JIBU LAKO YANI NI MANENO MACHACE KAZI KUBWA ZAIDI!
 
Kwa wale msiojua,Mheshimiwa Baba Nabii Geor Davie Ngurumo ya Upako anaonekana channel teni kila jumanne sa 2 usiku.

Karibu umuangalie msemaji wa serikali ya Mungu duniani karne ya 21.. Tanzania tumebalikiwa,Mungu anasema na dunia kutokea hapa kwetu Tanzania.

shapeimage_3.png
 
Hivi kuna umuhimu gani wa kuunganisha his Excellency na honorable kwa pamoja?


Huyo uheshimiwa kautoa wapi?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom