WildCard said:Someni yote aliyoyaandika Mwalimu; sikilizeni hotuba zake zinazoendelea kurushwa na redio yetu ya Taifa; mtagundua kwamba akili na mawazo ya Mwalimu vilikuwa vya kwake mwenyewe na aliweza kuyasimamia vizuri yale yote aliyoyaona ni sahihi na ya MSINGI kwa TAIFA letu.Angalieni mifano hapa kwa majirani zetu tu. Mtu anakuwa maarufu kwa sababu ya KABILA yake, DINI yake, UTAJIRI wake,... Rais anahutubia watu wake kupitia wakalimani...
WildCard,
..tumeishi wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. we have first hand experience ya matokeo ya utekelezaji wa mawazo yake.
..halafu wakati wa harakati za kupigania Uhuru, Mwalimu alilazimika kutumia mkalimani ktk mikutano ya hadhara mara mbili. ilitokea ktk maeneo ya mwanza na mbulu.
..sasa utaona kwamba hata wakati wa mkoloni Mwingereza Kiswahili kilikuwa kimesambaa maeneo mengi mno. ukweli huo unapingana na ile dhana kwamba Mwalimu Nyerere ndiye aliyekikuza kiswahili Tanzania.