Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Rev Kishoka:

Kwanza ningependa kukukosoa. Hakuna kitu cha bure. Vile vile misingi ya Ujamaa au usoshalisti haisemi kuwa
elimu au huduma za afya zitolewe bure.

Ujamaa na usoshalisti vyazo vyake ni umilikaji wa mitaji na mgawanyo wa mapato. Elimu iliyotolewa bure ilikuwa ni
sehemu ya mgawo wa mapato.

Lawama alizopata Nyerere ni sahihi kabisa. Kama elimu au huduma za afya ni sehemu ya mgawo wa mapato, je ni juhudi
gani watanzania walifanya kustahili mgao huo?

Vitabu vya Nyerere vinasema juhudi za kazi za watanzania zitumike katika kutoa elimu au kupata huduma za jamii. Lakini
hayo yaliishia vitabuni. Kwenye utendaji huduma zilitegemea mikopo na misaada kutoka kwa wahisani.

Mnaopiga kelele kutetea Nyerere kwa kutoa elimu ya bure naomba mtueleze ni vitu gani vilifanyika Tanzania kuweza kutoa elimu
ya bure. Watu hamna aibu kuona taifa mpaka leo linategemea misaada kutoka nje.

Zakumi,

Hakuna ambaye amesema kuwa Nyerere hakufanya makosa! Hata yeye mwenyewe alikiri hilo!

Sasa naomba niuulize, tukufanye wewe ni Rais wetu wa kwanza na ndio tumepata Uhuru, nchi ni changa, elimu na afya ni finyu na haba na hauna watu mahiri wa kutosha. Zaidi unabeba mzigo ulioachiwa na mtawala.

What would have Zakumi done? Tupe basi Manifesto yako ya ni jinsi gai ambavyo tungejenga Taifa letu na kuachana na utegemezi wa misaada.
 
Tatizo ni kwamba adherents wa J.K. Nyerere wanadhani kwamba tukisema huyu hero wetu alikosea pale na hapa basi ghafla ataanguka kwenye pedestal tuliyomuweka. Ataacha kuwa Baba wa Taifa. Wanahofia hilo. Mimi naamini J.K. Nyerere ni mnara na muasisi wa nchi yetu. Tena, let me break it to you, binafsi nadhani makosa ya kiuchumi tunayombambika J.K. Nyerere inawezekana ni yetu wote - Ujamaa ulishindwa, wataalam wanasema, moja ya sababu ni wananchi hawakuwa na mwamko/nia/motivation. Hili nadhani ni la wote, japo ni J.K. Nyerere ndie alichora mchoro. Tunapokosoa era ya J.K. Nyerere kwa namna fulani tunajiangalia wote, tukiongozwa na J.K. Nyerere, tulikosea wapi? Ili tusibugistepu tena. Sio vibaya tukaangalia tulipojikwaa, nakubaliana na wewe kabisa.



Japo alichofanya kufungulia watu thread nyingine amefanya ki-kejeli kejeli (angalia aliyoandika mle ) bado namuelewa, thread lazima iwe na muelekeo. Tatizo ni kwamba anasema hapa sio pa kueleza mapungufu ya Nyerere lakini anaona ni poa topic zisizohusika kabisa za kumpamba pamba J.K. Nyerere kupitia vipaza sauti vyake kama Mzee Bomani. Kwa hiyo, unaweza kuleta lolote hapa, mada yoyote hapa ya Nyerere, al muradi umuimbie imbie mapambio J.K. Nyerere. Hata ya kupotosha! Rev. Kishoka anaonyesha double standard.


Mimi kinachonikwaza zaidi ni kwamba Watanzania wengi hawajapewa taarifa zote za kilichojiri kuhusu era ya J.K. Nyerere. Bado wanalishwa taarifa za kina Mzee Bomani (tena hapa na assume kwamba ni kweli Mzee Bomani kamwambia Jasusi haya mambo). Simlaumu sana J.K. Nyerere kuhusu idea zake za Uchumi, ila napenda dunia ijue ukweli wa kilichojiri.


Inakera, lakini ukikumbuka kwamba wakati wa J.K. Nyerere wewe Jokakuu ungepandishwa kwenye Land Rover na kitambaa cheusi usoni na pingu ukapelekwa kwenye chumba cha giza kwa mateso, au kijijini kwenu, basi adhabu za kina Painkiller na Ole ni cha mtoto.



Swadakta. Hamna mtu level-headed hapa na menye civility kama Rev. Kishoka. Lakini kwenye mijadala inayogusa hisia zake kama huu, anashindwa kuwa consistently even-tempered. Inasikitisha.

Kuhani,

Hivi unamaana kututamkia wazi kuwa Nyerere alikuwa akiwafanyia watu mateso?

Sasa kama hiyo dhana ya kusema Nyerere alitesa watu, je dhana ya kusema waliomfuatia waliua watu utasemaje?
 
Nadhani ni ile nidhamu yetu ya woga ndio iliofanya wengi wasithubutu kuzichallenge hoja za Nyerere hence kuaminika kuwa hoja zake ni kali. Pia sidhani katika nchi ya watu millioni 30 kusiwe na watu hata kumi wanaoweza kwenda toe to toe na Nyerere. Angalia jinsi watu wanavyojadiliana kwa uhuru hapa...enzi za Nyerere kulikuwa na uhuru kama huu kweli?

Nyani ( I hate to call you Mc Pain)
Sasa ile nidhamu ya woga ilitoka wapi? Was it Nyerere's eyes? Maana kuna wakati niliongea na Nyirabu (rip) na akasema kabla ya kwenda kuonana na Nyerere alikuwa anapiga simu Ikulu kuwauliza wasaidizi wake Nyerere yuko katika mood gani siku hiyo. Why? Watu wengi sana nimepata kusikia wakiitwa Ikulu walikuwa wakitetemeka.
 
Kuhani,

Hivi unamaana kututamkia wazi kuwa Nyerere alikuwa akiwafanyia watu mateso?

Sasa kama hiyo dhana ya kusema Nyerere alitesa watu, je dhana ya kusema waliomfuatia waliua watu utasemaje?

Yes alitesa watu, Baba yangu alikuwa mmojawapo, na hakuishia hapo, baba yangu aliishi kwa maisha ya wasiwasi maisha yake yoote na UWT walikuwa wanatusumbua kila mara. Na ndio maana nilisema mwanzo kwamba mwalimu alikuwa hataki kusikiliza watu na ndio tatizo lake.
 
Nyani ( I hate to call you Mc Pain)
Sasa ile nidhamu ya woga ilitoka wapi? Was it Nyerere's eyes? Maana kuna wakati niliongea na Nyirabu (rip) na akasema kabla ya kwenda kuonana na Nyerere alikuwa anapiga simu Ikulu kuwauliza wasaidizi wake Nyerere yuko katika mood gani siku hiyo. Why? Watu wengi sana nimepata kusikia wakiitwa Ikulu walikuwa wakitetemeka.
Mimi nadhani tabia yake ya kutesa na kupinga wapinzani wake (kuwafunga) ndio kilichofanya watu wamuogope, lakini sidhani watu wamuone yeye kama Mungu or something, kama watu wakitofautiana na wewe unawafanyia mambo mabaya kweli watu watakuogopa, kwa hiyo alishajiwekea mazingira ya kuogopwa na ndio maana watu wakawa wanaogopa kwamba ukibishana naye utaishia pabaya, ndio maana akawa hana washauri. Kama mtu anakuwa hivyo watu watakuwa wakifuata anayoyasema na hawambishii.
 
Re: Who influenced Nyerere: his Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Ninaamini kuwa Mwalimu, kuna mazuri na mabaya aliyoyafanya kama kiongozi, na ninaamini kwa 100% kwamba haya mawazo ya Ujamaa na Azimio, yalikuwa ni yake yeye mwenyewe Mwalimu, kwa sababu kusema kuwa alikuwa influenced ni kujaribu either kumshusha hadhi kuwa hakuwa na huo uwezo wa kufikira kwenye hiyo level, au kujaribu kumkwepesha na lawama behind mawazo yake hayo bila ya kukusudia au kwa kukusudia,

Ninaamini yalikuwa ni yake mwenyewe, anaweza kuwa alipata msasa kidogo hapa na pale, lakini it was his ideas, kwa hiyo kwenye sifa za hizo ideas ambazo zipo apewe heshima yake, na kwenye mapungufu yake pia apewe halali yake kwa 100%, bila kusingizia anybody,

Binafsi sikubaliani na karibu 90% ya mawazo yake, lakini at the same token siamini kwamba Mwalimu, anapaswa kuwa subject wa kila tatizo la leo la Tanzania, kwa sababu pamoja na makosa yake pia yapo mazuri yake mengi, infact ni lazima tukubali kwa kukumbuka kuwa mpaka mwaka 1980, nchi ilikuwa bado ni nzuri na maisha yalikuwa fair and balanced, Tanzania bado tulikuwa na middle class, mambo yalianza kuharibika mwanzoni mwa 80s,

Kuna kiongozi mmoja aliyekuwa karibu na Mwalimu, then aliwahi kuniambia kua Mwalimu, made some bad investment decisions na serikali ikaishia kutapeliwa na watapeli flani huko majuu katika hiyo process nzima ya investiment, lakini sina uhakika how good and truthfull is this theory, sasa reading between the lines ya hii thread, unagundua kuwa hatuna uhakika na exactly what was Mwalimu's political mistakes, kwa sababu some of what we call his mistakes ukweli ni kwamba were his strengths ambazo mzizi yake ndio hasa msingi wa utaifa wetu leo, na tatizo kubwa kuliko yote ni kwamba wengi wetu hatumpendi period! Sasa Mother Theresa aliwahi kusema kuwa huwezi kumhukumu mtu ambaye humpendi tayari, na hata kabla ya kumpa nafasi ya kumfahamu vizuri.

Ninaomba kuwakilisha hamsini zangu.
 
Yes alitesa watu, Baba yangu alikuwa mmojawapo, na hakuishia hapo, baba yangu aliishi kwa maisha ya wasiwasi maisha yake yoote na UWT walikuwa wanatusumbua kila mara. Na ndio maana nilisema mwanzo kwamba mwalimu alikuwa hataki kusikiliza watu na ndio tatizo lake.

Lusajo,

If you do not mind, je kwa nini Mzazi wako na familia yenu mliishi kwa wasiwasi? Je alifanya nini mpaka Nyerere akawa anamwinda

Samahani kuuliza hili na kutoka nje ya mada.
 

Kuna kiongozi mmoja aliyekuwa karibu na Mwalimu, then aliwahi kuniambia kua Mwalimu, made some bad investment decisions na serikali ikaishia kutapeliwa na watapeli flani huko majuu katika hiyo process nzima ya investiment, lakini sina uhakika how good and truthfull is this theory, sasa reading between the lines ya hii thread, unagundua kuwa hatuna uhakika na exactly what was Mwalimu's political mistakes, kwa sababu some of what we call his mistakes ukweli ni kwamba were his strengths ambazo mzizi yake ndio hasa msingi wa utaifa wetu leo, na tatizo kubwa kuliko yote ni kwamba wengi wetu hatumpendi period! Sasa Mother Theresa aliwahi kusema kuwa huwezi kumhukumu mtu ambaye humpendi tayari, na hata kabla ya kumpa nafasi ya kumfahamu vizuri.

Ninaomba kuwakilisha hamsini zangu.

Hamsini zako zimefika.

Mkuu, heshima mbele.
 
Ya Jenerali Ulimwengu yamenigusa!

Azimio la Arusha lenyewe lilikuwa kwa kiwango kikubwa ni azimio la Nyerere, ingawaje lilipitishwa na Halmashauri Kuu ya TANU, na kwa kuungwa mkono na maelfu ya Watanzania, likawa azimio la Watanzania wote.

..Ukweli ni kwamba hakukuwa na mjadala uliowahusisha wananchi (au hata wana-TANU) katika utungaji wa azimio lenyewe wala katika mbinu za utekelezaji wake.

Nimeshawahi kuona mahali pengi mawazo kama haya ya ‘wasomi’ kwamba miaka hiyo kabla ama baada ya Uhuru “hakukuwa na mjadala uliowahusisha wananchi katika maamuzi ya kisiasa…….” Pengine tungejiuliza kidogo, hivi wakati huo kabla ama baada ya Uhuru, wananchi wangapi walikuwa na uelewa kisiasa wa kuweza kuchangia mawazo kikamilifu katika kutunga kitu kama Azimio la Arusha ama mbinu za utekelezaji wake? Wananchi waliokuwa na uelewa wa hata namna masuala ya utawala ama mchezo wa siasa ulivyo walikuwa ni wachache mno. Baadhi ya wasomi wachache Waafrika waliokuwepo wakati huo waliogopa kujiitosa kwenye siasa kwa kuogopa kupoteza ajira zao maana Mkoloni alikuwa haruhusu waajiriwa Serikalini kujiingiza kwenye siasa. Kwa hiyo, hata hao waliokuwa viongozi wa Chama cha TANU wengi wao walikuwa hawana kisomo chochote. Kwa maana hiyo walikuwa wakisikiliza na kutegemea mawazo ya watu kama Mwalimu wawaongoze. Ndio hao walioibuka na kaulimbiu ya “Zidumu Fikra…” Hata humu tukianza kuimba “Zidumu Fikra za Mchungaji Kishoka” sidhani kwamba atatuambia ‘ah sitaki jamani’, tumeamua wenyewe hakutuomba wala kutulazimisha! Hata hivyo, Mwalimu alikuwa mwenye busara aliwahi kuikana kaulimbiu hiyo.

Nikirudi kwenye uelewa mdogo wa siasa wakati huo, ni dhahiri kwamba kama Mwalimu angeliutaka/kuupenda ubepari akaujengea hoja, akauhubiri/kuupigia debe, asingelishindwa kupata wafuasi wengi wa kumuunga mkono. Moja ya sababu za Mwalimu kulivalia njuga suala la ‘elimu kwa wote’ kwa makusudi kabisa, ilikuwa ni kutaka watu waelimike ili huko mbele ya safari waweze kuwa na uwezo wa kutafakari wenyewe na kuamua mustakabali wa nchi yao. Leo hii, pamoja na elimu bado hatuoni watu wengi (ilivyokusudiwa) wanaokuja na jipya zaidi ya kujenga hoja zao kuzunguka yale yale yaliyoanzishwa na Mwalimu kwa kuunga mkono ama kuyapinga!

Mwaka 1968, tutakumbuka, walichomoza wabunge kadhaa waliotaka kufurukuta na kuihoji TANU ndani ya Bunge la chama kimoja. Alichofanya Nyerere ni ‘kuwashitaki’ wabunge hao (Kaneno, Bakampenja, Choga, Masha, Anangisye, Mwakitwange) ndani ya vikao vya chama. Wakanyang’anywa uwanachama wa TANU, na hivyo wakapoteza ubunge.

Pengine Mwalimu alifanya makosa katika baadhi ya hatua alizochukua. Lakini, katika kuwashughulikia hao wanaodaiwa kufurukuta kuhoji, kama aliwapeleka ama aliwashitaki kwenye vikao vya Chama ikadhihirika ndani ya kikao kwamba wana makosa, wakahukumiwa na vikao hivyo, kosa la Mwalimu ni lipi?

Niliwahi kusikia kwamba Jenerali Ulimwengu alikuwa mmoja wa Wabunge G… waliokuwa wanataka Tanganyika wakati ule. Inasemekana walikwenda Msasani kwa Mwalimu kuelezea greaviences zao zilizowafanya watake/kudai Tanganyika yao! Je, katika mkutano wao na Mwalimu hawakuwa na majadiliano naye, aliwaburuza tu wasomi wazima? Nasikia aliwashinda kwa kuwaambia jambo jepesi sana, Jenerali anaweza kutuambia kama ni kweli ama la. Eti Mwalimu aliwaambia nyinyi ni Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba, kama mwataka Tanganyika yenu basi vueni kwanza huo Ubunge wa Jamuhuri ya Tanzania ndipo mdai Tanganyika! Sijui kama walifanya hivyo.

Hakika ilianza kusadikika kwamba ukipata laana ya Kambarage ujue umemalizika kisiasa, imani ambayo imezidi kujengeka katika miaka ya karibuni.

Watu ambao walidhani wanaweza kumshinda Mwalimu kwa hoja, walipoona kila wakijaribu anawaweka mahali wakajiona hoja zao hazina uzito, ndio hao wanaoeneza uvumi kwamba Mwalimu alikuwa akitoa laana za kisiasa! Walikuwa wakijimaliza wenyewe. Sisi hao hao tunaodai kwamba Mwalimu alikuwa akimaliza watu kisiasa, wakati mwingine tunamsifu kwamba alikuwa anaona mbali! Muona karibu ukipeleka hoja zako zenye mwelekeo wa kuangalia mambo ya karibu karibu tuuu lazima zitapwaya tu mbele ya hoja za muona mbali. Ukweli ndio huo!

Tukubaliane kwamba Mwalimu alikuwa binadamu na aliweza kukosea kama binadamu mwingine yeyote. Lakini, mengi aliyobuni Mwalimu, akafanya na kuyasimamia yalikuwa na mantiki sana na kwa kuwa alikuwa anaelewa kwamba analolisimamia na kulivalia njuga lilikuwa na manufaa kwa Taifa alilokuwa analiongoza, hoja za kumtaka awaze vinginevyo alikuwa hazikubali kwa sababu alikuwa anaona mbali na alikuwa anajua analofanya ni kwa nia njema na lengo zuri.

Utamaduni ulioanzishwa wakati wa Nyerere umeendelea ndani ya chama-tawala kiasi kwamba majadiliano ni nadra sana, na mara nyingi mijadala huzuka ili kumshughulikia mtu fulani, na wala si kusaili hoja wala falsafa. Athari mojawapo ya utamaduni huo ni kwamba hivi sasa, Nyerere akiwa hayupo, hakuna kiongozi hata mmoja, hata wale waliokuwa safu ya mbele kabisa katika kuhubiri Ujamaa leo hii huwezi kuwatambua.
Tatizo hapa si utamaduni ulioanzishwa na Mwalimu bali ni ubinafsi na unafiki wa viongozi wengi waliojiingiza kwenye siasa. Baadhi ya viongozi walikuwa wakiimba wimbo wa Ujamaa wakati roho zao zikitamani ubepari. Kwa hali hiyo walikuwa waoga hata kuujadili Ujamaa wenyewe!

Hali hii ilianza kujitokeza hata wakati Mwalimu akiwa madarakani. Kadri umri ulivyoongezeka na nguvu za mwili kupungua ndivyo kasi ya kusimamia sera na utekelezaji wake ilivyoendelea kupungua, kiasi kwamba chama na sera zake vilianza kuonyesha uzee kadri nywele za Mwalimu zilizvyozidi kuwa nyeupe.

Hii ni kejeli isiyo ya lazima. Mwalimu alikuwa na dhamira ya kuacha uongozi tangu miaka ya ’70 zaidi ya miaka 10 kabla ya kung’atuka mwaka 1985. Aliamini kwa dhati kabisa kwamba walikuwepo watu ambao wametajwa humu na baadhi ya wachangiaji, watu kama Marehemu Sokoine, Marehemu Mzee Bomani, Mzee Malecela, Mzee Job Lusinde, Dr. Salim Ahmed Salim, Judge Sinde Warioba, Mzee Cleopa Msuya na wengine ambao hadi leo hii bado mishipa ya miili yao imejaa damu ya Ujamaa na roho zao zimejaa uzalendo usiotetereka kwa Taifa letu. Mwalimu aliwaelewa hivyo na aliwathamini sana. Hawa kwa namna moja ama nyingine wangeliweza kuendeleza kwa dhati kabisa ‘Ujamaa na Kujitegemea’ kama ulivyoasisiwa na Mwalimu, kwa staili zao wenyewe na kwenda na wakati lakini kwa lengo lile lile! Miongoni mwa hao niliowataja yumo ambaye alikuwa ndilo chaguo haswa la Mwalimu kwa urais wa mwaka 1995, kiongozi huyo alimkatalia Mwalimu kwa sababu zake wakati huo. Mwalimu alisikitika lakini aliheshimu maamuzi ya kiongozi huyo. ‘Rafiki’ yake Jenerali alikuwa ni second choice na yupo mtu aliyempigia debe kwa Mwalimu ambaye hata siku moja hajatajwa popote! Wapo wanaoamini kwamba ‘rafikiye’ Jenerali alidhani anaweza kuwa na mawazo mbadala ya kuendeleza Taifa nje ya misingi aliyoiweka Mwalimu. Matokeo tumeyaona.

Katika hali ya kutokuwapo na mjadala, sera zilizolenga kumkomboa Mtanzania zikaishia kumletea matatizo ambayo yaliupa Ujamaa jina baya. Serikali ikajiingiza katika biashara isiyokuwa yake – kuuza nyama na chumvi; vyama vya ushirika vikavunjwa; serikali za mitaa zikafutwa, na kadhalika.
Maandishi kama haya hayamtendei haki Mwalimu. Mara ngapi Mwalimu alikuwa akienda Chuo Kikuu kujadiliana na wasomi kuhusu mustakabali wa nchi? Mlango wa Msasani ulikuwa wazi wakati wote lakini watu kwa woga wao wakawa hawathubutu kuomba kuonana na Mwalimu ili watoe mawazo yao. Wengine wakawa wanasingizia kwamba Butiku alikuwa akiwazuia kumuona Mwalimu! Wachache waliokuwa wakijiamini, Mwalimu alikuwa akiwasikiliza kwa makini sana. Mwalimu alikuwa akiwasikiliza wazee kwa vijana, hata wahudumu, wapishi, madobi, madreva n.k. na kufanyia kazi aliyoyapata kutoka kwao, sembuse viongozi wenziwe?

Hivi ni kweli Mwalimu alikuwa akilizuia Bunge la chama kimoja kujadiliana juuya namna ya kuboresha ama kushughulikia matatizo ya ki-sera zilizolenga kumkomboa Mtanzania mpaka sera hizo zinakufa etc etc? Viongozi wa mashirika na wananchi waliopewa na Serikali majukumu ya kuuza “nyama na chumvi” wangelikuwa ni watendaji wazalendo wenye uchungu wa dhati ya maendeleo ya nchi yao, mashirika yote yakaendeshwa kwa ufanisi uliodhamiriwa, leo hii Tanzania tungelikuwa wapi? Mameneja wangapi walijenga nyumba na kufuja fedha za mashirika, kufanya ubadhilifu wa kila aina kwa kutumia nafasi za uongozi walizopewa? Kama Wachina wameweza kujipatia maendeleo ya kiuchumi haraka, sisi ambao tunaambiwa kiongozi wetu alikuwa akiwaiga wao na kusikiliza kila alilosema, ilikuwaje na tulishindwaje kuwa kama Wachina?

Ushauri toka kwenye masufuria jikoni: Hatujachelewa. Tutafute njia za kisasa tuwarudishe vijana ‘kambini’, tuwafunze uzalendo wa kupenda na kujali nchi yao kuliko jambo lingine lolote. Sie wazee tukae tucheze na wajukuu zetu na kutoa mawazo ya kukumbushana tulikotoka badala ya kudhani kwamba leo hii tutaweza kufanya yale tuliyoshindwa huko nyuma kwa visingizio kwamba Mwalimu (aliyekuwa na uchungu na nchi yake toka rohoni) alikuwa hawapendi ama alikuwa na nia mbaya na wale wote waliokuwa na hoja zao nyepesi na wenye kuona karibu!
Mchungaji Kishoka, ukoko upo tu. Siku ukija nyumbani nitafute kama nitakuwa bado hai tutajikumbusha ya Ferry na Bunge!
 
I understand kuwa baba yake kijana aliwahi kuwa kiongozi wa TANU Youth League, ninakumbuka mara kwa mara nikiwa mdogo sana kwenda kumtembelea jela, yaani Magereza Ukonga, ninakumbuka vizuri sana kuwa kila tulipokwenda kumuona, alikuwa kila akiletwa akizungumza na wakulu niliokwenda nao kwa kuchuchumaaa, I never understood why? Na sikuweza kuuliza sababu au hata kwa nini alikuwa under that situation,

Lakini years later nikiwa a grown up tayari, niliwahi kwenda kule Magereza Ukonga kumuona mshikaji wangu, aliyekuwa deported kutoka majuu, sijui siku hizi enzi zile ukiwa kwenye hiyo situation ilikuwa ni lazima ule kama three to six months Ukonga, unless una familia ya kibopa wanakuwahi Airport, na kwa bahati mbaya patner wangu hakuwa kwa hiyo akasota siku nilipokwenda kumuona, nilipata bahati ya kuingia na kula a min tour mle ndani, mpaka sehemu za wakulu wanapolala na the rest of the place,

I mean, sidhani kama kuna dhambi kama ya kumpeleka bina-adam mwenzako sehemu kama ile bila makosa ya kweli, na kwa mara ya kwanza nikapata ukweli wa kwa nini wafungwa wanapo ongea na askari au raia kutoka nje wanachuchumaaa, haruhusiwi kusimama kumbe ni sheria ya mle ndani, that was wasup ilikuwa Jumapili inmates hucheza sana mpira siku hiyo, na kulikuwa na mpira mkubwa sana on the day,

Now my point is kama kweli makosa ambayo to this day sina uhakika nayo sana aliyoyafanya baba wa huyu bwana mdogo, yalikuwa warranted kumpelekea kwenye yale maisha, kwa sababu kama hayakuwa basi Mwalimu was a leader with two faces, I hope he was damn right on this one!
 
Hebu substantiate hicho kitu, vinginevyo utaambiwa acha udaku we bibi wewe!

Kwa nini hao wachache walifungwa, kufukuzwa kazi, kufungiwa vijijini au kwenye vyumba vya giza?

Acha kupotosha. J.K. Nyerere angekataa kuimbiwa nyimbo za kusujudu watu wangeacha. Mkapa alikataa kuitwa "Mtukufu." Na watu wakakoma! Anashindwa hata na Mkapa? What a vain demigod!

Na ndio hicho tunachojaribu kuonyesha hapa. Sasa unachobisha hasa hasa ni nini sasa?

Umeshawahi kusikia kitu kinaitwa mahakama za Kangaroo ? Jaji, wakili, prosecutor, wazee wa baraza, court reporters na polisi wa Jaji wote lao moja. Don't be naive.

Umesikia kwa nani, Butiku au Mkapa ? Au Mzee Bomani ? Umesikia ? Watu tunapambana na uongo uongo uliohubiriwa miaka 47 wewe unakuja na michongo ya "nimesikia!"

Ni ukweli kwako, ulioutengeneza mwenyewe. Eti J.K. Nyerere aliona mbali. Na, hoja za nani zilishinda mwishoni, kina Kambona au Nyerere ? Mchangiaji asiyejua kitu kuhusu historia!

Hakuna anae debate ubinadamu wa binadamu hapa. Niambie nisichokijua, sio habari za huyu binadamu alikuwa binadamu. Tunachambua binadamu hapa, kama ulikuwa hujui.

Naive, sijapata kuona.

Unamaanisha majadiliano kwa viboko ?

Maofisa wa serikali hawatakiwi kwenda nyumbani kwa Rais kujikomba komba undugu. Wanaongea rasmi bungeni, cabinet meetings, vikao vya chama, na kupitia official and expert recommendation kwenye makaratasi. Sio "kuomba kuonana Msasani... kusikilizwa kwa makini." Nakwambia wewe ni ludicrously naive sijapata ona.

Madobi na wapishi! Angalia hivi vi komedi vyako. Yani unajipiga risasi mguuni kwa kuonyesha kwamba Nyerere alikuwa comfortable kujadili siasa na wahudumu na madereva. J.K. Nyerere mwenyewe angesikia unasema hivyo angekuruka. Unatia huruma!

Ala, kumbe na wewe hujajui haya! Sasa watuhubiria nini ? Mwalimu alizuia majadiliano yaliyokuwa hayapigi muhuri sera zake. Hicho ndilo tatizo hapa, sio hilo ulilolisema wewe.

Hatuongelei ubaya na ufisadi wa mameneja wa era ya Nyerere hapa. Kuna sababu nyingi zilizosababisha Ukimwi wa Uchumi wakati wa era ya J.K. Nyerere. Rushwa ya viongozi ni moja wapo ya hizo ngono za Uchumi. Lakini hapa, bibi, tunaongelea sehemu ya J.K. Nyerere, dalali na pimpu wa hiyo biashara ya Ujamaa iliyofunga jela waliokataa kushiriki ufuska na mawazo wasiyokubaliana nayo.

Kwani ujamaa ndio umeleta maendelea China ? Tafiti kwanza. Sio kujiandikia tu yaliyo kichwani mwako!

Ndugu yangu Kuhani,

Hivi Bibi Ntilie kakukosea nini mpaka unamjibu kwa kejeli, dharau, ghadhabu na hasira namna hii?

Ningekuelewa ungeweka gadhabu zako kwangu, Jasusu, Mwanakijiji hata FMES. Lakini huyu Mama? Kakukosea nini? Je Bibi Ntilie kumpa wasifu Nyerere ni kosa mpaka umkosee adabu kiasi hicho?
 
Ndugu yangu Kuhani,

Hivi Bibi Ntilie kakukosea nini mpaka unamjibu kwa kejeli, dharau, ghadhabu na hasira namna hii?

Ningekuelewa ungeweka gadhabu zako kwangu, Jasusu, Mwanakijiji hata FMES. Lakini huyu Mama? Kakukosea nini? Je Bibi Ntilie kumpa wasifu Nyerere ni kosa mpaka umkosee adabu kiasi hicho?

Sawa. Ngoja nikafute.

Bibi Ntilie samahani, Rev. Kishoka samahani, na wote waliotegemea uungwana zaidi ya huo.
 
Hamsini zako zimefika.

Mkuu, heshima mbele.

Hapana sikukutumia wewe, you can keep it maana sihitaji, not from you mtu usiyekua na heshima wala adabu hata na kina mama watu wazima umri wa mama zetu, ndio maana watu wanakimbia hapa siku hizi,

No thanx, keep your heshima sizihitaji, kama ni hii habari nimeitoa longtime ago nenda nyuma kwenye topic za Mwalimu utazikuta, keep your heshima shihitaji kabisaa!
 
Ushauri toka kwenye masufuria jikoni: Hatujachelewa. Tutafute njia za kisasa tuwarudishe vijana ‘kambini’, tuwafunze uzalendo wa kupenda na kujali nchi yao kuliko jambo lingine lolote. Sie wazee tukae tucheze na wajukuu zetu na kutoa mawazo ya kukumbushana tulikotoka badala ya kudhani kwamba leo hii tutaweza kufanya yale tuliyoshindwa huko nyuma kwa visingizio kwamba Mwalimu (aliyekuwa na uchungu na nchi yake toka rohoni) alikuwa hawapendi ama alikuwa na nia mbaya na wale wote waliokuwa na hoja zao nyepesi na wenye kuona karibu!
Mchungaji Kishoka, ukoko upo tu. Siku ukija nyumbani nitafute kama nitakuwa bado hai tutajikumbusha ya Ferry na Bunge!

Bibi Ntilie, heshima mbele sana na ubarikiwe sana, maana maneno ni mazito sana na coming from you, hakuna ubishi wala mikwaruzo, ila heshima tupu.
 
Ndugu yangu Kuhani,

Hivi Bibi Ntilie kakukosea nini mpaka unamjibu kwa kejeli, dharau, ghadhabu na hasira namna hii?

Ningekuelewa ungeweka gadhabu zako kwangu, Jasusu, Mwanakijiji hata FMES. Lakini huyu Mama? Kakukosea nini? Je Bibi Ntilie kumpa wasifu Nyerere ni kosa mpaka umkosee adabu kiasi hicho?

Mkuu Kishoka pole sana, unajua kwenye msafara wa mamba, na unajua sana kua kwenye demokrasia tunahitaji sana kuwa na uvumilivu wa hali ya juu kwa sababu tumetoka mbali sana na this game.
 
Hili chapisho langu niliwahi kulieleza kwenye thread moja hapa JF, kwa wale waliokwisha isoma, watanisamehe kwa kurudia tena. Japokuwa nimeibadirisha kidogo ili iendane na maudhuwi ya hapa jamvini.


Nakumbuka kipindi kile cha watawala wa kigeni (mkoloni), Tanganyika ilikuwa na utawala wa majimbo. Na ndipo tulipo shuhudia Mashirika ya umma (Strong cooperative movements) ya kikweli yakijitahidi na kuleta maendeleo kwa wanachama wake na kwa mkoa husika.

Cooperative movement zilianza miaka ya 1925, wakati huo kule Kilimanjaro kulikuwa na Kilimanjaro Native Planters’ Association (KNPA) amabyo ilisajiriwa mwaka 1933, na ilimilikiwa na wananchi wa mkoa husika. Baadae ikaja (KNCU). Kule kusini kwa ndugu zangu wa kusini, kulikuwa chama kilicho julikana kwa jina la Ngoni-Matengo Cooperative, kilicho pata usajiri Songea mwaka 1936.

Nakumbuka mpaka utaalam wa mbegu bora ulikuwa umepiga hatua kubwa sana kipindi hicho ambacho inasemekana uchumi wa Tanganyika na ule wa Korea (sikumbuki kama ni kusini au kaskazini), ulikuwa sawa. Ajabu leo wametuacha miaka zaidi ya 100 na zaidi.

Nikifumba macho nakumbuka mbegu zilizopewa majina ya Serena, Lulu na Sandala, hizi ni mbegu za Mtama. Na kwenye mahindi tulikuwa na Katumbili na Mwezi Mmoja... nk.

Ila mambo yalikuja kubadilika pale Nyerere alipoona kuwa baadhi ya majimbo yanapata maendeleo makubwa kiuchumi kuliko mengine. Na akahofia sana majimbo ya kule kusini (i.e Ruvuma) kuwa huwenda wakajitenga na kujiunga na Malawi. Jambo ili ndo lililo pelekea kuundwa kwa mashirika mengine yaliyopelekea yale yaliokuwa na nguvu wakati huo, kufa na kusababisha maendeleo ya mikoa kurudi nyuma. Mnakumbuka RTC?

Msumari wa mwisho ni pale walipo amua kutaifisha mashamba na viwanda kwenye lile azimio la unyang'anyi lililo pewa jina la Azimio La Arusha.

Wakubwa (Nchi za ulaya), waliofirisiwa mali zao nao wakatuwekea mtima nyongo kwenye soko la kimataifa. Pamba, Mkonge Chai na mazao yote ya biashara yakapigwa chini kiahina. Japokuwa Nyerere kwa kiburi kikubwa aliwaambia hao tulio waita mabepari na makabaila shamba..., kuwa waje tena Tanganyika baada ya mika kumi (10??). Waje ona maendeleo tutakayokuwa tumepiga...(!?)

Leo hii Chama tawala na serikali yake hawaoni haya wala aibu mabaya waliyo yafanyia raiya wa nchi hii.

Nyerere huyu huyu ndiye aliye walazimisha watu waende kwenye vijiji vya ujamaa, visivyo tayarishwa na visivyo faa kuishi wanadamu. Je Hamkumbuki Gezaulole, Kigugumo na Mwanadilatu (kama sikosei).

Je hamkumbuki mauwaji ya watu wasio na hatia kule Shinyanga? Mauwaji yaliofanywa na polisi ambao kisheria wapo chini ya wizara ya mambo ya ndani. Na kipindi kile (1977, kama sikosei). Waziri wa mambo ya ndani alikuwa Mwinyi. Ambaye alikuwa chini ya Rais wa Jamhuri. Mwinyi kwa ujasiri mkubwa akatangaza kujiudhuru uwaziri. Akapelekwa Misri kuwa barozi.

Miaka ile ya 1970 mwishoni Nyerere kwa kutumia uswahiba wake na Obette akapeleka majeshi na kuivamia nchi huru, nchi ya Uganda. Tukaviita vita vile vya Kagera vita vya kumng'oa Nduli. Ndugu na jamaa zetu wengi wakapoteza maisha, na waliobaki wengi walirudi vilema, na matatizo ya sononi (Akili). Na waliobaki wakapewa ahsante ya mdomo na kuwasifia kuwa eti mashujaa.

Nchi ikaingizwa kwenye umaskini na madeni makubwa. Tukaambiwa wananchi tufunge mikanda miezi kumi na minane, matokeo yake imepita miaka zaidi ya kumi na minane uchumi wetu umepata mtindio wa kuto kukua. Baadhi ya raiya wema walio amuwa kuleta mali toka nchi jirani (Nakumbuka bidhaa za kutoka Namanga) na ughaibuni. Wakazushiwa kuwa ni Waujumu Uchumi. Ikazushwa mbinu nyingine ya kuwanyang'anya raiya mali zao kwa kisingizio cha uhujumu uchumi. Nchi ikapiga hatua za miaka ishirini nyuma kuelekea kwenye umasikini.

Nyerere baada ya kukoswa koswa kupinduliwa zaidi ya mara 19, akaamuwa kung'atuka kwa kuona nchi imemshinda na haipigi maendeleo, kwa siasa zake mbovu. Nakumbuka kuna wakati ilikuwa ukipita njiani na askari wa JKT (si polisi) wakikuona umekamata japo boksi tupu ya dawa ya meno au ile sabuni ya lifebouy, basi ujuwe utaangushiwa kipigo cha mbwa mwizi eti nawe muujumu uchumi. Tukaishia kufulia sabuni za mchubuo.

Mwinyi alikabidhiwa nchi ikiwa haina kitu. Hapo ndipo ilipo onekana kuwa bora wale wenye huwezo wa kuleta mali na bidhaa mbali mbali waruhusiwe na kupunguziwa kodi, ili wananchi wapate afueni. Japokuwa Nyerere hakupenda wananchi wapate unafuu wa maisha, lakini hakuwa tena na uwezo wa kuwakataza.

Rais Mwinyi kati ya hotuba yake moja aliwahi kutuuliza raiya kama tupo tayari kuona bidhaa zikimiminika madukani hata kama hatuna pesa. "Tukajibu tupo tayari babaaaa...!" Baada ya hapo ndipo wananchi tukashuhudia bidhaa zikimwagika madukani na maduka ya kaya yakaanza kupotea kidogo kidogo. Tukaanza kusahau kufukuzia magali ya ugawaji (kwa wakazi wa DSM).

Waswahili tunasema, ukijikwaa usiangalie ulipo dondokea, angalia pale ulipo jikwaa. Ili kesho usijikwae tena...!

Ila Watanzania tunaangalia, tulipo dondokea na sipotulipo jikwaa.


Habari ndo hiyo....! Naomba kuwakilisha hoja...!
 
Zakumi,

Hakuna ambaye amesema kuwa Nyerere hakufanya makosa! Hata yeye mwenyewe alikiri hilo!

Sasa naomba niuulize, tukufanye wewe ni Rais wetu wa kwanza na ndio tumepata Uhuru, nchi ni changa, elimu na afya ni finyu na haba na hauna watu mahiri wa kutosha. Zaidi unabeba mzigo ulioachiwa na mtawala.

What would have Zakumi done? Tupe basi Manifesto yako ya ni jinsi gai ambavyo tungejenga Taifa letu na kuachana na utegemezi wa misaada.

Rev:

Nisingetumia manifesto ya aina yoyote hile. Ningejaribu kutengeneza models ambazo zingetumia local resources na kujali wenyeji katika maeneo yao.

Kama wachagga walikuwa na mashamba binafsi na waliweza kujenga shule zao basi kulikuwa hakuna sababu ya wao kuwepo kwenye mpango wa UPE.

Vilevile pamoja na kuwa nchi yenyewe ni changa, kitu cha kwanza ni lazima kiwe cha kwanza.

Hivyo miaka ya mwanzo, mipango ingelenga kwenye kujitosheleza kwa chakula na elimu ya kuwafanya watu wawe wazalishaji wazuri wa mazao ya chakula na biashara. Vitu hivi haviiitaji rocket scientists na resource zilizokuwepo wakati tunapata uhuru zingeweza kutusukuma.
 
Rev:

Nisingetumia manifesto ya aina yoyote hile. Ningejaribu kutengeneza models ambazo zingetumia local resources na kujali wenyeji katika maeneo yao.

Kama wachagga walikuwa na mashamba binafsi na waliweza kujenga shule zao basi kulikuwa hakuna sababu ya wao kuwepo kwenye mpango wa UPE.

Vilevile pamoja na kuwa nchi yenyewe ni changa, kitu cha kwanza ni lazima kiwe cha kwanza.

Hivyo miaka ya mwanzo, mipango ingelenga kwenye kujitosheleza kwa chakula na elimu ya kuwafanya watu wawe wazalishaji wazuri wa mazao ya chakula na biashara. Vitu hivi haviiitaji rocket scientists na resource zilizokuwepo wakati tunapata uhuru zingeweza kutusukuma.

Zakumi,
Hindsight is always 20/20. You can afford to say that now from the comforts of hindsight.
 
Back
Top Bottom