Who are they: Mbowe, Sitta, Slaa, Zitto, Mwakyembe, Kubenea, Lissu, Rostam...

Admin na Mod

hivi inaruhusiwa kuweka matokeo ya coursework na exams alizofanya mheshimiwa Freeman Mbowe kule Hull university hapa kwenye forum?

sitaki kuweka vitu kisha baadae nikafungiwa

please advice
 
Matokeo ya mitihani huwa ni siri kati ya chuo na mwanafunzi. Hata waalimu huwa hawajui performance ya mwanafunzi zaidi ya somo wanalomfundisha. Je wewe uliyapataje, unafanya kwenye ofisi ya registrar? Kama uko huko kwenye ofisi ya registrar, huoni kuwa utakuwa uanvunja mwiko wa kazi yako?

Au labda, je huko Uingereza matokeo huwa yanatangazwa hadharani kama matokeo ya form 6 pale Tanzania? Kama hutolewa hadharani namna hiyo basi huna kosa lolote kuyaleta hapa kwa vile siyo siri.
 
kama mna maswali itakuwa vizuri mkimtumia PM Admin kuliko kuanzisha thread, ebu imagine kila mtu ana maswali halafu anaanzisha thread yake hapa itakuwaje ?
Kama amesema its ok kuweka hayo majibu, then wee yaweke akadamnasi tuone !
 
Nashangaa kuona watu wanazungumzia kuhusu upatikananji wa matokeo ya Mheshimiwa Mbowe. Ni habari ngapi huwa zinajadiliwa humu ambazo upatikanaji wake huwa ni kwa njia zisizo sahihi? Mbona watu walikuwa wakitaka kufahamu habari ambazo ni siri kati ya mgonjwa na daktari wake? Jinsi habari ilivyopatikana isiwe issue, swali nije kuiweka hadharani ni sahihi au la!
 
Nashangaa kuona watu wanazungumzia kuhusu upatikananji wa matokeo ya Mheshimiwa Mbowe. Ni habari ngapi huwa zinajadiliwa humu ambazo upatikanaji wake huwa ni kwa njia zisizo sahihi? Mbona watu walikuwa wakitaka kufahamu habari ambazo ni siri kati ya mgonjwa na daktari wake? Jinsi habari ilivyopatikana isiwe issue, swali nije kuiweka hadharani ni sahihi au la!

Kwa sababu aliyeanzisha alianza na swali inabidi lijibiwe na ndio chanzo cha mjadala, kama angeyaweka tu hadharani tungeelekea kwingine kimjadala.
 
well ukiona watu walitaka kujua habari kuhusu daktari na mgonjwa wake ( specifically Amina Chifupa in this case ninavyojua ndio unachoongelea ) ni kwamba, ebu angalia the situation ilikvyokuwa, kafa kifo cha kutatanisha, so suddenly, and no reasonable cause of death could be pictured, ndio maana kila mtu alikuwa stunned na kutaka kujua nini kilichotokea kwa " NATIONAL PUBLIC FIGURE", nilielewa kwamba masuala hayo ni personal but angalia kifo ni cha utata kabisa, sasa katika hali ya mitihani, ukiniambia mtu ambae anaenda shule na inafahamika na yeye ni kiongozi which makes him a public figure, sidhani kama itakuwa busara kama kuweka matokeo yake bila idhini yake mwenyewe, LAKINI ( read and understand carefully here ) ukiniambia mtu ambaye ni PUBLIC FIGURE halafu haijulikani kama anasoma then within no time anatokea hadharani na kusema ana MASTERS OF SOMETHING, come on ! hapo lazima tujue wapi aliposoma, matokeo, jee shule ilikuwa accredited, na mfano wa hawa watu ambao ni public figures na walijitokeza ghafla na vyeti ya elimu ya juu ni kama MREMA, CHITALILO mbunge wa ccm, EMMANUEL NCHIMBI na phd yake feki isiyokuwa na maelezo wapi kasoma na kadhalika.
Nadhani utakuwa umeelewa na kama hujaelewa feel free kuuliza maswali, na pia sio lazima kukubali na mawazo yangu kwani ndio uzuri wa mijadala sio kila mtu ataungana na hoja inayotolea. Mimi sifagilii chama chochote tz bali nafagilia maendeleo ya nchi yangu !
 
bandika matokeo ya kiongozi wetu tuone, ili tujue kama kweli mkuu anatafuna shule au just anazuga tu?


hizi zama za uwazi na ukweli kila kitu kinajadilika tuwekee tujadali. na hasa huyu bwana ambae nilisikia alikuwa na tabia ya utoro.
 
HAINA HAJA kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.ni Ubwege itasaidia nini? Kaa nayo, incase amefeli na chuo kimemrudisha Home, basi tuarifiwe tu na si kutoa matokeo. Nafikili hili linahitaji COMMON SENSE na si kumuuliza Admin even kwa private Email. Does it mean vijana tuliopo UK wote tunafanya vema au....Kama admin/Moderators akipita ktk thread nashauri aifunge...
 
pointless. too aggresive on other people's opinions. let me do u a favor, since u have shown too much pointless thoughts on ur saying above, i wouldnt recommend anybody else to reaf it and instead should ignore it. u see how much that really feels ? its the same way other people just like u said about them.
 
Admin na Mod

hivi inaruhusiwa kuweka matokeo ya coursework na exams alizofanya mheshimiwa Freeman Mbowe kule Hull university hapa kwenye forum?

sitaki kuweka vitu kisha baadae nikafungiwa

please advice

Devil - Utakuwa umeyapata vipi wewe matokeo ya mtihani wa mtu? Huyo aliyekupa, kama ni mfanyakazi wa chuo hicho humtakii mema hata kidogo.

Kama ni Mbowe mwenyewe ndio kakupa, (kwa sababu zake mwenyewe, i.e., kafanya maajabu, straight As), basi huna sababu ya kuomba ruhusa ya kuyabandika hapa. Vinginevyo, linaweza kuwa sokomoko la karne hapa; likiwahusisha chuo, waajiriwa wao, na washikaji wako waliokuwezesha kuyapata hayo matokeo!

Do not even try it, that is my advice.
 
HAINA HAJA kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.ni Ubwege itasaidia nini? Kaa nayo, incase amefeli na chuo kimemrudisha Home, basi tuarifiwe tu na si kutoa matokeo. Nafikili hili linahitaji COMMON SENSE na si kumuuliza Admin even kwa private Email. Does it mean vijana tuliopo UK wote tunafanya vema au....Kama admin/Moderators akipita ktk thread nashauri aifunge...


Nakuunga mkono Chuma,


Haina haja ya kuweka matokeo ya mtu hadharani incase ungelikuwa wewe ungelikubali results zako ziwekwe hadharani?

Admin funga mjadala
 
....mjumbe wa shetani!

....nashangaa ruksa imeombwa.

....hivi masuala ya kishetani yanahitaji ruksa!au ndo kupimana joto!
 
mimi nashauri uyaweke tu, ila ukiyaweka weka na ya watanzania wote wanaosoma hapo Hull. Hii itasaidia katika kumlinganisha Mhe. Mbowe na watanzania wengine, na hapo inajumuisha na matokeo yako wewe mwenyewe, kwani na wewe ni mwanafunzi hapo.

Asante.
 
Ndiyo yaweke wazi, matokeo ya Mtihani sio siri wala nini; hata kwenye neshno websaiti kila leo yanabandikwa; ukiomba kazi wapeleka na matokeo; hakuna noma naona. Itatusaidia kufanya maamuzi mbalimbali kuhusu huyu kiongozi wetu.
Asante.
 
Kama Mhe.Mbowe amefanya vizuri sana akawa wa kwanza kwenye mitihani yake ya mwisho au amefanya vibaya sana na kurudishwa kwa kushindwa kwenye mitihani yake yoyote itakuwa vizuri kufahamu matokeo yake.Kama amepata alama za kawaida haitasaidia lolote tukipatiwa matokeo yake.Tunataka tumjue kwa viyu visivyokuwa vya kawaida sana kwa watu wengine.
 
Tangia pale alipoamua kuomba uongozi wa umma, Mh. Mbowe hana cha mambo binafsi wala nini, kila kinamchomhusu umma un haki ya kufahamu.

Devil, weka matokeo!
 
Back
Top Bottom