Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Hivi China na wao bado ni Wakomunisti (Wajamaa) au na wao wamedonyoa kidogo kutoka kwenye ubepari?
 
Hivi China na wao bado ni Wakomunisti (Wajamaa) au na wao wamedonyoa kidogo kutoka kwenye ubepari?

Nyani Ngabu,

Kila mfumo unakwenda mbele na kurudi nyuma huku ukijifanyia marekebisho. Wachina bado wanaendesha siasa zao Kikomunisti lakini uchumi wao umepanuka kwa kutumia misingi ya soko huria na Ubepari lakini likidhibitiwa na Siasa za ukomunisti.

Sasa wao na regulation zao wanaonekana kuwa ni ma-survivor wa msukosuko wa uchumi wa dunia.

Unakumbuka betwen 1997-2002, uchumi wa Asian Tigers ulitetereka huku Singapore, Japan, Malaysia, Taiwan, South Korea, Thailand na Vietnam walitetereka vibaya hata India, huku China uchumi ukikuwa kwa karibu 9%+!
Hata wakati Europe ilikuwa inachechemea China kwa miaka 10 imeendelea kujijenga na bila kutetereka na sasa kila mtu anahaha kufanya biashara nao!

Hivyo usishangae kuwa pamoja na hali ya kisiasa ambayo tunaambiwa si nzuri na dhuluma kwa haki za binaadamu, China inaendelea kupeta kiuchumi huku ikiwekeza katika uchumi wa Marekani.

Sasa walichofanikiwa China pamoja na ubabe wa Ukomunisti ni kuendelea kulijenga Taifa lao lenye umri mkubwa tangu wakati wa Ming Dynasty. Wananchi wao wamelazimika kufuata muongozo wa viongozi wao na kulijenga upya Taifa lao.

Mwezi mmoja uliopita, kwenye gazeti la Times kulikuwa na article inayozungumzia Wachina ambao wamepata nafasi kusoma katika nchi za magharibi na hawakushawishika kuikimbia nchi yao au kulia ukimbizi wa kisiasa au haki za binadamu, bali wamerudi China kuijenga na kuilinda nchi yao.

Tofauti ya Wachina na sisi ni kuwa kwa kiasi fulani pamoja na kuwa Serikali yao ni ya kibabe, inawazikiliza na kuwashirikisha Wananchi wake katika maendeleo mapya.

Deng Xiao Ping ndiye alikuwa mwanamapinduzi wa kuleta mfumo mpya wa uchumi China baada ya Mao Tse Tung kufa na kumng'oa Huo Guo Feng na lile kundi la Gang of Four ambao walikuwa ni sasa na Kingunge weyu na wenzake !

Sisi Serikali yetu inatutenga na kukataa mawazo yetu.

Tunajaribu kuishauri na kuisukuma Serikali na Wanasiasa wetu kuwa wepesi wa kuleta mukumo wa Maendeleo lakini tunaonekana kuwa tunawaingilia kazi au hatuji tunalolisema.

Leo hii natamani sana kama Nyerere angekuwa hai na walio karibu nae wamdondoshee nyeti kuwa kuna hiki kijiwe, ungeona vumbi likitimka ndani ya CCM!
 
Mchungaji Kishoka,

Nilipotea kidogo mapishi yalikuwa mengi!

Katika kujadili juu ya “Who influenced Nyerere on his Ujamaa Philosophy and Azimio Principles”, mbali ya kuliangalia suala zima ‘kisomi’ na kuona labda aliiga kwa wasomi gani ama nchi gani, yatupasa pia tuangalie historia ya maisha yake tangu kuzaliwa.

Mwalimu Nyerere alizaliwa kwenye familia kubwa ya Chief Burito aliyekuwa na wake 13 na watoto kibao. Ujamaa ulianzia hapo. Alijifunza misingi ya ‘ujamaa’ wa mwafrika wa wakati huo – kushirikiana katika kazi za kila siku, kuchunga na vijana wenziwe, kulima na hatimaye mavuno ya pamoja, kula nako kwa pamoja na nduguze na mgeni yeyote aliyefika kwenye compound ya Chief Burito.

Ujamaa ni Utu na ni imani inayopaswa kujengeka kwenye nyoyo za watu wasio na ubinafsi. Katika mazingira aliyokulia Mwalimu Nyerere ubinafsi haukuwa na nafasi sana. Na Nyerere alipoenda Tabora School, ‘ujamaa’ wake kwa maana ya kuwa radhi kugawana kidogo alichonacho na wenziwe ulijidhihirisha. Yasemekana, ingawa alikuwa akienda shule na fedha kidogo sana za matumizi, siku zote alikuwa tayari kuzitoa zote kuwasaidia wanafunzi waliokuwa na shida.

Msimamo wake wa kutetea kwa nguvu zote kile alichoamini pia ulianza kujengeka mapema akiwa kijana. Alipokuwa shuleni Tabora Mwalimu alionyesha tabia ya kupenda kutetea haki na usawa (nguzo moja ya Ujamaa) za wanafunzi. Alikuwa na ujasiri wa kukabiliana viongozi ma-Kaka pale alipoona mwanafunzi anaonewa. Wakati mmoja alienda hadi kwa Mwalimu Mkuu kujaribu kumtetea mwanafunzi aliyedhalilishwa na Kaka wa bweni kwa kupewa adhabu ya kufungwa kamba miguu na mikono. Hata hivyo, Mwalimu Mkuu alitoa uamuzi wa kumpendelea Kaka, akamwamuru Nyerere amchape fimbo yule mwanafunzi aliyekuwa akimtetea!

Mwishowe, Walimu waliona njia ya kufanya aache kutetea wengine ni kumteua naye awe Kaka. Lakini, haikuwa dawa. Pamoja na kuwa Kaka, aliwashawishi wanafunzi waugomee mtindo uliokuwepo shuleni hapo wa ma-Kaka kujigawia chakula kingi kuliko wanafunzi wengine. Walimu walipofanya uchunguzi, walishangaa kugundua kwamba Kambarage ndiye alikuwa chanzo cha mgomo!

Hata ujasiri wake wa kukabiliana na “Tembo” katika kutetea kile alichokiamini aliudhihirisha wakati huo akiwa shule. Siku moja kulikuwa na majadiliano yaliyofanyika mbele ya Mwalimu Mkuu yaliyohusu “Je, Tanganyika iendelee kuwa chini ya utawala wa Waingereza?” Nyerere, bila woga wowote alipinga kwa nguvu hoja ile na kuelezea waziwazi uovu mwingi uliokuwa ukifanywa na Serikali ya Uingereza katika kuitawala nchi kwa mabavu na kwa misingi ya ubaguzi wa rangi. Mashambulizi aliyoyatoa dhidi ya Serikali yalimfanya Mwalimu Mkuu (Mwingereza) ahamaki kusikia Serikali yake ikishambuliwa na mwanafunzi! Akajaribu kumnyamazisha, kwa kumwamuru akae chini asiendelee kuzungumza. Nyerere hakukubali kunyamazishwa, aliendelea kuzungumza. Mwalimu Mkuu alipozidi kumlazimisha aache kuzungumza, Nyerere alitoka kwenye ukumbi kwa hasira na kwenda bwenini kubeba sanduku lake arudi kwao Butiama! Ilibidi Mwalimu Mkuu atume watu kumshawishi asiondoke. Alibaki shuleni, lakini akawa amekwisha kudhihirisha msimamo wake katika kutetea kile alichokiamini.

Kwa hiyo, mwaka 1943 akiwa Makerere College, akishirikiana na wanafunzi wenziwe kutoka Tanganyika, walipoanzisha chama chao walichokiita Tanganyika Welfare Association, Mwalimu Nyerere tayari alishakuwa amepanga akilini mwake ni nchi ya aina gani ambayo angelipenda Tanganyika iwe. Ramani ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea alikwishaichora kichwani mwake tangu wakati huo. Siasa za Chama cha Labour cha Uingereza, na Ujamaa wa China, ama Mama Joan Wicken m-Socialist wa Labour Party kuwa msaidizi wake wa maisha, vilikuwa ni vibwagizo tu vilivyomsaidia kuimarisha fikara zake katika kuumba Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ya TANU na kubuni Azimio la Arusha ambalo basically lilihusu ujenzi wa uchumi wa nchi maskini, pamoja na miiko ya uongozi, ambayo iko kisheria hata kwenye mataifa makubwa ya kibepari.

Mchungaji, sie akina Bibi Ntilie huo ndio mchango wetu wa mawazo tukiwa tunatayarisha msosi wa wajukuu!
 
Bibi Ntilie, umetupa kitu muhimu sana ambacho wakati mwingine tunakikosa; kufikiria kuwa formation ya mtu inatokana na intellectual pursuits zake na ni nje ya mang'amuzi yake. Mara nyingi utaona kuwa watu kama Mwalimu, Gandhi, Mandela, Luther n.k ambao walisimama kupinga uovu hawakufanya hivyo kutokana na hoja ya kisomi (ambayo bila ya shaka walikuwa nayo) lakini ni kutokana na mang'amuzi yao kuwa uovu hauwezi kuvumiliwa au kutolewa udhuru.

Ni hii tunu ya ajabu sana ambayo inamfanya mtu kuchukua msimamo ambao kwa wengine unaweza kuonekana ni kujitafutia sifa kumbe ni kuwa hawezi kuukana ukweli ambao umeangaza kwenye akili zake.

Na ndio maana naamini kuwa tukikaa chini na kujichunguza sisi wenyewe tutajikuta tunafanya uamuzi wa kuwa katika upande mmoja au mwingine; Kama mtu amekulia katika anasa na starehe ni vigumu sana kwake kuachana na mawazo hayo ya kustahili na kuunga mkono wapambanaji. Mtoto wa tajiri akigeuka na kuwa mtetezi wa maskini watu watamuona shujaa kwa sababu hana sababu ya kufanya hivyo.

Ndio maana Musa hakueleweka alipoamua kuiacha nyumba ya Farao na kujiunga na wana Izraeli utumwani.

Hivyo mtoto wa Chifu ambaye katika misingi ya aina fulani ana kuwa na kaujiko kule kwao amepata urafiki na wamisionari n.k anapoamua kuacha raha hiyo na kutaka nchi yake iwe na uhuru wake anafanya kitu akiongozwa na kitu zaidi yeye mwenyewe.

Mchango wako japo kidogo unatupa mwanga kidogo wa kuelewa the motivation behind the man, the myth and the legend that is Mwalimu Nyerere.
 
Bibi Ntilie,

Naam umeamsha baraza na kutukumbusha malezi yetu ya nyumbani ambayo mara nyingi huwa tunayasahau kuwa yamechangia kiasi gani kujijenga kitabia na kifikra.

Ni faraja kubwa sana kwa sisi "Pro-Nyerere" kusikia hadithi za ndani na za watu wa karibu naye wakiongelea yaliyotokea si kwa maadniko na hotuba zake, bali vitendo na msimamo wake hata kabla ya kuwa kiongozi wa Taifa!

Nibakishie ukoko wajukuu wakimaliza kujichana!
 
Lusajo, haitoshi mtu kuwa na mawazo tofauti tu ili asikilizwe, ni lazima awe na hoja yenye nguvu kushinda hoja iliyopo. Yeye mwenyewe alisema hivi "mtu mwenye akili akija na kukushauri kitu cha kipumbavu akijua na wewe una akili (kwamba utakiona ni cha kipumbavu) na wewe ukakubali atakudharau".
Nikiangalia baadhi ya watoa hoja humu na watu ambao tunajadiliana nao humu na kuwaweka hao kwenye utawala wa Mwalimu na kuwaambia watoea ushauri kwa Mwalimu na wakatoa jinsi wanavyotoa humu sitoshangaa kwanini ilikuwa ni vigumu kumshauri lolote.

Na kama mawazo ya namna hii ndiyo yanayotolewa kwa Kikwete sishangai kwanini tunaona hamsikilizi mtu yeyote kwa sababu kama hoja zinatolewa au zinapangwa zinavyopangwa hapa basi tuna matatizo makubwa zaidi kuliko uongozi mbaya.

Well, ninachotaka kusema ni kuwa Nyerere hakulazimika kukubali mawazo tofauti, alitakiwa kukubali mawazo yenye hoja tofauti na kubwa kuliko hoja zake. So far, sijasikia hoja iliyowahi kutolewa na kumshawishi Mwalimu aachane na hoja yake ya awali labda mara chache sana.
Mzee Mwanakijiji au mwana-jamii yeyote anayemfahamu Mwalimu naomba mniambie kwamba nani alikuwa anamshauri katika mambo yake? kwa sababu hata kama mtu una vision lazima uwe na washauri au kama alikuwa anakwenda na vision yake peke yake. Ni kweli ilibidi watu wam-convice na waende na strong plan ya kum-convice, what if he was hard head yaani alikuwa hamsikilizi mtu? kwa sababu hata wewe unajua kuna watu huku JF ambao hata uwaambiaje hawakubaliani na wewe!. Kwa hiyo hata ukimuambia nini at the end yeye ndiye Raisi na ndio anaamua cha mwisho kwa hiyo sijui kama alikuwa anawasikiliza hao watu au hawasikilizi, na ni kina nani aliokuwa anawasikiliza.
Na haikuwa lazima Nyerere kukubaliana na mawazo ambayo yalikuwa tofauti kabisaa, ila kama alikuwa anasikiliza hata hoja za kuboresha alichokuwa anakifanya yaani Ujamaa. Mimi naona ndio maana hata na Kwame N hawakuelewana kwa sababu ilikuwa ni vigumu sana kumshauri au kumbadili mawazo kwa sababu alikuwa sio mtu wa kubadilika (yaani anachofikiri yeye ndio uamuzi wa mwisho) haya ni mawazo yangu tu.
 
Lusajo,
Hilo swali ulilomwuliza Mwanakijiji--nani alikuwa anamshauri Mwalimu, niliwahi kumwuliza marehemu Mzee Bomani. Huyu mzee walitoka mbali sana na Mwalimu Nyerere tangu siku za TANU. Aliniambia kuwa watu wengi waliogopa kutoa ushauri kwa Mwalimu kwa sababu waliogopa maswali ambayo Mwalimu angewauliza. Ilibidi ujenge hoja yako barabara kabla ya kuitoa mbele ya Mwalimu na mzee Bomani alisema kuwa watu walikuwa wavivu wa kufanya homework zao na wakaishia kusema kuwa Mwalimu haambiliki, lakini si kweli. Mzee Bomani mwenyewe kuna vitu vingi tu alivyokuwa anashauriana na Mwalimu na kusikilizwa.Ukimshawishi Mwalimu hoja yako na kujibu maswali yake basi anaweza kukubaliana na ushauri wako. A lot of people did not have the patience to defend their hojas.
 
Labda hao waliokuwa wanamshauri arguments zao za kubadilisha mawazo ya Mwalimu zilikuwa ziko weak. Kwa mfano Mwalimu alimfukuza kazi Mtei kwa kumshauri Mwalimu kufuata masharti mbali mbali ya IMF ikiwemo kushusha thamani ya shilingi yetu. Mwalimu aliona kushusha thamani ya pesa yetu kulikuwa hakuna faida yoyote kwa Watanzania. Na alitoa mifano kama ifuatayo kabla ya kushusha thamani ya shilingi tulikuwa tunanunua trekta moja kwa ajili ya kilimo kwa magunia 10 ya kahawa baada ya kushusha thamani trekta lile lile tungelinunua kwa magunia 15 ya kahawa kwa hiyo kushusha thamani ya shilingi yetu kulikuwa hakutusaidii chochote.
 
Jasusi uliyosema hapo juu yananikumbusha msimamo wa Mwanakijiji anaouonesha hapa jamvini kuhusiana na siasa zetu.... in a way wengi huwa wanamwona ni "haambiliki."
 
Lusajo,
Hilo swali ulilomwuliza Mwanakijiji--nani alikuwa anamshauri Mwalimu, niliwahi kumwuliza marehemu Mzee Bomani. Huyu mzee walitoka mbali sana na Mwalimu Nyerere tangu siku za TANU. Aliniambia kuwa watu wengi waliogopa kutoa ushauri kwa Mwalimu kwa sababu waliogopa maswali ambayo Mwalimu angewauliza. Ilibidi ujenge hoja yako barabara kabla ya kuitoa mbele ya Mwalimu na mzee Bomani alisema kuwa watu walikuwa wavivu wa kufanya homework zao na wakaishia kusema kuwa Mwalimu haambiliki, lakini si kweli. Mzee Bomani mwenyewe kuna vitu vingi tu alivyokuwa anashauriana na Mwalimu na kusikilizwa.Ukimshawishi Mwalimu hoja yako na kujibu maswali yake basi anaweza kukubaliana na ushauri wako. A lot of people did not have the patience to defend their hojas.
Asante Kaka kwa hiyo mmoja wa washauri aliowasikiliza ni Mzee Bomani.
 
Rev. Kishoka,
Asante kwa kuanzisha mjadala huu. Bibi Ntilie, asante kuonekana tena. Usiwe unapotea namna hiyo, naelewa majukumu ni mengi lakini hapa JF pia mchango wako ni lulu.
 
Jasusi uliyosema hapo juu yananikumbusha msimamo wa Mwanakijiji anaouonesha hapa jamvini kuhusiana na siasa zetu.... in a way wengi huwa wanamwona ni "haambiliki."

JF kwa vichwa bwana, ukifikiri umemaliza kuvihesabu siku zote unakumbushwa kuwa bado kabisaa, ahsante mkuu Steve Deeee! Maneno mazito sana haya!
 
Hilo swali ulilomwuliza Mwanakijiji--nani alikuwa anamshauri Mwalimu, niliwahi kumwuliza marehemu Mzee Bomani. Huyu mzee walitoka mbali sana na Mwalimu Nyerere tangu siku za TANU. Aliniambia kuwa watu wengi waliogopa kutoa ushauri kwa Mwalimu kwa sababu waliogopa maswali ambayo Mwalimu angewauliza. Ilibidi ujenge hoja yako barabara kabla ya kuitoa mbele ya Mwalimu na mzee Bomani alisema kuwa watu walikuwa wavivu wa kufanya homework zao na wakaishia kusema kuwa Mwalimu haambiliki, lakini si kweli. Mzee Bomani mwenyewe kuna vitu vingi tu alivyokuwa anashauriana na Mwalimu na kusikilizwa.Ukimshawishi Mwalimu hoja yako na kujibu maswali yake basi anaweza kukubaliana na ushauri wako. A lot of people did not have the patience to defend their hojas.

Sio kweli.

Kulikuwa kuna sababu kwa nini J.K. Nyerere alitaka tuimbe "Zidumu fikra za Mwenyekiti..." Maana yake fikra zingine hazikaribishwi.

Hadithi za kina Mzee Bomani ni historia potofu ambazo anaweza kuhadithia wasioelewa kilichojiri tu. Ukimuuliza Mzee Bomani maoni yake kuhusu Nyerere ni kumpelekea ngedere kesi ya nyani. Hawa wote ndio watendaji, "ndio-mzee," chinja-chinja wa kisiasa na kimatendo katika mkoba wa vifaa vya J.K. Nyerere.

Na, hata kusema J.K. Nyerere haambiliki ni kupendezesha lugha tu. J.K. Nyerere alikuwa nduli wa mawazo, kama sio nduli. Alitumia dola kushughulikia waliotofautiana nae (4). Aliyethubutu kubisha aidha alifungiwa kijijini ( Balozi Kassanga Tumbo (1) au jela (Chief Justice Wolfango Dourado ( 3 ), Abdallah Said Fundikira, Mwinyijuma Othuman Upindo, na James Mapalala (2), kufukuzishwa nchini (Waziri Kambona), kufukuzwa kazi (Rais Jumbe) na orodha inaendelea na kuendelea na kuendelea....(Kassim Hanga, Makamu wa Rais wa Zanzibar, na walinzi wake; Waziri Abdulrahman Mohamed Babu (5), na Wabunge Joseph Kasela Bantu na Mbunge Eli Anangisye, aliyekamatwa na kufungwa bila mashitaka baada ya kuchangia mjadala wa kikao cha Bajeti Bungeni, 1968! ( 6).

Kusema J.K. Nyerere alikuwa ana hoja kali sana kiasi kwamba hakukuwa na wengi wanaoweza kujadiliana nae ni kituko kwa sababu inamaanisha watu wote walikuwa watupu ila Nyerere na wachache fulani. Huku ni kupumbazika kulikotokana na kuleweshwa propaganda. Toka mdogo unaimbishwa nyimbo:

"Kambona, kaolewa!
Wapi? Huko Ulaya

Kambona, kaolewa!
Wapi? Huko Ulaya

Na nani ? Waingereza"

Ni lazima upumbazike. Hata mimi utotoni nilipumbazika. Kuja ukubwani nakuja kuambiwa eti Kambona alilazimika kuingia mitini kwa sababu alitofautiana mawazo ya mfumo wa kiuchumi. Hebu angalia hilo ndugu yangu. Sio nduli wa mawazo huyo J.K. Nyerere? Binadamu kweli unamfunga Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar kwa sababu ametoa hotuba kama mgeni mwalikwa kwenye mkutano wa Tanganyika Law Society kujadili kuboresha na kubadili Katiba! (3) Huyu Muasisi Marehemu J.K. Nyerere utasema kweli sio nduli wa mawazo? Eti, "ilibidi ujenge hoja barabara." Ukipumbazwa unaweza kuamini ya ajabu!

Rev. Kishoka, kama nimetoka nje ya mada ni katika kurekebisha historia inayopotoshwa hapa. Nina marafiki mababa zao wameuawa baada ya kuugulia kwenye vyumba vya giza Oysterbay Polisi baada ya kuswekwa miaka bila mashitaka. Umenikamata nishitaki, usiniweke niugue kisukari na magonjwa ya moyo kwenye chumba cha giza polisi, nikitoka nakaa kidogo nakufa!

( 1 ) The Standard (Tanganyika), 28 Sept. 1962.

( 2 ) Chris Maina Peter; A Comparative Study of the African Human and People's Rights Charter and the New Tanzanian Bill of Rights 31 (Studies in Human Rights No. 10, Consortium on Human Rights Development, University of Denver 1990).

( 3) Ahmed Rajab, Foul Play, Afr. Events, Nov. 1985, at 28.

(4) Chris Maina Peter; Incarcerating the Innocent: Preventive Detention in Tanzania; 1997 The Johns Hopkins University Press, Human Rights Quarterly 19.1 (1997) 113-135

(5 ) H.G. Mwakyembe, Issa G. Shivji; The Parliament and the Electoral Process, in The State and the Working People in Tanzania; 1986 Colin Leys, Tanganyika: The Realities of Independence, in Socialism in Tanzania 187 (East African Publishing House Political Studies 14, Lionel Cliffe & John S. Saul eds., 1972).

(6) Ludovick S Mwijage, The dark side of Nyerere's Legacy; Raymond F. Hopkins, The role of an MP, Swarthmore College
 
Rev. Kishoka,

Soma Ujamaa Vijijini Mwalimu Julius K. Nyerere. Kilitungwa 1962/63 kwahiyo ni wazi alikuwa na hayo mawazo siku nyingi kabla hata ya kutangaza Azimio la Arusha.

Pia lazima ujue movements za vijana miaka hiyo ilikuwa ni kuelekea kwenye Ujamaa.

Baadhi ya vichwa vya Labour UK walimuunga mkono Nyerere na wengine kuishia kuhamia TZ na kufanya kazi na Mwalimu muda wote akiwemo huyo mama aliyekuwa secretary wake ambaye aliacha kazi yake ya maana na kumuunga mkono Nyerere.

Binafsi naamini Mwalimu alikuwa influenced sana na Labour ya miaka ya 50/60 na akachanganya na culture za Kiafrika za kusaidiana enzi hizo.

Mhashamu Kishoka (au Kijembe)

Swali lako ni zuri sana kihistoria, ila kama alivyosema Mtaznania hapo juu, mimi nadhani kuwa Nyerere hakuwa influenced na mtu yoyote katika kuamua kuwa mjamaa zaidi ya jamii alimokulia. Baba yake alikuwa na wake takribani arobaini au zaidi, na huyu Kambarage aliyekuja kuwa baba yetu wa Taifa alikuwa mtoto ambaye hata baba yake Chifu Burito hakuwa anamfahamu kama ni mtoto wake. Nyerere alililelewa katika msingi wa ujamaa; alipata mapenzi zaidi kutoka kwa jamaa zake na akakua huku akijua kuwa maisha hayaendi bila kuwa na jamaa karibu (mama Clinton alisema kuwa it takes a village).

Kama alivyosema Mtanzania hapo juu, mawazo ya kijamaa ya Nyerere hayakuja ghafla tu na hayakutokana na desa lolote. In fact kumsahihisha Mtanzania ni kuwa Nyerere aliandika insha kuhusu ujamaa wa kiafrika wakati akiwa mwanafunzi wa Edindburgh University mwaka 1950 au 1952 hivi, yaani miaka yapata 10 kabla hajajua kuwa atakuwa mkuu wa nchi na miaka 17 kabla hajaamua kutekeleza ndoto hiyo.
 
Back
Top Bottom