WHO inatakiwa izijibu hoja za Rais Magufuli kwa umakini mkubwa. Tropical diseases kama TB, Malaria kwanini hazina chanjo na zinaua sana?

Mamabo ya maajabu kabisa. Yaani, jiwe anauliza WHO wajieleze kuwa wameshindwa na chnjo ya malaria na TB na kuna watu waku staajabisha kabisa. "eti who wajibu masuala" kabla kutuletea vaccine. huu ni mtihani kweli kweli. Huku tunakufaaaa. Zanzibar tunakufa maana kuna watu wanamuabudu Jiwe na hawshughuliki na kujikinga. Tunaambiwa tu pneumonia wakati ni korona. Pneumonia inatibiwa kwa antibiotics. Corona haina dawa. Hata ukivuta BANGI unakufa tu.
 
Viongozi wa afrika ni alinacha sana kwahiyo anataka kutuambia amekumbuka shuka wakati kumekucha
 
kwa hiyo mabeberu wanawaonea wivu upcoming superpowers kwa kuwaletea chanjo ya covid 19
Ila chanjo nyingine hawawaonei wivu....
Inahitaji uwe na akili ya mwendawazimu ili kukuelewa
 
U

Umeliweka vizuri sana. Tuna kiongozi Mkuu mropokaji. Nitamlaumu Kikwette milele kwa chuki yake dhidi ya Lowassa na kumg'ang'ania Membe hadi tukaingia kwenye huu mkenge.
Mungu aliruhusu jambo hilo kutokea ili waTZ watoke usingizini na kuchukia ujinga.
Utatawaliwa na mtu yeyote wa sisiem hata kama hana akili sawasawa hiyo ni lazima penda usipende siyo ombi.
Sisiem itatawala tanzania mpaka mwisho wa dunia
 
Wala siyo kwamba hatuwezi kutengeneza chanjo zetu na wala si kwamba hatuna akili. Tatizo kubwa ni ukoloni, na miaka ile ilikuwa ni ukoloni wa kutawala kimabavu moja kwa moja ila kwa zama hizi ni ukoloni wa kutumia mifumo. Njia za ukoloni ni tofauti ila matokeo ni yale yale. Kazi kubwa ya mkoloni ni kuhakikisha kwamba anaondoa ile hali ya kujiamini na kujithamini kwa yule anayemtawala. Kwa ukoloni wa sasa hivi mifumo kama WHO, IMF n.k inahakikisha inatengeneza mazingira uone kile unachokifanya nje ya mifumo yake hakina uhalali wala hakina matunda. Na ndicho tunachojaribu kupandikiziwa ili tuwasubiri wao, tufanye yao na tuwasikilize wao tu.

Mtu yeyote huru au nchi yoyote huru haiwezi kusubiri WHO anasema nini. Wanafanya mambo yao. Kuna mtu mmoja hapo juu kauliza eti WHO ni akina nani kama si nchi zote? Mi nimebaki kumshangaa maana wakati mifumo hii inaanzishwa baadhi ya nchi zilikuwa hata hazipo ikiwemo na nchi yetu. Sasa mifumo wajitengenezee wao, wewe upachikwe tu na kulazimishiwa halafu useme huo mfumo upo kwa interests zako? Unaweza usijitoe lakini unaweza pia kukubali uhalisia kuwa ile mifumo ilitengenezwa kulinda maslahi ya wenye nguvu. Kama kuna kifaida tunakipata kwa kuwemo WHO au IMF au whatever, kuna faida kubwa wanaipata wale wenye hisa kubwa katika mifumo hiyo.
Me sidhani kama ni sahihi sana mpaka sasahivi kulaumu athari za ukoloni au ukoloni mamboleo,, kama tunatambua ukoloni na ukoloni mambo leo basi tunajielewa kwa nini tuendelee kulaumu na kushindwa kufanya mambo yetu ikiwepo kufanya tafiti na chanjo mbalimbali? Tusipokuwa na mifumo ya elimu inayoangalia maslahi yetu hatutafika popote.China na North Korea wamefika hapo leo kwa sababu ya kutengeneza mifumo yao bora ya elimu,leo hii badala ya kuanzisha somo la historia Tanzania ambayo tayar lipo lingeongezewa baadhi ya mambo kwa maboresho lakini nguvu kubwa tungeweka kwenye science.Mfano mwanafunzi anaeweza biology na brunches zake asome kuanzia darasa la nne mpaka Chuo kikuubadala ya kumjazia mwanafunzi rundo la masomo ambayo anasoma juujuu.
Wala siyo kwamba hatuwezi kutengeneza chanjo zetu na wala si kwamba hatuna akili. Tatizo kubwa ni ukoloni, na miaka ile ilikuwa ni ukoloni wa kutawala kimabavu moja kwa moja ila kwa zama hizi ni ukoloni wa kutumia mifumo. Njia za ukoloni ni tofauti ila matokeo ni yale yale. Kazi kubwa ya mkoloni ni kuhakikisha kwamba anaondoa ile hali ya kujiamini na kujithamini kwa yule anayemtawala. Kwa ukoloni wa sasa hivi mifumo kama WHO, IMF n.k inahakikisha inatengeneza mazingira uone kile unachokifanya nje ya mifumo yake hakina uhalali wala hakina matunda. Na ndicho tunachojaribu kupandikiziwa ili tuwasubiri wao, tufanye yao na tuwasikilize wao tu.

Mtu yeyote huru au nchi yoyote huru haiwezi kusubiri WHO anasema nini. Wanafanya mambo yao. Kuna mtu mmoja hapo juu kauliza eti WHO ni akina nani kama si nchi zote? Mi nimebaki kumshangaa maana wakati mifumo hii inaanzishwa baadhi ya nchi zilikuwa hata hazipo ikiwemo na nchi yetu. Sasa mifumo wajitengenezee wao, wewe upachikwe tu na kulazimishiwa halafu useme huo mfumo upo kwa interests zako? Unaweza usijitoe lakini unaweza pia kukubali uhalisia kuwa ile mifumo ilitengenezwa kulinda maslahi ya wenye nguvu. Kama kuna kifaida tunakipata kwa kuwemo WHO au IMF au whatever, kuna faida kubwa wanaipata wale wenye hisa kubwa katika mifumo hiyo.
 
Chanjo na dawa nyingi hazitengenezwi na serikali bali makampuni binafsi. Makampuni haya yanafanya biashara na sio huduma. Kwa sababu hiyo yanajikita katika chanjo na dawa za magonjwa yanayowasumbua watu wa magharibi kwa sababu wanajua wanaweza kuwauzia na kupata faida. Magonjwa yanayosumbua nchi maskini hazipewi priority kwa sababu wanajua hazina uwezo wa kuzinunua kwa bei itakayofidia gharama za utafiti na utengenezaji. Ndio maana utafiti wa chanjo na tiba ya magonjwa kama malaria au sleeping sickness, magonjwa ambayo hayapo katika nchi za magharibi unafadhiliwa na taasisi kama za wakina Bill and Melinda Gates Foundation ambazo hazina utaalam na resources za kutosha kuwekeza katika tafiti zote zinazohitajika za maradhi yanayopatikana katika nchi zetu.

Kwa kifupi tukitaka chanjo kwenye haya magonjwa tunatakiwa tuunganishe juhudi za nchi zetu kwa kushirikiana na taasisi rafiki kufanya utafiti ili tupate chanjo. Njia nyingine ni kuongeza juhudi kuyatokomeza hayo magonjwa badala ya kutegemea chanjo. Shida ni kuwa hatuna nia za kisiasa katika suala hili na mzigo tumewatwika wakina Bill Gates.

Amandla...
 
Kuna unafiki sana kwenye hii pandenic ya corona na namna inavyoshughulikiwa na hizi taasisi za kimataifa. Mtu mwenye fikra huru atakwambia "to hell with corona na politics zake" maana ukichunguza kwa kina kuna ubinafsi na uongo uongo mwingi uliojificha nyuma ya mwamvuli wa "sayansi".

Ok, vaccine za kwanza kuhusiana na corona ni zile za China na Urusi. Ila dunia pamoja na WHO imetuaminisha kwamba zile hazipaswi kupewa air time mpaka tusubiri za Ulaya na Marekani. Magu akitilia mashaka hizi motives anakuwa amekosea?

Haya, wakati wa maelekezo ya kupambana na corona - social distancing, kuvaa mask, bla bla... - WHO walikuwa wanasifia nchi flani flani za kiafrika zilizokuwa zinatekekeza maagizo hayo kama marobot. Sasa hivi kuna vaccines za corona ila tunaambiwa kwamba nchi za kiafrika zitaanza kupata dose zake kuanzia labda mwishoni mwa mwaka 2021.

Nchi inayojitambua na kama unajitambua huwezi kuweka tumaini lako kwenye vaccine za corona ili kupambana na corona. Magu kashasoma hilo gemu lote na yupo sahihi kusema kwamba maisha ya watanzania kwenye corona version 1 hayakusubiri vaccine, na pia hayatasubiri vaccine kwenye corona version 2. Ni upuuzi kutegemea corona vaccine unayoweza kuipata mwaka 2022. Ina maana basi maisha hayataendelea hadi tusubiri vaccine ya 2022 tena wanayotuchagulia wao? Umaskini wa fikra ni umaskini mbaya sana.
Paragraph ya pili ni UONGO ili kuhalalisha hoja yako. Kama wadau walivyotangulia kusema, huo wivu wa mabeberu kwa nini tusiuone kwenye chanjo za polio, TB, dawa za ARV nk
Nakubaliana na hoja ya kujiridhisha na ubora wa chanjo, lakini hoja ya eti mabeberu wana wivu na sisi, ina ukakasi mkubwa kwa sababu kila tulichonacho, siyo sisi pekee tunavyo(madini, rasilimali za asili, bahari, maziwa nk)!
 
Kama kuna kitu ananifurahisha sana mhe rais basi ni issue hi ya Corona; hu ugonjwa upo na unaua sana but kwa huku kwetu unaua basi sio kiviiile kama huko kwenye hizo nchi za weupe; huko kwa weupe, corona imeua na inaua sana hadi sasa hivi, swali kwanini msukumo wa chanjo unaelekezwa sana Africa ambako hakuna athari kubwa sana kama huko kwao?
Ebora iliua sana Guine na Congo but je WHO walipiga kelele kama sasa? Jibu ni HAPANA, why hawakupiga kelele kama sasa? Ni jibu lipo wazi, ugonjwa umeua weusi na sio weupe, Ebora ingekua imeanzi kwao, kelele nyingi sana zingepigwa but ilianzia Africa, haikufika Ulaya na Marekani na labda China na Japan. Napenda pia msimamo wa rais, rais anao msimamo wake na haangalii wengine wanacho kisema.
Paragraph ya pili, PROPAGANDA TUPU, hivi ni kwa faida ya nani?
 
Paragraph ya pili ni UONGO ili kuhalalisha hoja yako. Kama wadau walivyotangulia kusema, huo wivu wa mabeberu kwa nini tusiuone kwenye chanjo za polio, TB, dawa za ARV nk
Nakubaliana na hoja ya kujiridhisha na ubora wa chanjo, lakini hoja ya eti mabeberu wana wivu na sisi, ina ukakasi mkubwa kwa sababu kila tulichonacho, siyo sisi pekee tunavyo(madini, rasilimali za asili, bahari, maziwa nk)!
Mi bado sijaelewa lengo la kutumia chanjo za polio, TB au dawa za ARVs kama counterargument kwamba ubeberu wanatumia pandemic ya corona kujineemesha zaidi kupitia vaccines zao. Ni kweli chanjo ya polio ilitusaidia, ni kweli dawa za ARVs zimesaidia sana tu. Ni makosa makubwa ya kimkakati kwamba hatukujifunza kutengeneza dawa zetu na kwamba miaka mingi baadaye bado tunaendelea kuwategemea wazungu kwa ajili ya afya za watu wetu.

Magufuli anachosema, au ninachojaribu kukisoma kupitia attitude ya Magufuli (na wale wanaomsupport) kuhusiana na corona, ni kwamba enough is enough! -- Tanzania haitaki kuendelea kuwa tegemezi wa Magharibi kwenye mambo yanayohusu afya ya watu wake, na kwenye mambo mengineyo pia. Hatua ya kwanza ni kusema HAPANA kwenye inshu ya chanjo ya corona. Kusema hapana huku, kutatufanya, kwanza, tupambane na corona kwa namna yetu iliyo ndani ya uwezo wetu. Pili, kutatujengea uzoefu wa nini cha kufanya janga kama hili likitokea tena. Kama miongoni mwa uzoefu huo ni kuona umuhimu wa kujijengea uwezo wa kutengeneza chanjo zetu wenyewe, well and good!

Kitu ambacho watu kama nyie mnakiadvocate ni kuendelea kuitazama magharibi kama baba yenu na Mungu wenu kwenye mambo yanayohusu mambo yenu. Yaani mmeifanya Marekani na Ulaya kama one-stop-shop kwa matatizo yenu yote, na kwenda kinyume na kile wanachokifanya, au wanachokisema basi unaonekana umekosea, dah! Maana halisi ya uhuru ni doing your own thing eti. Viongozi wa nchi hii wenye fikra kama zako ndio wameirudisha hii nchi nyuma sana.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom