#COVID19 WHO inasimama na mataifa ya Afrika, chonde chonde msifunge mipaka

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Wakati idadi ya nchi zinazotangaza marufuku ya safari za ndege kwa mataifa ya Kusini mwa Afrika ikiongezeka kutokana na hofu ya aina mpya ya virusi vya COVID-19 vya Omicron, shirika la afya la Umoja wa Mataifa ulimwenguni WHO leo limezisihi nchi kufuata sayansi na kanuni za kimataifa za afya za mwaka 2005.

Kwa mujibu wa taaifa ya WHO iliyotolewa leo mjini Brazzaville vizuizi vya usafiri vinaweza kupunguza kidogo kusambaa kwa COVID-19 lakini vitaweka shinikizo na mzigo mkubwa katika maisha na riziki za watu.

Limeongeza kuwa “Endapo vizuizi hivyo vinatekelezwa, basi visiwe vya uvamizi au kuingilia bila ulazima, na vinapaswa kuzingata misingi ya sayansi, kulingana na Kanuni za afya za kimataifa ambazo ni chombo kinachofunga chini ya sheria za kimataifa na kinachotambuliwa na zaidi ya mataifa 190. Wiki hii, mataifa yatashiriki kikao maalum cha Baraza la Afya Duniani, kilichoandaliwa na WHO kujadili jinsi ya kujiandaa kwa pamoja na kukabiliana vyema na milipuko huu mpya, kwa kuzingatia ahadi zao kwa kanuni za afya za kimataifa.”

Afrika Kusini ilifuata kanuni za afya za kimataifa na punde tu maabara yake ya kitaifa ilipotambua lahaja ya Omicron ililiarifu shirika la WHO kuhusu mlipuko huo tarehe 24 Novemba.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti amesema “Kasi na uwazi wa seŕikali za Afŕika Kusini na Botswana katika kuufahamisha ulimwengu juu ya aina hii mpya ya virusi inastahili kupongezwa. WHO inasimama pamoja na nchi za Kiafrika ambazo zilikuwa na ujasiri wa kushiriki kwa ujasiri habari za kuokoa maisha za afya ya umma, na kusaidia kuilinda dunia dhidi ya kusambaa kwa COVID-19.

Katika mkesha wa kikao maalum cha kujitayarisha kwa janga hili, ninahimiza nchi zote kuheshimu majukumu yao ya kisheria na kuzingatia masuala ya kisayansi kwa afya ya umma. Ni muhimu kwamba nchi ambazo ziko wazi na takwimu zao ziungwe mkono kwani hii ndiyo njia pekee ya kuhakikisha tunapokea takwimu muhimu kwa wakati ufaao.”
Mtoa huduma wa kujitolea anayeitwa Trinity anafanya kazi katika hospitali ya COVID-19 huko Nasrec, Johannesburg.

Mtoa huduma wa kujitolea anayeitwa Trinity anafanya kazi katika hospitali ya COVID-19 huko Nasrec, Johannesburg. IMF/James Oatway

Tuchukue tahadhari na kuweka mikakati ya kujilinda​

Wakati uchunguzi ukiendelea kuhusu laina hii mpya ya virusi ya Omicron, WHO inapendekeza nchi kuchukua mtazamo wa kisayansi na mbinu zinayozingatia hatari na kuweka hatua ambazo zinaweza kuzuia uwezekano wa kenea kwa virusi hivyo.

Marufuku ya safari za ndege imewekwa kwa nchi za kusini mwa Afrika, lakini hadi sasa ni nchi mbili tu ambazo zimegundua luwepo wa aina hiyo mpya ya virusi.

Wakati huo huo kuna nchi katika kanda zingine ambazo zimeripoti kesi za Omicron.

Dkt. Moeti amesisitiza kwamba "Pamoja na aina hiyo ya Omicron ya viruzi iliyogunduliwa sasa katika maeneo kadhaa ya dunia, kuweka marufuku ya kusafiri ambayo inalenga Afrika inashambulia mshikamano wa kimataifa. COVID-19 hutumia vibaya migawanyiko yetu kila wakati. Tutaweza tu kuvishinda virusi hivi iwapo tutashirikiana kutafuta suluhu.”

WHO inaongeza usaidizi katika ufuatiliaji wa masuala ya genomic barani Afrika. Maabara za masula hayo zinapaswa kupata rasilimali watu za kutosha na vifaa vya upimaji ili kufanya kazi kwa uwezo wake kamili.
Muhudumu wa afya akiandaa chanjo ya COVID-19 katika hospitali mjini Moghadishu Somalia

Muhudumu wa afya akiandaa chanjo ya COVID-19 katika hospitali mjini Moghadishu Somalia © UNICEF/Ismail Taxta

WHO imesema iko tayari kusaidia mahitaji ya ziada ya rasilimali watu pamoja na kuhamasisha fedha na utaalamu wa kiufundi ili kuimarisha shughuli za kukabiliana na COVID-19 ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji, matibabu na kuzuia maambukizi na ushiriki wa jamii katika nchi za kusini mwa Afrika.

Kwa kuongezea, WHO imesema inafikia nchi zote katika Kanda ya Afrika ili kuhakikisha zinapokea rasilimali muhimu kuweza kugundua na kujiandaa kwa uwezekano wa wagonjwa wa Omicron.

WHO inazitaka nchi kuchukua hatua muhimu ili kuimarisha juhudi za kufuatilia virusi vya Omicron, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa vifaa vyao vya kupima PCR vinaweza kuibaini, kuongeza sampuli zao na mpangilio wa sampuli za vipimo vya COVID-19 kwa angalau mara mbili hadi sampuli 150 kwa wiki kutoka kwenye idadi ya sasa ya wastani wa watu 75, na kukagua sampuli za awali kwa ajili ya dalili zinazowezekana kuwa ni za Omicron.

Mwezi Septemba 2020, WHO na vituo vya Afrika vya kudhibiti na kuzuia magonjwa vilizindua mtandao wa maabara 12 ili kuimarisha ufuatiliaji wa genome wa virusi.

Ufuatiliaji wa genome umesonga mbele kwa kiasi kikubwa tangu kuanza kwa mwaka 2021, huku bara hilo la Afrika likirekodi ongezeko la mara tano la idadi ya mpangilio wa genome.

UN Swahili
 
Muhudumu wa afya akiandaa chanjo ya COVID-19 katika hospitali mjini Moghadishu Somalia UNICEF/Ismail Taxta

Corona Ni Illusion;
 
Kiherehere chao....na wakome. Walitaka kupata sifa ...watu hawawezi kutengeneza chanjo, wanajifanya wamegundua variant.

Wangeacha Denmark, na German au Australia watangaze..na wasingefunga safari za ndege

Ona Sasa Ramaphosa anatoa mlio wa huzuni...Peak holiday season inapotea... serikali inapoteza billion $$$
 
Back
Top Bottom