Whitney Houston Aibuka Upya, Kutoa Albamu Mwezi Septemba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Whitney Houston Aibuka Upya, Kutoa Albamu Mwezi Septemba

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, Jun 6, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,611
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Whitney Houston
  Nyota wa muziki wa R&B wa Marekani Whitney Houston amerudi tena kwenye ulingo wa muziki kwa kishindo na albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Just Whitney.. ' inatoka mwezi wa tisa. Unapozungumzia nyimbo za miziki ya taratibu na ya kuchombeza huwezi ukaacha kumtaja Whitney Houston kwani Whitney anatambulika kama malkia wa miziki hiyo akiwa miongoni mwa wanamuziki wachache ambao nyimbo zao za zamani bado zinaendelea kutamba hadi leo.

  Whitney Houston mwenye umri wa miaka 45 alilipwa dola milioni 100 na kampuni ya Arista Records ili kutoa albamu yake hiyo mpya ambayo inategemewa kumrudisha kwenye chati za juu za muziki baada ya kutokutoa albamu yoyote katika kipindi cha miaka saba baada ya kudumbukia kwenye dimbwi la utumiaji wa madawa ya kulevya.

  Whitney alionekana kurudi kwenye fomu yake ya zamani pale alipowadatisha wapenzi wake alipopanda jukwaani kuimba kwenye party iliyofanyika kabla ya tuzo za Grammy mwezi februari mwaka huu.

  Pamoja na habari ya albamu ya Whitney kuwa nzuri masikioni mwa washabiki wengi wa muziki duniani, albamu hiyo imeleta uchachu kwenye kampuni ya Arista iliyorekodi albamu hiyo baada ya albamu hiyo kuvuja kwenye internet kabla hata haijatolewa rasmi.

  Wataalamu wa muziki na mambo ya uchumi wanatabiri kwamba kampuni ya Arista Records itazama kama meli ya Titanic ilivyozama baada ya kumlipa Whitney dola milioni 100 halafu ikashindwa kuwazuia wafanyakazi wake wasiivujishe albamu hiyo.

  "Just Whitney.." itakuwa madukani kuanzia tarehe moja mwezi septemba.
   
 2. M

  Mubii Senior Member

  #2
  Jun 12, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani huyu dada ana sauti nzuri sana ambayo nadhani hakuna anayemfikia katika miaka hii ya karibuni. Dunia tumedhulumiwa sana uhondo kwa miaka saba na sasa sijui kama Whitney ataweza kufikia kiwango chake cha zamani. Ama kweli madawa ya kulevya ni adui mkubwa hapa duniani na imeharibu wengi wenye talents nzuri.
   
Loading...