WHO: Hatushangai kuona maambukizi ya kwanza ya homa ya nyani (Monkeypox) kutoka kwa binadamu kwenda kwa mbwa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Shirika la Afya Ulimwenguni limesema kuwa halijashangazwa na ripoti ya kwanza iliyotolewa hivi karibuni inayoonesha kuwa mbwa ameambukizwa ugonjwa wa homa ya nyani kutoka kwa binadamu aliyekuwa anaishi naye.

Kwa mujibu wa Dr. Rosamund Lewis, kiongozi wa jopo linalofuatilia kwa ukaribu ugonjwa huu kutoka WHO amesema kisa hiki kilichotokea huko Paris ni kipya kuwahi kudhihirika duniani, lakini hakiwashangazi.

Ripoti hii mpya inatoa uthibitisho wa uwezekano wa binadamu kuambukiza wanyama wengine tofauti na zamani ambapo jambo hili lilionekana kama nadharia.

Kituo Cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa cha Marekani (CDC) kimefanya mabadiliko madogo kwenye mwongozo wake wa kudhibiti ugonjwa huu kwa kuweka wazi kuwa maambukizi kutoka kwa binadamu kwenda wanyama sasa yanawezekana, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari.

WHO, CDC pamoja na Taasisi mbalimbali za kimataifa zinaendelea kufuatilia kisa hiki lakini kwa hatua ya sasa, wanyama waliokutana na mtu yeyote aliyeambukizwa ugonjwa huu wanapaswa kutengwa kwa siku 21 huku wakifuatiliwa kwa ukaribu.

Jarida la kitabibu la The Lancet ndilo lilichapisha ripoti ya kisa hiki kwa mara ya kwanza Agost 10, 2022.

Ugonjwa huu unaofanana na tetekuwanga uligunduliwa kwa mara ya kwanza duniani mwaka 1958.

Chanzo: CNN
Utafiti: The Lancet
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom